The earth is flat and is not rotating

The earth is flat and is not rotating

Hoja nzuri sana, imejengwa vema ktk namna ya kuchallenge nadharia zilizopo!!

Critique: Kama dunia ni flat na co duara, JE NANI AMEWAHI FIKA KWENYE NCHA ZA HII FLAT??
AU PEMBEZON MWA HYO DUNIA FLAT???
Make Dunia kama ni flat tutegemee kuona KINGO zake kama ilivyo kwa upanga, au kiwanja cha mpira au la vingnevyo!!
Sura halisi ya dunia hii flat umbile lake lipoje????

Me nilivyomuelewa mtoa mada ni kuwa dunia iko flati lakini ni duara kama vile kisosi na siyo kama meza. Ndio maana ameweka na mfano wa ramani ya UNO.
 
Same speed!!! Vitu vyote vilivyoko duniani na kwenye atmosphere yake vina move at the same speed same momentum. Vituo vya anga vya utafiti ni moving station viko fixed kwenye orbit na vinazunguka kwa speed sawa na ya dunia. Na ndio maana unaviona kama viko stationary

Hivi hizi commercial Jet zinazokumbwa na masaibu angani zinakuwa nje ya atmosphere au zenyewe sio sehemu ya inzi kwenye ndege ?
Mfano ni AirAsia
 
Same speed!!! Vitu vyote vilivyoko duniani na kwenye atmosphere yake vina move at the same speed same momentum. Vituo vya anga vya utafiti ni moving station viko fixed kwenye orbit na vinazunguka kwa speed sawa na ya dunia. Na ndio maana unaviona kama viko stationary

Hivi hizo setelite ziko spinned katika orbit au zinatumia locomotive engenes kama jet engine katika kuvispeed up viendane sawa na speed ya dunia katika kulizunguka jua n at the same time katika kujizungusha yenyewe katika mhimili wake? Nataka kujua tafadhali
 
Nia yako ni nzuri,ila kuna tatizo humu jamvini,kama unafwatilia mada hii utakuja kuliona tatizo husika.

Mkuu Imany John hapa jamvini kuna maada nzuri sana kama hizi ila wachakachuaji ni wengi hasa wale wa ku-PROVE THAT BLAAH-BLAAH IS/ISN'T BLAAH-BLAAH ndio wanaotukosesha utam wa 3D

.made in mby city.
 
Problem ni kwamba watu wanafikiri dunia ni duara kabisa kama mpira, no! Yaani ni kwamba shape yake ni duara sawa lakini sio round ile ya mpira kama picha ya mpira jamani. Ingekuwa na duara hilo kama tungesawazisha milima yote (mfano kilimanjaro wenye futi kama 5000 hivi kwenda juu) na mabonde yote ambamo kuna maji na kusikokuwa na maji (mfano lake Tanganyika lenye zaidi ya kilometa moja na nusu kwenda chini). Yaani shape generally ni round lakini kwenye sphere hiyo kuna milima na mabonde ila kutokana na ukubwa wa kipenyo cha dunia, milima hiyo ni kama kipele tu usoni!!

Ila hata mimi theory ya mtoa mada imeni-confuse sana! Hasa hapo kwenye usafiri wa ndege. Kama dunia ni duara route ya ndege flani (mfano kutoka London kwenda Western Sydney) isingekuwa ileile wakati wote kwa sababu destination point (mfano sydney) ingekuwa inahamahama kutokana na kuzunguka kwa dunia na kutokana na ukweli kwamba ndege inakuwa ilikuwa juu wakati dunia inazunguka na hivyo haikuzunguka nayo.


Wewe utakuwa umesahau ulivyofundishwa na mwalimu wako..
Fikiria tena
 
Biblia naona jamaa alienda chaka kidogo, pembe nne za dunia haimaanishi dunia ni flat, kwani si kuna north,west,east na south!! Afu anavosema jua na mwezi vikasimama, hiyo ni lugha ya picha tu... Kama haamini dunia ni round akasome kwenye bibllia
Isaya 40:22 "Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia, nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi"
Mkuu soma Ayubu 26:10 " Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana"

Hivyo mkuu kama dunia ni duara kama shape basi isingekuwa na mipaka... ndo mana nikasema iko as disk... yani kana "cd" au kama ramani ya dunia katika bendera ya UN
 
Unaposema dunia ni flat una maanisha 2D (x,y) na kwa mtazamo wako kusingekuwa na milima ndani yake. Kimahesabu dunia inakuwa flat kama unachukua dunia kuwa kama tufe ikiwa na radius sawa kutoka katikati kwenda kwenye uso wa dunia (Tanget). Hii ni kwa ajili ya kurahisisha mahesabu. Lakini kiuhalisia Dunia haiko kama tufe dunia ina umbile la "Geoid" (sielewi kiswahili chake, labda u-google). Geoid inachukua umbile la duni kama unavyoona kwenye uso wa dunia kukiwa na mabonde, milima, nk. Kajifunze somo linaitwa Geodesy (Physical Geodesy and Geometrical Geodesy).
 
hahaha dunia ikiwa flat ukitaka kwenda marekani unaweza tokea australia na kuzunguka kulia ukafika, au ukatokea hapa bongo ndege ikaenda kushoto na ukafika.. sasa ingekua flat wa australia si wangefika mwisho wa dunia afu waanguke... hahaha au kama ni bahari basi si maji yangemwagika mwisho wa dunia yakaisha manake ingekua ka meza.. hahaha hadi najihisi naongea pumba


Kamanda naamini mleta mada na wengine washaelewa somo..
Big up
 
Tunapotengeneza ramani tunatengeneza ramani ikiwa katika 2D, yaani imebadilishwa kutoka 3D (Curved surface) kwenda 2D (Flat surface). Hii nafanyika kimahesabu zaidi kwa kutumia kile tunaita projection, na zipo projection za aina mbalimbali.
 
hahaha dunia ikiwa flat ukitaka kwenda marekani unaweza tokea australia na kuzunguka kulia ukafika, au ukatokea hapa bongo ndege ikaenda kushoto na ukafika.. sasa ingekua flat wa australia si wangefika mwisho wa dunia afu waanguke... hahaha au kama ni bahari basi si maji yangemwagika mwisho wa dunia yakaisha manake ingekua ka meza.. hahaha hadi najihisi naongea pumba

Mkuu jaribu kuangalia ramani ya dunia katika bendera ya UN... dunia sio flat as rectangle au mraba ni "duara flat" labda niseme hivyo
 
Ila hata mimi theory ya mtoa mada imeni-confuse sana! Hasa hapo kwenye usafiri wa ndege. Kama dunia ni duara route ya ndege flani (mfano kutoka London kwenda Western Sydney) isingekuwa ileile wakati wote kwa sababu destination point (mfano sydney) ingekuwa inahamahama kutokana na kuzunguka kwa dunia na kutokana na ukweli kwamba ndege inakuwa ilikuwa juu wakati dunia inazunguka na hivyo haikuzunguka nayo.

kutokana na fixed time and distance za destinations mbili inaonesha kuwa hakuna mzunguko wa dunia... kama mzunguko wa dunia ungekuwepo basi time na distance zingebadilika...
 
Hoja nzuri sana, imejengwa vema ktk namna ya kuchallenge nadharia zilizopo!!

Critique: Kama dunia ni flat na co duara, JE NANI AMEWAHI FIKA KWENYE NCHA ZA HII FLAT??
AU PEMBEZON MWA HYO DUNIA FLAT???
Make Dunia kama ni flat tutegemee kuona KINGO zake kama ilivyo kwa upanga, au kiwanja cha mpira au la vingnevyo!!
Sura halisi ya dunia hii flat umbile lake lipoje????

as UN Flag inavoonekana ndivo dunia ilivyo....ndilo umbile lake... katka kingo sijapata clues ambazo hata mm znazoni convince zaid... ila kuna hii ya Antarctica kuwa ni longest block of ice inayoaminika kuwa ndio mpka wa bahar....
nina weza nikaikubali hii kwa kutumia bible katika Ayub 26:10 " Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana"
 
Bado mtoa mada ana hoja za kufanyia kazi. ndege inaporuka inakua imeacha uso wa dunia hivyo ni kweli kama inaelekea mashariki basi umbali ungeongezeka na kama ingeelekea magharibi umbali ungepungua.
 
Acha uvivu wa kufikiri, kwa hiyo ulitegemea kuwa ndege inayotoka UK kwenda US inaweza tu kuganda hewani na baada ya muda wakatua USA? Ingekuwa hivyo hawa ndege warukao angani kama vile njiwa na kunguru ingekuwa shida sana kulenga (ku-aim) destinations zao, maana warukapo kutoka mti mmoja kwenda mwingine wasingeweza kuufikia maana speed ya dunia ni kubwa kuliko speed yao. Jibu ni kwamba vyote hivyo vyote ni sehemu ya dunia na tupo kwenye mzungo muda wote. Ili usiwe sehemu ya mzunguko huu unatakiwa utoke duniani na uende anga za mbali. Utafaidi kuona dunia ikizunguka kwa speed ya hatari.

Haya niliyajua nikiwa darasa la tano.
 
