The dark side of business

The dark side of business

Hakuna shule hakuna chuo utafundishwa kuhusu dark side of anything,Kuna njia mbili tu za kujua wasichokijua watu wengi,njia nyepesi zaidi ni kujua kupitia shuhuda za watu waliopita kwenye kivuli cha mauti na wakatoka salama na njia ngumu zaidi ndio Kama niliyopitia Mimi,i dip my feet into the ways of darkness.

Angalizo
Hiki ninachoandika ni experience ya miaka mingi nyuma, now mimi ni mtu safi,i believe in G-d na kwa kila nnachofanya i pray for his guidance.

Lengo la uzi
Nataka ujue upande wa pili wa shilingi,the dark side of business,uujue ulimwengu wa kiroho wa Biashara kwasababu huko ndio karata zinachezwa huko ndio kete zinasukumwa,sitaki upite dark side nataka upite light side(G-d side) kwasababu mafanikio bila giza yanawezekana.

This is my story
Nikiwa advance kwenye mkoa mmojawapo wa kanda ya ziwa,hapo shule nilipangwa room moja na machalii wawili kutoka A town na Kama unavyojua spirit ya wachaga wengi ni Biashara so ikawa story nyingi ni kuhusu biashara,chalii mmoja(tumwite fabi)ndio alikuwa moto sana na issue za biashara,kwasbb baba yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa sana huko chuga,so jamaa alitamani kuvaa viatu vya baba yake.
Mzee wa fabi alikuwa ana hardware mbili kubwa town na nyumba za kutosha,alikuwa ni realestate guru,simply huyu mzee alikuwa tajiri,Kuna likizo tulienda chuga ili nipate mawili matatu kuhusu biashara.

Mzee fabi:ahaa wewe ndio rafiki yake fabi
Mm:ndio mzee,
Fabi:huyu ndio yule rafiki yangu niliyekuambia anapenda kufanya biashara
Mzee fabi:sawa,karibu sana kijana ila someni hizi Biashara mtazikuta tu,sisi hatukusoma lkn hesabu za Biashara tunazijua...(wote tukacheka)then mzee akaondoka akaenda kwenye mishe zake.
siku iliyofuata fabi alinizungusha kwenye miradi ya mzee,alikuwa na lodge 3,semi mbili na nyumba za wapangaji za kutosha,I was amazed!nikasema hakika business is a sure way onto riches,nilitamani nianze mishe za biashara hata kabla sijamaliza shule,kichwa iliwaka moto,baada ya likizo tulirudi shule nikiwa na vibe la kutosha.

Tukiwa shule
Tukawa tunaulizana tukimaliza shule tufanye issue gani!,fabi akawa anasema akimaliza anataka kuuza vocha za jumla(vocha za mitandao ya simu)mimi nikawa nasema nataka kuuza mafuta(dealer wa hizi cooking oil) so siku moja tukaenda town(shule yetu ilikuwa porini,ndani ndani) lengo la kwenda town ilikuwa ni kufanya utafiti wa hizo mishe tulizoplan kuzifanya,hapa nieleze ujanja flani aliotufundisha mzee wake fabi"ukitaka upate wazo zuri la Biashara angalia customer Queueing" akimaanisha angalia biashara inayotengeneza foleni ya wateja,isee huyu mzee hajasoma lkn alikuwa na nondo Kama za rich dady😃
Sasa huwezi kuamini tulizura pale town kucheki hizo mishe Kama zinatengeneza foleni ya wateja,kwanza tuliona maduka mengi yanayofanya mishe hizo ni ya wahindi(huko mbele nitakuja kueleza dark side ya hawa jamaa hapa bongo,Wana hadi kitabu maalumu cha namna ya kumpiga pin mtu mweusi awe Kama working machine)hawa jamaa kwa sehemu wametuzidi kete(kete za kiroho)....maduka mengi makubwa yalikuwa yao na kweli ile mishe ya vocha tuliona ina foleni si ya kitoto hadi na mm nikashawishika ku abort mishe ya mafuta!niingie kwny vocha.
*****************************

Wadau itabidi nigusie issue muhimu tu ili gazeti lisiwe refu,Sasa nini kitajiri baada ya kumaliza six na kuingia rasmi mtaani..........nitarudi
***************************
Inaendelea.................

