PreGE2025 The Chanzo yaondoa Maudhui ya Askofu Gwajima YouTube Kufuatia wito wa TCRA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Au kile alichosema Gwajima kuwa kuna kikundi ndio kimetoa hayo maelekezo? Basi hicho kikundi ni balaa!
 
Ila ujumbe umefika kwenye hadhira iliyokusudiwa...
Ile Video sasa imeshanyonywa na GenZ wa Kenya jana nilikuwa naiona imefanywa meme katika package ya kumtukana bimkubwa 😂🤣

Too little too late
 
Leo Mei 27, 2025, The Chanzo imepokea wito kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu maudhui ya video tuliyochapisha katika chaneli yetu ya Youtube, ambayo ni mkutano na waandishi wa habari mazungumzo aliyoyafanya Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe (Chama cha Mapinduzi - CCM), mnamo Mei 24, 2025.

Kutokana na mazungumzo hayo kuendelea kufuatiliwa, ili kuboresha uwazi, na imani ya wafuatiliaji wetu, The Chanzo inapenda kuwajulisha wasomaji na wadau wake wengine kuwa imetubidi kuyaondoa maudhui hayo kutokana na wito huo.

Sehemu ya taarifa tuliyopokea kutoka TCRA inaeleza:

"Maudhui hayo yaliyopakiwa na Chanzo Online TV yalikuwa ni maelezo ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Josephat Gwajima, hayakufuata Sheria, Kanuni, Maadili wala Misingi ya Uandishi na Utangazaji wa Habari kutokana na kukosa mizania/kuwa na taarifa za upande mmoja tu bila ya kuwapa nafasi upande wa Serikali au Mamlaka husika kutolea ufafanuzi shutuma au taarifa kuhusu idadi ya watu waliodaiwa kutekwa kama ilivyodaiwa katika taarifa husika. Kitendo cha Chanzo Online TV kupakia taarifa zenye kuegemea upande mmoja kinaweza kuhamasisha au kuchochea chuki dhidi ya Serikali kutoka kwa wananchi wake."

Wakati ni nadra wito wa namna hii kutokea, kutokana na wito huu kutoka TCRA, leseni ya maudhui inatutaka kuyaondoa maudhui hayo; jambo ambalo tumelifanya leo Mei 27, 2025, 10:09 asubuhi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Safi sana!
 
Kama kawaida watu wana comment bila kuingia hata YouTube, video imezagaa YouTube. Hao The Chanzo wanatafuta kiki tu. Video imewekwa YouTube kutoka vyanzo mbalimbali na server tofauti hadi marekani na ulaya. TCRA wanajisumbua tu.
 
Sio wao tu hata Gwajima mwenyewe kaipandisha youtube na Instagram
Ujanielewa,nimeomba kujua,why the chanzo only!?,, Tatizo si kuwapandisha hao jamaa wawili,kwani wao waweze wananini na wengine washindwe wananini? Au wamefeli wapi?
 
Kumbe kuna channel bado wanayo?!
Safi
Zipo nyingi tu, hao TCRA wamechanganyikiwa. Video ikiwa na tatizo lolote unawasiliana na YouTube wenyewe wanajiridhisha na kuifuta wenyewe. Hiyo ya kuamuru hizi online tv zifute ni utoto, mtu yeyote binafsi hata mimi na wewe unai upload kwenye account yako na hawakufanyi kitu. Hiyo video ipo chanel binafsi kibao YouTube sababu haina tatizo lolote kwa mujibu wa kanuni za YouTube. TCRA wanatapatapa wamechanganyikiwa.
 
Basi hao wanaoambiwa wazifute kwasababu ni wanafuasi wengi humo youtube labda
 
Ujanielewa,nimeomba kujua,why the chanzo only!?,, Tatizo si kuwapandisha hao jamaa wawili,kwani wao waweze wananini na wengine washindwe wananini? Au wamefeli wapi?
Asilimia kubwa ya media zimeondoa hayo maudhui na sababu nadhani imetajwa hapo na the chanzo, kwahyo sio the chanzo only media nyingi tu zimefuta
 
Leo Mei 27, 2025, The Chanzo imepokea wito kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu maudhui ya video tuliyochapisha katika chaneli yetu ya Youtube, ambayo ni mkutano na waandishi wa habari mazungumzo aliyoyafanya Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe (Chama cha Mapinduzi - CCM), mnamo Mei 24, 2025.

Kutokana na mazungumzo hayo kuendelea kufuatiliwa, ili kuboresha uwazi, na imani ya wafuatiliaji wetu, The Chanzo inapenda kuwajulisha wasomaji na wadau wake wengine kuwa imetubidi kuyaondoa maudhui hayo kutokana na wito huo.

Sehemu ya taarifa tuliyopokea kutoka TCRA inaeleza:

"Maudhui hayo yaliyopakiwa na Chanzo Online TV yalikuwa ni maelezo ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Josephat Gwajima, hayakufuata Sheria, Kanuni, Maadili wala Misingi ya Uandishi na Utangazaji wa Habari kutokana na kukosa mizania/kuwa na taarifa za upande mmoja tu bila ya kuwapa nafasi upande wa Serikali au Mamlaka husika kutolea ufafanuzi shutuma au taarifa kuhusu idadi ya watu waliodaiwa kutekwa kama ilivyodaiwa katika taarifa husika. Kitendo cha Chanzo Online TV kupakia taarifa zenye kuegemea upande mmoja kinaweza kuhamasisha au kuchochea chuki dhidi ya Serikali kutoka kwa wananchi wake."

Wakati ni nadra wito wa namna hii kutokea, kutokana na wito huu kutoka TCRA, leseni ya maudhui inatutaka kuyaondoa maudhui hayo; jambo ambalo tumelifanya leo Mei 27, 2025, 10:09 asubuhi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

TCRA bana. 🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom