oel200e
JF-Expert Member
- Nov 17, 2013
- 276
- 118
Habarini,
Katika pitapita zangu za kujua vitu nikakuta hii kitu kuhusiana na dunia kutokuwa ni duara na ni tambarale pia haizunguki katika muhimili wake kama tulivofundishwa huko shule za awali.
Kuna baadhi ya ushahid unaotokana na mazingira jinsi yalivo pamoja na udini kidogo...
1. kwa mazingira jinsi yalivyo:
Kwanza kuhusu "earth is not rotating" .... kawaida dunia inazunguka jua kwa muda siku 365 na hujizungusha katika muhimil wake kwa muda wa masaa 24 kumaliza mzunguko wake, na ndipo tunapata usiku na mchana.... (hivi ndivo navojua mm na wewe)
lakini kuna maelezo yanayo onyesha kuwa dunia haijizungushi bali jua na vilivo juu vinaizunguka dunia. proof wanaosema kwamba dunia haizunguki ni hii ya usafiri wa ndege.
Tuanze kwa kusema kwamba dunia inajizungusha katika muhimili wake kwa speed ya 6070 km/hr kutokea magharibi kwenda mashariki, ndio maana tunapata kuona jua linachomoza kutokea mashariki na kuzama magharibi.
Sasa tuchuke mfano ndege inatokea marekani (Washington DC) kwenda uingereza (London). Hivyo ndege inatoka magharibi kwenda mashariki. Umbali kutoka marekani mpaka uingereza ni 5934.6 km na inachukua masaa 7 na dakika 39, hivyo ndege husafiri katika umbali huo kwa 775.76 km/hr. Hivyo kama dunia inakuwa katika speed yake ya 1675 km/hr basi huu umbali ungeongezeka zaid maana dunia ingekuwa inazidi kwenda mbele kutoka magharibi kwenda mashariki na ndege hiyo kwa speed hiyo ya 775.76 km/hr. [lets assume kwamba umbali huo unatokana na speed ya dunia na speed ya ndege kutoka magharib kwenda mashariki]
JE, KAMA NDEGE INATOKA UINGEREZA KWENDA MAREKANI UMBALI UTAKAO KUWA COVERED NA NDEGE UTAKUWA SAWA NA WA MWANZO (5934.6 KM) KAMA DUNIA INAJIZUNGUSHA KUTOKA MAGHARIBI KWENDA MASHARIKI?
JIBU NI HAPANA, MAANA KAMA NDEGE INATOKA MASHARIKI KWENDA MAGHARIBI NA DUNIA INAZUNGUKA KUTOKA MAGHARIBI KWENDA MASHARIKI BASI UMBALI UTAPUNGUA MAANA DUNIA NA JUA ZITAKUWA OPPOSITE DIRECTION.
View attachment 216726
Lakini kiuhalisia umbali utakuwa ni huohuo na masaa ya kusafiri yatakuwa ni hayohayo... HIVYO HII INAONESHA KUWA DUNIA HAIZUNGUKI.
Pili kuhusu "the earth is flat and not round".... bado kuna debate zinaendelea kuelezea kivipi dunia ni flat na sio duara kama tunavojua. Ila katika hili kuna maswali mengi sana, maana kuna issues za horizon, light, space and sky ceiling, land curvature ambazo mm mwenyewe binafsi naendelea kuzifatilia ila kwa sasa sina clue ambazo zitani support kuelezea kivip dunia ni tambarale.
Ila inasemekana dunia ina umbo la flat disk kama hii.
View attachment 216727
Hii ni bendera ya United Nations na ramani yake ya dunia iko tofauti na ramani ambazo tunazozijua. Hivyo inasemekana kuna siri katika shape ya dunia. flat earth society wanaamini kuwa dunia iko hivyo ila kwa pande nne sio round kama inavoonekana kwenye hiyo picha juu.
Pia kuhusu maji ya bahari kuna kuta za barafu zinashilia hayo maji. Hii inawezekana baada ya ile mada ya kuto kuwepo kwa south pole kule Antarctica.
Kunasemekana Antarctica ni kubwa kuliko tunavoiona katika ramani, pia ndiko kunakoaminika kuwa ni kitovu kitakocho onyesha kuwa dunia sio duara bali ni tambarale.
Maana hakuna ndege inayoruhusiwa kipita katika anga la Antarctica. Jiulize, Kina "NASA" wanadai wameenda mwezini, wametuma vifaa vya kisasa huko sayari mars na vyengine mbali zaid lakini wameshindwa kupita juu ya Antarctica kisa ni baridi kali... JIULIZE!!!!!!
2. Udini:
Katka udini nitazungumzia katika upande wa imani ya kikristo.
1. katika agano la kale yoshua alisimamisha jua. Yoshua 10: 12-13 "12 Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni;
Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.13 Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao."
hii inaonyesha kuwa Jua ndilo linalozunguka dunia na sio dunia linazunguka Jua, Hivyo dunia haizunguki na iko stationary
2. katika agano jipya shetani alimchukua Yesu mpaka mahali pa juu na kumuonyesha ulimwengu wote:
Luka 4 : 5 -8
5 Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
6 Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza. 7 Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."
8 Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."
kama dunia ingekuwa duara basi ingekuwa haiwezekani kwa falme zote za ulimwengu kuonekana kwa mara moja.
3. malaika wanne katika kona za nchi:
Ufunuo 7 : 1
"1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote."
hii inaonesha kuwa dunia pia sio duara, maana kama ni round hizo pembe nne za nchi zitapatikanaje?. Hivyo dunia might be square or rectangle.
TUJADILI ZAID NI HAYA NILIYOYAKUTA KATIKA KUJUA ZAID...... THANKS
Seriously?!(politely 😊😉 Hivi huioni hata hiyo picha ya satellite kama inaonesha dunia ni a sphere?....kama ni disc kwa nini huoni continents zote?.....alafu I think utakua umesahau principles za "physics" kama uliisoma advance....kama wewe upo ndani ya gari linalotembea (au tuseme juu yake) ukikimbia utabaki pale pale? Au urefu wa gari unaongezeka?
Au unajua kwa nini ukishuka kwenye gari linalotembea huwa unaanguka,or else na wewe ukimbie?..it's because tupo kwenye uniform motion...dunia haijawahi kusimama,ipo kwenye motion siku zote,na sisi na vitu vyote,ni kama abiria,japo tumekaa ila we are in motion..so the distance remains the same.UNLESS unasafiri nje ya dunia,ndio maana I think it takes a lot of power to travel to the moon,na huchukua masaa mengi zaidi.
Alafu,Ina maana na mwezi pia unazunguka au umesimama according to your theory?...kuhusu BIBLE...I will get back