Kuna uzi wangu niliutupia hapa unasema"experience ya miaka 15 ya kijiajiri(nadiriki kusema business is a sure way onto true riches)"kwenye huo uzi sikuelezea hiyo miaka 15 nilikuwa nafanya mishe gani, simply ilikuwa ni mishe ya vocha(wholesale)

Sasa baada ya kumaliza six,nilirudi mtaani na harakati za biashara zikaanza rasmi,kuna biashara ndogo nilianzisha lkn mawazo yangu yalikuwa ni mishe ya vocha za jumla, sema mtaji ulikuwa kipengele,so nikavutavuta siku mpk naingia chuo,ile biashara mdogo ilienda poa kimtindo,kuna dogo nilikuwa namwacha shop,mm naendelea na kitabu,nikapata boom(kwny intake yetu tulichelewa kupata,so tukapewa lumpsum ya mwaka mzima ilikuwa Kama 2.4M),chap nikaigeuza kuwa mtaji wa Biashara ya ndoto zangu,hii biashara ya vocha ni kama Biashara ya mafuta,faida yake ni ndogo sana lkn ukiuza mzigo mkubwa faida unaiona,kipindi hicho hii mishe ilikuwa 🔥 🔥 ila now days ni ya kawaida sana,kuuza mzigo wa milioni 5 kwa siku ilikuwa ni jambo la kawaida,nilichanganya shule na biashara kwasababu sikuwa na gutts tena za kusubiri mpk nimalize.
Chuo kilipoisha,
Kwa kweli sikuwa hata na chembe ya kutafuta ajira ijapokuwa matokeo yalikuwa mazuri,washkaji niliomaliza nao walikimbilia ajira,mimi nikaingia rasmi kwenye biashara ya vocha za jumla, wakati namaliza chuo mtaji ulikuwa kama 3M hv lkn ndani ya miezi sita mtaji ukafika 10M miezi sita mingine ikafika 20M,kwa waliofanya mishe hii backdays wanajua kama ukiuza mzigo wa milioni basi faida ni elfu 20,nilikuwa nauza mpk 8M kwa siku,kukunja laki hadi laki na nusu perday ilikuwa kawaida,dat time nikanunua kiwanja,nikajenga maflemu kama nane,then kwa nyuma niliplan kujenga apartments za kupangisha,nilinunua hiace(daladala)ili nitanue wigo,it was amazingl!coz I was just 23,nikazidi kusema "business is a quickest way onto riches" ila sikujua kuwa business is also a riskiest way onto riches,kwa ufupi ile side A ya biashara niliimaster ipasavyo,nilipiga kazi sana mpk watu wakahisi natumia ndumba,kwasababu ofisini watu walikuwa wanajaa,foleni kama nmb,hakika biashara na maisha kwa ujumla viliniendea poa,mtaani kila mtu alitamani afanye biashara kwakile alichokiona kinatokea kwangu,nilitengeneza jina kwa muda mfupi sana ghafla yakaanza mapicha picha,mara nikute damu kwny kiti ninachokalia pale ofisini,Mara hirizi,pesa zikawa zinapotea kimazingara,hua siamini uchawi lkn hiki kilichokuwa kinatokea ni uchawi bila chenga,nilifukuza wafanyakazi lkn haikusaidia(nilihisi wananipiga)nilipiga moyo konde lkn changamoto zilizidi to the extent nikaanza kuogopa biashara,kwa kweli nilibaki njia panda,ila Kuna wazo likanijia,juu ya nini cha kufanya......................
*****************************
Biashara zina ups and downs,niliona upande mmoja,sasa dunia inanionyesha upande wa pili,nini kitaendelea baada ya kupata wazo.............usikose

JamiiForums



Sasa tuendelee
Mawazo ya kuhisi nalogwa yalitawala kichwani mwangu na ni kawaida ya mbongo kuwaza hivyo,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi,nimwelezee hii changamoto ya pesa kupotea kimazingara,nasema kimazingara kwasababu nilifukuza wafanyakazi nikabaki mwenyewe lkn kila nikipiga hesabu mtaji unakata tu,hata ungekuwa wewe ungehisi kuna namna Kuna mchezo unachezewa,ikabidi nimtafute mzee fabi,yeye ni mzoefu kwny biashara na mambo kama hayo itakuwa amepitia.
Mm:habari mzee wangu za siku.
Mzee fabi:salama,nani mwenzangu
Mm:ni Mimi,rafiki yake na fabi(nikajieleza mzee akanikumbuka,nikamweleza changamoto ninayopitia)
Mzee fabi:kijana mambo hayo Ni kawaida sana kwenye biashara,kwani fedha zako hapo dukani hua unaziweka kwenye nini?
Mm:naziweka kwenye draw
Mzee fabi:usiweke fedha kwenye draw ya mbao,nenda mjini kanunue safe.
Mm:mzee ninapitia changamoto za fedha kupotea kimazingara,hiyo safe itanisaidia kweli?(niliuliza kwa mshangao)
Mzee fabi(huku akicheka):kijana nimefanya biashara zaidi ya miaka 30,ninajua mengi,fanya nilichokuambia..
Kwa kweli sikutaka kuuliza sana nikaonekana ni much know,nikashindwa kusaidika.

Nilienda town,nikanunua safe ya kilo 50 nikaanza kuweka fedha zangu humo na u can't believe,sikupoteza tena fedha baada ya kufanyahivyo.

