The dark side of business

The dark side of business


JamiiForums

Inaendelea................

Kuna uzi wangu niliutupia hapa unasema"experience ya miaka 15 ya kijiajiri(nadiriki kusema business is a sure way onto true riches)"kwenye huo uzi sikuelezea hiyo miaka 15 nilikuwa nafanya mishe gani, simply ilikuwa ni mishe ya vocha(wholesale)

Sasa baada ya kumaliza six,nilirudi mtaani na harakati za biashara zikaanza rasmi,kuna biashara ndogo nilianzisha lkn mawazo yangu yalikuwa ni mishe ya vocha za jumla, sema mtaji ulikuwa kipengele,so nikavutavuta siku mpk naingia chuo,ile biashara mdogo ilienda poa kimtindo,kuna dogo nilikuwa namwacha shop,mm naendelea na kitabu,nikapata boom(kwny intake yetu tulichelewa kupata,so tukapewa lumpsum ya mwaka mzima ilikuwa Kama 2.4M),chap nikaigeuza kuwa mtaji wa Biashara ya ndoto zangu,hii biashara ya vocha ni kama Biashara ya mafuta,faida yake ni ndogo sana lkn ukiuza mzigo mkubwa faida unaiona,kipindi hicho hii mishe ilikuwa 🔥 🔥 ila now days ni ya kawaida sana,kuuza mzigo wa milioni 5 kwa siku ilikuwa ni jambo la kawaida,nilichanganya shule na biashara kwasababu sikuwa na gutts tena za kusubiri mpk nimalize.
Chuo kilipoisha,
Kwa kweli sikuwa hata na chembe ya kutafuta ajira ijapokuwa matokeo yalikuwa mazuri,washkaji niliomaliza nao walikimbilia ajira,mimi nikaingia rasmi kwenye biashara ya vocha za jumla, wakati namaliza chuo mtaji ulikuwa kama 3M hv lkn ndani ya miezi sita mtaji ukafika 10M miezi sita mingine ikafika 20M,kwa waliofanya mishe hii backdays wanajua kama ukiuza mzigo wa milioni basi faida ni elfu 20,nilikuwa nauza mpk 8M kwa siku,kukunja laki hadi laki na nusu perday ilikuwa kawaida,dat time nikanunua kiwanja,nikajenga maflemu kama nane,then kwa nyuma niliplan kujenga apartments za kupangisha,nilinunua hiace(daladala)ili nitanue wigo,it was amazingl!coz I was just 23,nikazidi kusema "business is a quickest way onto riches" ila sikujua kuwa business is also a riskiest way onto riches,kwa ufupi ile side A ya biashara niliimaster ipasavyo,nilipiga kazi sana mpk watu wakahisi natumia ndumba,kwasababu ofisini watu walikuwa wanajaa,foleni kama nmb,hakika biashara na maisha kwa ujumla viliniendea poa,mtaani kila mtu alitamani afanye biashara kwakile alichokiona kinatokea kwangu,nilitengeneza jina kwa muda mfupi sana ghafla yakaanza mapicha picha,mara nikute damu kwny kiti ninachokalia pale ofisini,Mara hirizi,pesa zikawa zinapotea kimazingara,hua siamini uchawi lkn hiki kilichokuwa kinatokea ni uchawi bila chenga,nilifukuza wafanyakazi lkn haikusaidia(nilihisi wananipiga)nilipiga moyo konde lkn changamoto zilizidi to the extent nikaanza kuogopa biashara,kwa kweli nilibaki njia panda,ila Kuna wazo likanijia,juu ya nini cha kufanya......................
*****************************
Biashara zina ups and downs,niliona upande mmoja,sasa dunia inanionyesha upande wa pili,nini kitaendelea baada ya kupata wazo.............usikose
Lamomy mganga wako pale Ukinga hajambo?
 
Ni ngumu sana kwangu kuamini kwenye uchawi kwasababu ni dhana ambayo haijathibitishwa kisayansi....

Lakini potelea pote...

Wewe kuamini uchawi hakuniathiri mimi kwa namna yeyote.

Na kama ulivyosema, siwezi kujua kila kitu.

Ubishi ni lazima kwasababu hata mimi nikileta mada yangu inayopinga uchawi, mnaoamini mtaona nakosea, mnavuta upande wenu.