Kama ingekuwa flat si ingekuwa na mwisho au tutadai na yenyewe ni infinite....!? Nimewaza tu

Unapodai earth not round naweza nikakuunga mkono sababu shape ya earth ni irregular na siyo regular ila huwa inafanyiwa approximation kui-cover ionekane iko spherical ili iweze kufanyiwa mathematical computation hapa nahusisha survey of the earth kwa kuingiza concept ya Ellipsoid na Geoid ambapo kwenye survey huwa wana assume the earth distance is horizontal so slunt huwa haziwi considered so kwa kuwa shape of earth ina kuwa approximated hivyo ni rahisi kusema siyo round BUT THE EARTH IS NOT FLAT

Nimejaribu kukumbuka wakat nipo darasa la tatu/nne katika kipind cha sayansi tulifundishwa jinsi ya kupata mchana na usiku kwa kutumia round world map na torch sasa hii concept ukijaribu kui-apply kwenye flat earth tutapataje usiku na mchana?

Hapa najaribu kuhusisha na kuchelewa kwa mawio na macheo ya jua mfano hata hapa Tanzania mtu wa mtwara na kigoma wanatofautiana hata Marekani state zao zinatofauti ya masaa. Je ikiwa flat tutatofautiana kama hivi?

Jaribu kusafiri na meli/mtumbwi/mashua wakati wa alfajiri au jioni exactly utaona how the earth is spherical not flat kwa sababu ya mawio/ macheo ya jua na hii huwa ni Moja ya theory inayo-prove the earth is spherical
 
as UN Flag inavoonekana ndivo dunia ilivyo....ndilo umbile lake... katka kingo sijapata clues ambazo hata mm znazoni convince zaid... ila kuna hii ya Antarctica kuwa ni longest block of ice inayoaminika kuwa ndio mpka wa bahar....
nina weza nikaikubali hii kwa kutumia bible katika Ayub 26:10 " Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana"

LITTLE HULK, it's OK nazidi kufungua mind yangu bado!!
Kama ni hvyo, Dunia imejishikisha au imeunganika nanini kwenye ncha zake???
Je waliowahi kufika huko kwenye ncha hzo kama za UN flag kama ulivyodai walishuhudia nn au shimo refuuu ambalo MTU au vitu huweza dumbukia???
 
Last edited by a moderator:
Habarini,

Katika pitapita zangu za kujua vitu nikakuta hii kitu kuhusiana na dunia kutokuwa ni duara na ni tambarale pia haizunguki katika muhimili wake kama tulivofundishwa huko shule za awali.

Kuna baadhi ya ushahid unaotokana na mazingira jinsi yalivo pamoja na udini kidogo...

1. kwa mazingira jinsi yalivyo:

Kwanza kuhusu "earth is not rotating" .... kawaida dunia inazunguka jua kwa muda siku 365 na hujizungusha katika muhimil wake kwa muda wa masaa 24 kumaliza mzunguko wake, na ndipo tunapata usiku na mchana.... (hivi ndivo navojua mm na wewe)

lakini kuna maelezo yanayo onyesha kuwa dunia haijizungushi bali jua na vilivo juu vinaizunguka dunia. proof wanaosema kwamba dunia haizunguki ni hii ya usafiri wa ndege.

Tuanze kwa kusema kwamba dunia inajizungusha katika muhimili wake kwa speed ya 6070 km/hr kutokea magharibi kwenda mashariki, ndio maana tunapata kuona jua linachomoza kutokea mashariki na kuzama magharibi.

Sasa tuchuke mfano ndege inatokea marekani (Washington DC) kwenda uingereza (London). Hivyo ndege inatoka magharibi kwenda mashariki. Umbali kutoka marekani mpaka uingereza ni 5934.6 km na inachukua masaa 7 na dakika 39, hivyo ndege husafiri katika umbali huo kwa 775.76 km/hr. Hivyo kama dunia inakuwa katika speed yake ya 1675 km/hr basi huu umbali ungeongezeka zaid maana dunia ingekuwa inazidi kwenda mbele kutoka magharibi kwenda mashariki na ndege hiyo kwa speed hiyo ya 775.76 km/hr. [lets assume kwamba umbali huo unatokana na speed ya dunia na speed ya ndege kutoka magharib kwenda mashariki]

JE, KAMA NDEGE INATOKA UINGEREZA KWENDA MAREKANI UMBALI UTAKAO KUWA COVERED NA NDEGE UTAKUWA SAWA NA WA MWANZO (5934.6 KM) KAMA DUNIA INAJIZUNGUSHA KUTOKA MAGHARIBI KWENDA MASHARIKI?

JIBU NI HAPANA, MAANA KAMA NDEGE INATOKA MASHARIKI KWENDA MAGHARIBI NA DUNIA INAZUNGUKA KUTOKA MAGHARIBI KWENDA MASHARIKI BASI UMBALI UTAPUNGUA MAANA DUNIA NA JUA ZITAKUWA OPPOSITE DIRECTION.