Nilijaribu kutafuta uhusiano wa kupoteza fedha na kuziweka kwny safe then hazipotei,sikupata jibu,kumuuliza mzee nilishindwa,niliogopa kumkera kwa maswali,hii kitu mpk leo bado inanifikirisha,nilijaribu ku Google walau nitaambulia chochote,sikupata kitu,nikajua Kuna elimu nyingine zimefichwa ni wachache wanajua,wadau tupo hapa kujifunza sijui kila kitu so kama kuna mdau hapa jf anajua atumegee kuhusu hiyo elimu,inakuaje uchawi ushindwe kupenya kwny safe?hii ni sayansi ya namna gani?
In short hii changamoto iliisha kiihivyo,nikaendelae na business zangu Kama kawaida,lakini baadaye kidogo ikaibuka changamoto nyingine iliyonitikisa kibiashara..................
******************************
Nilichojifunza kwa mzee fabi ni kwamba kupata changamoto kwny biashara ni kawaida ila tatizo ni namna unavyozitatua,hebu tuone changamoto ya safari hii nitatoka vp..........let's keep diving

Ilipoishia..........
Ile changamoto ya kupoteza fedha iliisha kiivyo nikaendelea na business zangu Kama kawaida,lkn baadaye kidogo iliibuka changamoto nyingine Tena,iliyonitikisa kibiashara........

Sasa tuendelee

Baaba ya mzee fabi kunipa ujanja wa kuweka hela kwenye safe,nilijiona mshindi,Kuna siku ambayo sitakuja kuisahau,siku hiyo nafika dukani simkuti mlinzi,mimi hua nawahi sana kufika ili nionane kwanza na mlinzi ndio mambo mengine yaendelee,sasa siku hiyo sijamkuta,piga simu hapatikani,nikaenda dukani nakuta geti imerudishiwa tu,kuingia ndani naona paa imevunjwa,nikajua jamaa wameingia,isee mapigo ya moyo yalienda mbio,akili ikanijia nicheki ile safe, nayo haipo😭jamaa wameibeba kabisa,dah!hapo ndio nikajua sijui,kwenye ile safe kulikuwa na zaidi ya 10M,hiyo ilikuwa my saddest day tangu nianze biashara,nilitetemeka all the day,nilitafuta yule mlinzi bila mafanikio,hiyo kazi nikawaachia polisi,mpaka leo hajaonekana,sitamsahau yule mzee alinifanyia umafia wa kiwango cha kasusura!wadau sijui nisemeje ila kuna wakati unaweza kujiona the luckiest guy in the world and within a minute ukajiona the most cursed person in the world,ile daladala nayo ilipata ajali(nilikuja kuiuza kwa hasara kama screpa)it was sad time,nilitafuta ushauri kwa watu sikupata msaada wa maana na wengi walinishauri niende kwa wataalamu nikasafishe nyota,niondoe mikosi,nikawapuuza,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi lkn nilijishtukia ikabidi nimtafute kwanza fabi(fabi baada ya kumaliza six,mzee wake alimpeleka kwenda kusoma nje,lkn kipindi hicho alikuwa ameshamaliza yupo chuga kusimamia buss za mzee wake)
Mm:habari fab,za kitambo hiyo,mishe vp?
Fabi:isee mambo safi chalii yangu,niko chuga,nasimamia biashara za mzee,vp ww,upo kwny ajira au umejiajiri?
Mm:nimejiajiri,ajira zinachelewesha kaka(tukacheka then mazungumzo yakaendelea)
Nilimweleza fabi changamoto ninazopitia,so akaniambia usijali,we njoo chuga tutayajenga.

Chuga town
niliingia chuga,mida ya saa mbili usiku,fabi akaniambia nimemweleza mzee wangu changamoto unazopitia,amehaidi atakusaidia,nilifurahi sana,siku hiyo mzee fabi hakuwepo(kila siku ya ijumaa halali nyumbani,analala ofisini) akaingia asubuhi

Mzee fabi:vp kijana mbona umepungua sana?
Mm:kawaida tu mzee wangu si unajua vijana ni kupambana
Nikaendelaea kusema😛ole na kazi maana niliambiwa umelala ofisini.
Mzee fabi:yah,wakati mwingine kazi zinakuwa nyingi huna budi kulala ofisini,anyway kuhusu suala lako,tutakwenda baadaye kuzungumzia ofisini.