Hili jambo ni gumu kuliko tunavyolichukulia mkuu
Hakuna sehemu yoyote nimesema ninaamini uchawi, nilichosisitiza ni kuacha room ya majadiliano kwenye mada husika na sio KUBISHA kama ulivyosema.

"Badala ya KUBISHA, mhoji akuthibitishie"


NB: Comment yako imeibua swali fulani, ninaomba nikuulize:-

Je, unaamini kwamba KILA KITU kilichopo duniani kinaweza kuthibitishwa na kuelezewa kisayansi bila kuacha chembechembe za uncertainties,na kwamba sayansi ndio njia pekee?

Maana umesema kamwe huwezi amini kitu ambacho hakijathibitishwa kisayansi.
 
hivyo vitu vingine hawawezi kukuambia abadani, wewe utaona sijui management sijui kitu gani, e.t.c ! Ili udumu kwenye biashara na mafanikio lazima ujue Siri Za Ulimwengu wa Roho na uwe kwenye upande mojawapo kati wa hizi ( Ulimwengu wa Nuru au Ulimwengu wa Giza). Hakuna biashara inayofanikiwa yenyewe bila kuwa na nguvu zinaendesha hizo biashara.

Naomba nikuulize swali! Je wewe Unamiliki biashara yako kama kampuni?, Real estates? au hata hizi za kawaida?

Kama Bado una long way to go kujua Siri za biashara katika ulimwengu wa roho ili uweze Ku sustain! Na hichi ndicho huwezi kufundishwa Shule.

Usije ukaingia kwenye biashara kichwa kichwa kesho unatembea na boxer siku pale unapoona 50M, 200M zinapokatika kama maji ndani ya 3 months..e.t.c
Hakika ambao awajui ndo wanabisha kuna kampuni ya wazungu kuna jamaa walitumwa mayai ya bundi walipoyapata walipewa ml 40 sasa wapi yanaenda haijulikani hiyo watu wakae kwa kutulia wajifunze elimu isiyofundishwa darasan
 
Hao waganga wa kienyeji watumie huo uganga wao kwa nguvu zako zote wawazidi matajiri wakubwa kama kina Aliko Dangote, Bakhressa, Mo Dewji na wengineo.

Hao waganga ndio makapuku nambari moja maskini choka mbaya wanaishi kwenye vibanda vya udongo.

Halafu wajinga kama wewe unaamini mganga huyo ndio ataweza kukupatia utajiri!!!

Maisha si rahisi hivyo wewe!!
The world doesn't work like that my friend, everything have off-limits
 
The world doesn't work like that my friend, everything have off-limits
Unajifanya kuijua sana dunia, Lakini ukiambiwa uthibitishe uwepo wa huo utajiri wa kishetani unaanza stori mara oh nilisimuliwa na jamaa fulani, mara mzee fulani, mara kilipanda kikashuka.
 
Vp na wale wanaoenda kutoa kaafara za kuku. Naona pia inaunganishwa kwa roho za watu bila mtu kujua
Kwa ulivyo uliza swali. Majibu yategemeana na scenario husika
KUna kundi wao hua wanaiamini mizimu au wanaabudu mizimu ili wafanikiwe katika shughulizao iwe biashara au kiliomo au ishu yyte inayoitaji mtu kufanikiwa

Sasa damu hua ni kama sadaka kwani ndo chakula cha mizimu. Hua ni damu ya mifugo iwe ng'ombe au kuku.

ASsignment au mfano mzuri na kupa katafte na wewe u reason kuendana na uelewa wako. Kama hukufuatilia kwa makini live katafte interview na clip za kipind icho

Kipindi cha miaka 10 ya muziki ya msanii Bayamundi alienda kwao kigaoma na msanii kharmonize yeye akaamua kwenda kwao mtwara.
Kuna swali mtangazaji miliOmmY alimuuliza bayamondi kua
"Kipindi tunafika hapa kigoma kuna ndege sijui ni popo wale walikua wametanda wengi kweli kwenye ule mti ila wewe ulivyo fika au kutia mguu walipaa wakaondoka hii hali ili ibua maswali sana Kgoma

Majibu ya bayamundi " sipendi kuliongelea hilo swala ila wazee na wakubwa wamenikubali"
katafte mwenyew video za kipindi hicho
Kwa ufupi mifugo ilichinjwa sana baina ya wasnaii hao


