Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,081
- 2,325
Moja ya tatizo kubwa linalozikabili nchi za kiafrika ni kuganga njaa kwa kutumia kivuli cha siasa. Baada ya uchàguzi viongozi wa vyama vya siasa huendelea kuzunguka huku na huko kwa wa mgongo wa siasa ili kuhalalisha utumiaji wa fedha za ruzuku kwa kile kinachoitwa kuimarisha chama au kukosoa yale yanayofanywa na serikàli. Lakini wajue kuwa ukosoaji wa serikali nje ya taratibu rasmi za kikatiba hauleti matokeo yoyote chanya kwa serikali iliyopo madarakani kujirekebisha. Ukosooaji bora baada ya uchaguzi hutakiwa kufanyika bungeni. Ndio maana Kafulila alipoamua kuikosoa serikali kuhusu escrow, alifanya hivyo bungeni na matokeo yake yanajulikana.
Hakuna uhuru usio na mipaka.
Professoer amejikita kuhusu uhuru wa kisiasa, mbona hayaoni mengine yanayofanywa na uongozi wa sasa? Anataka nchi iendelee kutawaliwa na nguvu mbili. Moja iliyoshinda uchaguzi na inaendeaha serikali na nyingine iliyoshindwa ikiendesha maandamano.
Haiwezekani zizi likatawaliwa na fahari wawili.