Huyu mzee kwny duka lake moja la hardware ni jengo la ghorofa moja kwa juu ndio ameweka ofisi yake.
Nikafika ofisini kwake,yeye akaelekea dukani,mm akanipa funguo nitangulie ofisini,nikaingia ndani,nikaona kuna shelfu kubwa imejaa vitabu,kwa ukutani Kuna picha kubwa ya triangle ndani ya kiooa,nikiwa nashangaa shangaa,mzee akaingia akaniambia hivyo vitabu vyote nimevisoma,najua vitu vingi kuliko ww ijapokuwa sikusoma kama ninyi akimaanisha(mm n fabi)akaendelea kusema"elimu ya maisha haifundishwi shuleni,ipo katika kusoma vitabu"narudia tena kusema,huyu mzee alikuwa na nondo sio za nchi hii,ameniachia hazina kubwa sana kwny akili yangu,mzee aliongea mengi lkn alinisisitiza niielewe biashara kiroho la sivyo nitakuwa napiga double march time,sikuwa nimemwelewa hasa alimaanisha nn kuhusu kusoma vitabu na hasa alimaanisha vitabu gani,maana Mimi pia ni msomaji mzuri wa vitabu,nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza sema sikutaka kumchimba sana,mzee akainuka kwenye kiti akaenda kwenye shelfu akachomoa kitabu kimoja,akasema nenda kasome hicho,akanipa nauli na 2M ya kuboost mtaji,kwaana niliyumba vibaya,nikamshukuru sana mzee,then nikarudi zangu,kuendelea na haso.
******************************
Hiko kitabu kimebeba Siri gani....tunaelekea patamu,hii si ya kukosa...............
Rich dady poor dady
 
Mkuu, huwezi kua na experience ya kila kitu, hivo haipaswi kumbishia mtu mwenye experience ya jambo fulani ambalo wewe huna experience nalo.
Tutahakikisha vipi na kuthibitisha vipi hiyo experience ni ukweli na si uongo?

Nikikwambia nina experience ya kwenda kwenye sayari ya Mars kwa kupaa na ungo utakubali tu bila uthibitisho?
 
Tutahakikisha vipi na kuthibitisha vipi hiyo experience ni ukweli na si uongo?

Nikikwambia nina experience ya kwenda kwenye sayari ya Mars kwa kupaa na ungo utakubali tu bila uthibitisho?
Mkuu, kuna vitu huwezi vithibitisha kwa maandishi mpaka uingie field, vinginevyo utawaona wapuuzi tu wanaovisema.
 
Infropreneur Tanzanian Dream

Achana na infropreneur na uhakika na asilimia mia tano hana hata milioni mia bank, tena hiyo nyingi hata 20 tu hana.
Mwanzoni i was brainwashed na forbes, hawa motivation speaker kwamba usiogope anza kidogo kidogo fikirk positive.
I have seen the reality, nilipoteza 5 trucks za transit. I had over 400 million ,ikapukutika. Strange wenzako wanakuangalia mpaka nilipokuja kuambiwa na mtu mwingine mambo yanavyoenda.

Kuna watu unawakuta kwenye biashara wamestick hapo hapo hawataki kukua ,mwanzo nilikuwa nawashangaa sana .
cc kwa Xi jinping, asibishe vitu asivovijua anachukulia kirahisi rahisi tu kuwa ukitaka kufanikiwa tafuta eneo lenye mzunguko wa biashara..Hivi mtu kamiliki 400M in the bank account huyo kwamba huyo ni mjinga hajui mambo ya biashara? anakuja na hoja za kishule shule kirahisi...
apitie hii ajifunze kwa watu
 
NJIA YA KUFANIKIWA IN LIGHT SIDE
Nimeulizwa hili swali. Ni ipi njia ya kufanikiwa kiroho in Light side?

Kwa Experince na mtazamo wangu njia ni hii

Kwa wanao muamini Mungu
Njia pekee ya kufanikiwa kibiashara ni light side.

Unachohitaji ni [ A ]
Mtaji. , ubunifu, watu sahiihi, kujituma kutokukukata tamaa, kipaji ...n.k

Sasa Mungu anakujaje kwenye biashara.

Kwenye huu ulimwenhu kuna siri nyingi ambazo huwezi kuziona kwa macho ya kawaida au siku yakikukuta ndo utajua, vinginevyo endelea kusikia kwenye story za watu , siku ya kikukuta ndo uanze kuamini

Ili ufanikiwe Kwenye biashara kiroho kwa kupitia kwa Mungu kwa kinachohitajika Ni

Ulinzi wa kiroho = kwani kuna watu hawatapenda wewe uendelee au uwazidi ndipo chuki, majungu na kuendeaana kwa waganga panapo anziaga ni hapo ilimradi ufeli

Ukishatekeleza hayo nilioandika kwenye [ A] hapo juu. Maswala ya mvuto wa kibiashara na mafanikio yanatoka kwa Mungu

Cha muhumu ni wewe kuwa na uhusiano na conection na Mungu.

Unaipataje Hio connection na uhusiano?
Kwa

1 Toba na utakaso wa dhambi kwa kutubu.
Ili ukubali kuwa umeacha yale yote ya kale uliokuwa unayafacha dhambi ..nk yaani vitu visivyompendeza Mungu na umeamua kuwa mcha Mungu

2 Kusoma Biblia maana ndio maandiko yatakayo kuimarisha kiroho ili uwe mcha Mungu

3 maombi na sara. Ndo njia pekee ya kuongea na Mungu. Hakikisha unasali walau mara 3-5 kwa siku
( interval utakayo amua wewe kama kira baada ya masaa 8 au 6) ni sawa

4 Kufunga na kusali; namaanisha kukaa bila kula chakula waweza kunywa maji. Unaweza kuamua kufunga kuanzia asubuhi na ukala saa 12 jioni na saa 6 usiku.