View: https://youtu.be/b7pM3kO3Ml0?si=TELIJbMgJBRPiGIa

View: https://youtube.com/shorts/R7A7Gk7lwnE?si=F9cnc40CEtujAB8e

Kwa upande mwngine
Kuna wale wanao enda kwa watalaam kwa lengo la kutafta utajiri. Huwa wanaambiwa watoe kafara ya mtu wa karibu au ndugu sasa hapo mnyama kama kuku ndo anakuwa ana represent huyo mtu alietolewa sadaka. Kuku akichinjwa basi kitakachomkuta huyo mtu kimetokana tendo na sadaka alioitoa

Life is spiritual. Mafanikio ya mtu we yaache kama yalivyo hujui effort na hustle alioiweka mpka kafika hapo
 
Unajifanya kuijua sana dunia, Lakini ukiambiwa uthibitishe uwepo wa huo utajiri wa kishetani unaanza stori mara oh nilisimuliwa na jamaa fulani, mara mzee fulani, mara kilipanda kikashuka.
Ni hivi rafiki.... duniani tuna pande mbili tu, ni kwa Mungu au shetani... hakuna upande wa sayansi.... wewe upo wapi?....nao wote wasemao mimi ni sayansi, Mungu au shetani hawapo....hao ni wafuasi wa shetani,... Kwa sababu wameisikia kweli nao wameikataa na kufuata mawazo ya mioyo yao ambayo ni upotofu.
 
Ni hivi rafiki.... duniani tuna pande mbili tu, ni kwa Mungu au shetani... hakuna upande wa sayansi.... wewe upo wapi?....nao wote wasemao mimi ni sayansi, Mungu au shetani hawapo....hao ni wafuasi wa shetani,... Kwa sababu wameisikia kweli nao wameikataa na kufuata mawazo ya mioyo yao ambayo ni upotofu.
Mungu na shetani hawapo.

Mungu na shetani mmewatunga vichwani mwenu wala huwezi kuthibitisha uwepo wao.
 
Unajifanya kuijua sana dunia, Lakini ukiambiwa uthibitishe uwepo wa huo utajiri wa kishetani unaanza stori mara oh nilisimuliwa na jamaa fulani, mara mzee fulani, mara kilipanda kikashuka.
Mkuu, huwezi kua na experience ya kila kitu, hivo haipaswi kumbishia mtu mwenye experience ya jambo fulani ambalo wewe huna experience nalo.
 
Hakuna sehemu yoyote nimesema ninaamini uchawi, nilichosisitiza ni kuacha room ya majadiliano kwenye mada husika na sio KUBISHA kama ulivyosema.

"Badala ya KUBISHA, mhoji akuthibitishie"


NB: Comment yako imeibua swali fulani, ninaomba nikuulize:-

Je, unaamini kwamba KILA KITU kilichopo duniani kinaweza kuthibitishwa na kuelezewa kisayansi bila kuacha chembechembe za uncertainties,na kwamba sayansi ndio njia pekee?

Maana umesema kamwe huwezi amini kitu ambacho hakijathibitishwa kisayansi.
mahojiano mara nyingi yanaishia kwenye mabishano, haswa kwenye mada nyeti kama hizi

inafika mahali hisia zinaanza kuhusika

siamini kwamba kila kinathibitishika, lakini kuna vile nina uhakika havipo, ikiwemo uchawi kama tuujuavyo
 
Watu wasikokijua ni kwamba hao ng'ombe ni watu. Inaitwa nguvu ya sadaka katika utajiri. Siku moja nitawaletea na mimi uzi nawajuze siri iliyomo ndani ya sadaka. Hasa ile yakuumiza moyo.
Hapo sasa ndo huwa nachoka kabisa hawa waganga,anakusababisha unatoa kafara ya damu ya mtu pasipo kujua kwanini wengine huwa hawasemi

Kuna jamaa aliambiwa akapasue gogo atoe vipande vya kuni,ile anapasua akashangaa gogo linatoa damu,alivyomaliza mambo yake kwa mganga akapigiwa simu kutoka nyumban anaambiwa mama ake kafa

Ndo kama huyu ndugu yetu mwenye uzi,yeye alitaka kinga lakin mganga kampeleka mpaka kwenye kafara
 
Back
Top Bottom