View attachment 216726

Lakini kiuhalisia umbali utakuwa ni huohuo na masaa ya kusafiri yatakuwa ni hayohayo... HIVYO HII INAONESHA KUWA DUNIA HAIZUNGUKI.

Pili kuhusu "the earth is flat and not round".... bado kuna debate zinaendelea kuelezea kivipi dunia ni flat na sio duara kama tunavojua. Ila katika hili kuna maswali mengi sana, maana kuna issues za horizon, light, space and sky ceiling, land curvature ambazo mm mwenyewe binafsi naendelea kuzifatilia ila kwa sasa sina clue ambazo zitani support kuelezea kivip dunia ni tambarale.

Ila inasemekana dunia ina umbo la flat disk kama hii.

View attachment 216727

Hii ni bendera ya United Nations na ramani yake ya dunia iko tofauti na ramani ambazo tunazozijua. Hivyo inasemekana kuna siri katika shape ya dunia. flat earth society wanaamini kuwa dunia iko hivyo ila kwa pande nne sio round kama inavoonekana kwenye hiyo picha juu.

Pia kuhusu maji ya bahari kuna kuta za barafu zinashilia hayo maji. Hii inawezekana baada ya ile mada ya kuto kuwepo kwa south pole kule Antarctica.

Kunasemekana Antarctica ni kubwa kuliko tunavoiona katika ramani, pia ndiko kunakoaminika kuwa ni kitovu kitakocho onyesha kuwa dunia sio duara bali ni tambarale.

Maana hakuna ndege inayoruhusiwa kipita katika anga la Antarctica. Jiulize, Kina "NASA" wanadai wameenda mwezini, wametuma vifaa vya kisasa huko sayari mars na vyengine mbali zaid lakini wameshindwa kupita juu ya Antarctica kisa ni baridi kali... JIULIZE!!!!!!

2. Udini:

Katka udini nitazungumzia katika upande wa imani ya kikristo.

1. katika agano la kale yoshua alisimamisha jua. Yoshua 10: 12-13 "12 Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni;

Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
13 Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao."

hii inaonyesha kuwa Jua ndilo linalozunguka dunia na sio dunia linazunguka Jua, Hivyo dunia haizunguki na iko stationary

2. katika agano jipya shetani alimchukua Yesu mpaka mahali pa juu na kumuonyesha ulimwengu wote:
Luka 4 : 5 -8

5 Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,

6 Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza. 7 Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."

8
Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."

kama dunia ingekuwa duara basi ingekuwa haiwezekani kwa falme zote za ulimwengu kuonekana kwa mara moja.


3. malaika wanne katika kona za nchi:

Ufunuo 7 : 1

"1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote."

hii inaonesha kuwa dunia pia sio duara, maana kama ni round hizo pembe nne za nchi zitapatikanaje?. Hivyo dunia might be square or rectangle.


TUJADILI ZAID NI HAYA NILIYOYAKUTA KATIKA KUJUA ZAID...... THANKS

Sioni haja ya kujadili vitu ambavyo viko wazi kabisa. Kigezo cha kupima dunia does not ratate on its own axis kwa kutumia ndege sio sahihi kwa sababu ndege yenyewe imo kwenye mzunguko wa dunia. ni sawa na kusema ukiwa kwenye ndege economy class umekaa umbali wa mita nne kutoka chooni ambacho kiko nyuma halafu unasema eti kwenda chooni ni karibu sana kwa sababu unatembea opposite na elekeo wa ndege na kurudi kwenye kiti ni mbali sana eti kwa sababu ndege ina-speed kubwa kuliko kutembea. Wazo lako ni zuri la kuendelea kutafuta ukweli kwa wewe mwenyewe kwani wengine ukweli walishaujua siku nyingi!!!

Pila dunia ni flat, ili ni tatizo jingine la kukosa uelewa. Tayari naona una uelewa sijui kwa nini unashindwa kupata majibu. Kigezo cha bendera kusema dunia ni flat sio sahihi. Ulitaka bendera iwe na globe au mfano wa globe? Ikiwekwa kwenye bendera kama globe nchi nyingine zitaonekanaje? au globe liwe linazunguka au mtu azunguke, kitambaa chenyewe flat iweje picha isiwe flat? Hiyo ni another perspective of viewing the world kwa ajili ya purpose ya kuonyesha mataifa yote.

Dini ya Kikristo ilizinduliwa na Galileo kuwa dunia sio flat na wakaelewa, ila waislamu bado hawajazinduka, sijui dini za kijadi na wasiokuwa na dini wanamtazamoa gani. Ushauri: unaposhughulikia science usiingize dini au dini usiingize sayansi!
 
Back
Top Bottom