5 usiwe mtenda dhambi kupindukia

Ukishafanya vyote hvyo ndani ya mwezi 1 hadi 3 utakua tayari una ulinzi wa kiroho wa Mungu pamoja na connection na Uhusiano wake.

Dalili utaziona kwenye ndoto utakazo anza kuziota

Ukisha anza kufanikiwa anza kutoa msaada kwa watu wasiojiweza mayatima, wagonjwa nk ndo njia ya kuongeza baraka

Ukisha vipata hivyo 3 yaani Ulinzi wa kiroho wa Mungu, uhusiano mzuri na Mungu pamoja na connection nakuhakikishia hakuna wa kugusa kiiimanini , kichawi, kishirikina nk

NB. Ata ukachukue mafuta, mchangaa, kitambaa, udongo kwa nabii wako bila kufanya nilio andika hapo juu hutoboi kibiashara maana Mungu akikubariki ni Life time au milele. Yaan watoto na kizazi chako chote kitabarikiwa kupitia wewe ata kwenye kuendeleza miradi yako.

Wale wa dark side hua sio milele kila baada ya muda fulani huwa wanaambiwa watoe sadaka/ wa mwage damu au dawa imeishiwa nguvu inabidi kutumia dawa nyingine

Ukisha pata uwepo wa Mungu ndani yako , maombi yako yote ya direct ufanikiwe ki biashara zako.
Kumbuka huko mwanzo ulikua unaomba uwepo wa Mungu uje ndani yake na katika maisha yako.

Sija taja dini au kanisa kwani kwangu mimi dini au kanisa ni njia anayotumia binadamu kukaa karibu na Mungu au kukkutana na wacha Mungu wenzio yaani kwa lugha nyingine Religion and chuch is pathway to Godliness. Sio gurantee kwamba ukiwa dini fulani au kanisa fulani ndo unakua mcha Mungu. Kinachohitajika ni JITIHADA ZAKo BINAFSI kumtafta Munvu kwa kufanya niliyo yaandika hapo juu.

Mambo ya niende kwa Nabii sijui mchungaji aniombee hayasaidii na hayatakupeleka popote . Ni JuHudi binafsi ya kumtafta Mungu kwa kufanya nilioyoyaandika hapo mwenyewe sio na wanakanisa au na nabii wako


Hivyo vitu vi 3 utavipoteza kwa kuwa mtenda dhambi au kufanya dhambi kupindukia. hasa ya KUZINI

Kwa nini kuzini?
Kwa sababu kuna wanaume/wanawake wanabeba roho/ spirit chafu, maagano ya ukoo, laana ..nk sasa utakapo sex nae ndo nawewe unabeba hizo roho kwani kwenye sex ndo portal ya wewe kutoa au kutokwa na baraka/ ulinzi wa kiroho n.k.

wale wa dark side ndo maana mtalaam akikupa dawa moja ya sharti ya dawa fulani uwa usifanye Sex kwani unaweza kupoteza nguvu ya dawa kwenye tendo hilo.
Watalaam mambo ya kidunia huwa wanasema mwanamke akiwa kwenye siku zake hua ni hatari sana kwani anaweza kupokea au kukupa spirit/ roho/ laana / magano kupitia sex ( hii story ya siku nyingine)

Ukiwa ushapata vitu hivyo wi 3 ya ulinzi wa kiroho wa Mungu, connction pamoja na uhusiano na ukafanya zinaa na mtu hasiye mke wako wa ndoa BAAS hivyo ndo Mungu atakapo uondoa uwepo wake nda yako.. Utajihisi MWEUPE yaan huna kinga /ulinzi wowote ule wa kiroho. Na kati ya vitu vigumu duniani ni kuuludisha huusiano wako na Mungu baada ya wewe kuuvunja. (Mffano ni petro alivyo mkana Yesu ma 3 kafatilie ako ka kipande ka hio stori ana kwambia alijihisi mweupe, manung'uniko ya kutosha au kwa samson na delilah baada ya uwepo wa Mungu kumtoka samson haikua Easy hivihivi kuurudisha)

Ulinzi wa kiroho kwa binadamu unatoka kwa Mungu, mizimu, uchawi, ushirikina, majini n.k
Ndo maana ukienda kwa waganga cha kwanza ni kuk scan au kwa lugha nyingine kukuchunguza kwenye chungu iliwaone kama una kinga/ulinzi wwte wa kiroho wa kukulinda . Kama huna ndo utaskia anasema wewe ni MWEUPE. Yaan huna kinga au ulinzi au kama unao basi hauna nguvu unaweza kudhulika muda wowote

Mfano
Ndo maana una skiaga story za fulani kanyeshwa sumu ili afe ila bado yupo hospitalini anapigania maisha yake .

