Ashasembeko
JF-Expert Member
- Dec 14, 2017
- 225
- 910
Katika mchakato huu wa uchaguzi, vyombo vya habari, hasa magazeti yamekua yakikemewa kwa kuonesha upendeleo kwa CCM, na ni ukweli. Pamoja na mazingira hatarishi ya kufanya kazi zao, baadhi ya vyombo hivi vimejitahidi kutoa habari zinazotoa uwanja sawa kwa vyama vyote na kuripoti matukio nyeti yanayozua mjadala mtandaoni.
Chombo cha kwanza kinachostahili pongezi ni Gazeti la The Citizen - na nitatoa mifano.
Katika nakala yake ya tarehe 13/08/2020, ndio gazeti pekee lililoripoti habari ya njama za Tume ya Uchaguzi kuwa na mpango wa kuengua wagombea wa upinzani, na hii habari ilikua katika kurasa zake za mbele. Isome hapa.
Pia hili gazeti na kidogo, Mwananchi ndio magazeti pekee yalithubutu kuweka habari za Lissu kwenye kurasa zake za mbele. Mfano ni nakala ya tarehe 11/08/2020, ambalo waliripoti habari ya Lissu kutolipa kisasi. Soma hapa. Pia, the Citizen ndio gazeti pekee lililoripoti ujio wa Lissu nchini, Lissu kuteuliwa na Chama chake na Lissu kwenda kuchukua fomu Dodoma na kuziweka habari zote front page.
Kama mtakumbuka, ni gazeti pekee lililorepoti Habari ya Msajili wa vyama vya siasa kutanga kukifungia ACT Wazalendo
Ukiondoa Habari za siasa, gazeti la The Citizen pia, ndio gazeti pekee lililoripoti habari ya TCRA kuweka kanuni mpya, na kwenye hiyo Makala ikaweka mawazo mengi tu ya wakosoaji wa serikali. Pia ni gazeti lililorepoti Habari ya TCRA kuvitaka vyombo vya kimataifa kuomba leseni ili kufanya kazi na vyombo vya ndani ya nchi. Pia iliripoti habari ya Tume ya Uchaguzi kuengua mashirika kuu yasiyo ya kiserikali (NGOs) katika mchakato wa kusimamia uchaguzi.
Na Habari zengine nyingi sana. Mwananchi pia imejitahidi, ila nahisi The Citizen, limekua more objective, nahisi labda ni kwa sababu la kiingereza ndio maana watawala hawahangaiki nalo. The Guardian, limekua gazeti la hovyo kusema ukweli. Hata Habari zao hazina depth, sijui ni aina ya waandishi wao. Yaani inasikitisha, The Guardian ya enzi zile za Mengi wakati wa JK, ndio lilikua moto kweli, sa hizi limekua too shallow.
Leo pia kama mmegundua magazeti binafsi takribani yote yameripoti Habari ya kanisa la TAG kutaka uchaguzi wa huru na haki. Hili ni la kupongezwa pia, nilitegemea kama kawaida yao wangemuweka JPM kama cover story. Ni ujumbe mzuri mnatuma kwa wananchi nawapongeza na kuwapa moyo muendelee kuwa hivyo. Tuwape support tununue magazeti yao, kama tunavyowakosoa wakionyesha upendeleo.