HAPO unajifunza kwenye hii dunia sio kila kitu anapanga Mungu kitendeke vingine anapanga mwanadamu.
Turud kwenye mfano wetu wa sumu.


Sasa hapo kama alienyeshwa Sumu ni Mcha Mungu na Mungu hajapenda yeye afe atamuokoa arudi kwenye hali yake. AU
Kama huyo mtu alikua gwiji kwenye kuabudu mizimu na anatekeleza yte aavizwayo itampambania yeye aurudi kweye hali yake hivyohivyo kwa wachawi, majini n.k


Sasa wewe kama huna kinga / ulinzi utakua una ona una mabalaa na mikosi maana huna kinga/ ulinzi wa kujlinda mambo mengine ya kuache/ kupitie kushoto. Ndo mtu anakua na malalamiko ya kwanini mm hiki kinanikuta wengine hamn ( Mungu hajapanga vingine wamepanga binadamu kukukwamisha)

Ndo maana kwenye story ya " dark side of bussiness mzee ngurumo anasema dereva aliebeba ng'ombe kama hana ulinzi atakufa kwenye ajari. ( pia unajifunz mzee ngurumo na binadamu wengine wana ka technique ka kutambua fulani hana kinga au hana, usitukane au kumfanyia mtu mabaya huwezi kujua ulinzi wa kiroho alio nao una nguvu kiasi gani) ndo maana unaona wanasema ngoma nzito au kuingia choo cha kike watu wengine ni balaa unaweza kumtendea mabaya uu kumtumia kitu ila hakim kuti vinakurudia wewe alafu yakikurudia hua ni hatari sana kama sio kigo basi ni stroke au ulemavu


Na pale "kwenye ajari ya gari lilo beba ng'ombe" ndo maana kuna ajari nyingine zinatokea ila ukiangalia eneo au sehemu ajari ilipo tokea huoni damu ata barabarn. Damu huwa zinachukuliwa kimazingara na wachawi. Kuna mtu atabisha eti labda wamepata internal bleeding yaani damu imevujia kwa ndani/ ndani ya mwili.

( Tanzanian dream vipi hio ajari kwenye baranara kuna damu yyte ilichuruzika?)


Uki kaa na madereva wa mabasi na malori watakuelezea vizuri hio topic ya ulinzi / kinga kiroho kwani wanayo kutana nayo/ kuyaona barabarani ndo maana utaskia wana kimbilia kinga/ ulinzi wa kiroho



Wale wakina Tomaso wazee wa kubisha na kutoamini mpaka waone. Siwalazimishi muamini.
Na wapa assignemt.

Kila kipindi cha uchaguzi MCC utoa fedha nono kwa waganga wa Tz nzima ili wasitoe dawa yoyote kwa mwanachama yoyote wa upinzani itakayo msaidia ashinde chaguzi. Ka waulize waganga wa mkoa unaokaa walikutania wapi na MCC na wakapewa dau gani

Au
Ushasikia duka la muhindi au mwarabu limeibiwa kiujambazi? Basi kafatilie/ kawaulize waliowahi kuwaibia uwa kinawakuta nini? Sehemu zao za bishara huwa wana ulinzi wa kiroho wa kutosha usione kwa nje kaweka vitu vyke tu easy unakuta electronics kama Tv au pesa kaziachia wazi tu chukua kijambazi huone kitakachokukuta.

Au

kama umefatilia stroru ya mwana JF humu inasema kua walienda kwa mtalaam akawapa dawa na hirizi kabla hawajaenda kwenye tukio kufanya tukio lao la ujambazi. Kama ni ishu ya silaha na ngumi kwanini wasitumie kwenye kuiba mpka wakatafte kinga/ ulinzi utakao walinda pale watakapo pata shambulio la kiroho kwenye jambo lao.ni iweke hivi kua Kuna mali nyingine zimelinda kiroho. ( nyumba, benki, ikulu ila hii ni stori ya siku nyingine)

Usipo kaa na wakubwa wa nchii hii na dunia siri nyingine za ulimwengu unaweza ukafa hujazijua au kuzisikia masikion mwako

Hii njia ina Apply kwa mafanikio yoyote unayoyataka duniani iwe kibiashara, kimasomo, kilimo, siasa ...nk

Kwa kumalizia
Kwa experience yangu haya maisha tunayoishi ni ya kiroho. Unaweza ukakataa ila siku yakikukuta ndo utayajua kwa sahivi wewe kula shule ya dunia changanya na story za watu. Siku yakikukuta utaona vina make sense.

#SIKULAZIMISHI UAMINI MANENO YANGU. UNACHOTAKIWA KUFANYA NI WEWE KULA SHULE YA DUNIA/ ULIMWENGU NA CHAGUA NJIA YAKO KUISHI.
Kwa sasa tuachie hapo


100%
 
Hakika ambao awajui ndo wanabisha kuna kampuni ya wazungu kuna jamaa walitumwa mayai ya bundi walipoyapata walipewa ml 40 sasa wapi yanaenda haijulikani hiyo watu wakae kwa kutulia wajifunze elimu isiyofundishwa darasan
Wenyewe wanadhani ni rahisi rahisi..mtu analeta hoja za kishule shule sijui good customer care, sijui management, sijui location.. Hivyo vitu ni vipo tu unapotaka kufungua biashara lazima uangalie hivyo vitu.

Wanaposhindwa kujua ni kuwa hapa tunaongelea sustainability ya hiyo biashara/kampuni .e.t.c kuna mambo mengi ya kiroho lazima yahusike.
 
Huu ujinga ungefaa kwenye majukwaa mengine.

Like seriously sasa hapa kuna mjadala wa biashara au ujinga tu.

Yaani jukwaa la biashara badała ya kuongelea business objectives, strategies, monitoring of strategies, budgets, marketing.

Tuzungumzie huu upuuzi kama mambo ya biashara.
Wewe utapigwa seriously 😀😀😀
 
Leo nimetulia nimesoma huu UZi vzr kabisa japo sio mtu wa kifatilia mambo ya biashara na uchawi uchawi....

Ila hapa kuna ushauri nataka niwape ndgu zangu...
Hivi mnaonaje huyu jamaa Infropreneur tuka mkamata alafu tukampeleka kanisani tukamfungia kile chumba cha watu wanaungama alafu tunamuacha yeye na pasta mmoja wazichape...

Baada ya hapo mnanikabidhi mimi nampeleka msikiti pale masjidi mtoro tukamwadabishe....

😀😀😀😀
 
Anaebisha kwanini asimtafte mleta mada ampatie namba ya mzee ngurumo au mtalaam yeyote . Aanze kazi na yeye upande wa dark side ata kama ya kutafta mafanikio kwa njia hio, ndo uwe utafiti wake kuwa hii ni ishu uwa ya uongo au kweli.

Kisha alete mrejesho wake. Sio watu wakuletee tu uthibitisho, ni ishu ya wewe kuutafta uthibitisho

Au mpaka upewe namba za shetani ukutane nae stendi
 
Leo nimetulia nimesoma huu UZi vzr kabisa japo sio mtu wa kifatilia mambo ya biashara na uchawi uchawi....

Ila hapa kuna ushauri nataka niwape ndgu zangu...
Hivi mnaonaje huyu jamaa Infropreneur tuka mkamata alafu tukampeleka kanisani tukamfungia kile chumba cha watu wanaungama alafu tunamuacha yeye na pasta mmoja wazichape...

Baada ya hapo mnanikabidhi mimi nampeleka msikiti pale masjidi mtoro tukamwadabishe....

😀😀😀😀
The issue is very simple.

Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini waafrika watanzania wasiutumie kwa nguvu zao zote wawazidi matajiri wakubwa duniani kama kina Elon musk, Jeff Bezos, Billgates, Warren Buffett n.k

Au huyo shetani na yeye pesa zake ni za kuunga unga?

Toeni makafara ya kutosha tuone kama mtaweza hata kumfikia Mo Dewji kwa utajiri.

Kwa nini muandikie mate na wino upo?

Kama kweli kwa hakika, Kuna utajiri wa kishetani kwa nini mtu hautumii kwa nguvu zake zote awazidi matajiri wakubwa duniani kina Elon musk?

Au basi angalau afikie level zao kwa huo utajiri wa kishetani.
 
Anaebisha kwanini asimtafte mleta mada ampatie namba ya mzee ngurumo au mtalaam yeyote . Aanze kazi na yeye upande wa dark side ata kama ya kutafta mafanikio kwa njia hio, ndo uwe utafiti wake kuwa hii ni ishu uwa ya uongo au kweli.

Kisha alete mrejesho wake. Sio watu wakuletee tu uthibitisho, ni ishu ya wewe kuutafta uthibitisho

Au mpaka upewe namba za shetani ukutane nae stendi
Huyo mzee ngurumo kwani yeye hataki kuwa tajiri?

Huyo mzee ngurumo kama ana nguvu za kitajiri kweli, Kwa nini azitumii kwa juhudi zake zote awazidi matajiri wakubwa kama kina Mo Dewji Bakhressa?

Tumieni huo utajiri wa kishetani kuanzisha makampuni makubwa, real estates na Viwanda vikubwa vya uzalishaji ndipo nitajua huo utajiri wa kishetani upo kweli na unafanya kazi kweli.
 
The issue is very simple.

Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini waafrika watanzania wasiutumie kwa nguvu zao zote wawazidi matajiri wakubwa duniani kama kina Elon musk, Jeff Bezos, Billgates, Warren Buffett n.k

Au huyo shetani na yeye pesa zake ni za kuunga unga?

Toeni makafara ya kutosha tuone kama mtaweza hata kumfikia Mo Dewji kwa utajiri.

Kwa nini muandikie mate na wino upo?

Kama kweli kwa hakika, Kuna utajiri wa kishetani kwa nini mtu hautumii kwa nguvu zake zote awazidi matajiri wakubwa duniani kina Elon musk?

Au basi angalau afikie level zao kwa huo utajiri wa kishetani.
Sasa unaambiwa wao uchawi wao mkubwa mkuu..
Kwani kwanini wewe mbishi hvo..
Kwani wewe ulivokua mdogo ulikua dini gani ...?
 
Kwa nilivyo nikisha sikia mtukasema yeye ni Atheist. Uwa na mheshimu mtazamo wake na sisiwezi kubishana nae
Screenshot_20241211-152057_Opera Mini.jpg


Kwani hio nayo hua ni dini au tabaka na lina waanzilishi wake na kuna vitabu vyao wanavyosoma
 
Sasa unaambiwa wao uchawi wao mkubwa mkuu..
Kwani kwanini wewe mbishi hvo..
Kwani wewe ulivokua mdogo ulikua dini gani ...?
Kwanza hizi habari za utajiri wa kishetani zipo kwenye mentality za waafrika maskini choka mbaya.

Kama kuna utajiri wa kishetani kwa nini huutumii kufanikiwa kama kweli upo?

Kwa nini unafanya kazi? Kwa nini unatafuta hela kwa jasho?

Kwa nini usikae na hayo matunguli yalete pesa automatically kila siku bila kujihangaisha kufanya kazi?

Mimi mtu akiweza kuanzisha kiwanda kikubwa cha uzalishaji kwa uchawi tu, bila kutumia mkopo wowote wa kibenki au taasisi yeyote ya kifedha, Au akiba yake yeyote ya fedha.

Yani Atumie uchawi tu kujenga kiwanda. Hapo ndio nitajua kwamba kweli kuna utajiri wa kishetani.

Unless otherwise, Hizi ni stori za kusadikika tu, hakuna utajiri wa kishetani.
 
Kwa nilivyo nikisha sikia mtukasema yeye ni Atheist. Uwa na mheshimu mtazamo wake na sisiwezi kubishana nae
View attachment 3174476

Kwani hio nayo hua ni dini au tabaka na lina waanzilishi wake na kuna vitabu vyao wanavyosoma
Hata wewe ulizaliwa Atheist bila kuwa na imani yeyote ile ya Mungu au miungu.

Mpaka pale ulipo aminishwa na wazazi wako kwenye kuamini Mungu na miungu.

Hivyo kila binadamu alizaliwa Atheist Bila kuwa na imani yeyote ile. Hadi pale alipo aminishwa na kukaribishwa kwenye imani za Mungu au miungu.
 
The issue is very simple.

Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini waafrika watanzania wasiutumie kwa nguvu zao zote wawazidi matajiri wakubwa duniani kama kina Elon musk, Jeff Bezos, Billgates, Warren Buffett n.k

Au huyo shetani na yeye pesa zake ni za kuunga unga?

Toeni makafara ya kutosha tuone kama mtaweza hata kumfikia Mo Dewji kwa utajiri.

Kwa nini muandikie mate na wino upo?

Kama kweli kwa hakika, Kuna utajiri wa kishetani kwa nini mtu hautumii kwa nguvu zake zote awazidi matajiri wakubwa duniani kina Elon musk?

Au basi angalau afikie level zao kwa huo utajiri wa kishetani.
Utakuwa haujamuelewa mtoa mada...Mtoa mada hajaomgelea utajiri wa shetani...anaongelea Kinga za kiroho na mbini unapofanya business...Hao matajiri wakubwa we Ushawahi Fanya nao kazi?una uhakika hawafanyi chochote...Kawaulize customer care wa call centre wanaofanya .ye mak
ampuni makubwa ya simu wahindi Huwa wanafny
a inada Gani.?
Wahindi hauwwzi kuwatenga na Ibada zao....Waafrika we kama haujawahi kwenda Kwa mganga Wala kanisani ....Jua wazazi wako wanatambika.....au walikutambikia
 
Utakuwa haujamuelewa mtoa mada...Mtoa mada hajaomgelea utajiri wa shetani...anaongelea Kinga za kiroho na mbini unapofanya business...Hao matajiri wakubwa we Ushawahi Fanya nao kazi?una uhakika hawafanyi chochote...Kawaulize customer care wa call centre wanaofanya .ye mak
ampuni makubwa ya simu wahindi Huwa wanafny
a inada Gani.?
Wahindi hauwwzi kuwatenga na Ibada zao....Waafrika we kama haujawahi kwenda Kwa mganga Wala kanisani ....Jua wazazi wako wanatambika.....au walikutambikia
Hakuna kinga za kiroho, mbona watu wanafilisika kila mara na hizo kinga unazodai zipo haziwasaidii chochote?

Au hizo kinga zina kinga nini?

Maana hata matajiri wakubwa biashara zao kuna muda huyumba na kupitia ups and downs.

Sasa hizo kinga zina kinga kitu gani haswa?
 
Back
Top Bottom