The earth is flat and is not rotating


Me nilivyomuelewa mtoa mada ni kuwa dunia iko flati lakini ni duara kama vile kisosi na siyo kama meza. Ndio maana ameweka na mfano wa ramani ya UNO.
 

Hivi hizi commercial Jet zinazokumbwa na masaibu angani zinakuwa nje ya atmosphere au zenyewe sio sehemu ya inzi kwenye ndege ?
Mfano ni AirAsia
 

Hivi hizo setelite ziko spinned katika orbit au zinatumia locomotive engenes kama jet engine katika kuvispeed up viendane sawa na speed ya dunia katika kulizunguka jua n at the same time katika kujizungusha yenyewe katika mhimili wake? Nataka kujua tafadhali
 
Nia yako ni nzuri,ila kuna tatizo humu jamvini,kama unafwatilia mada hii utakuja kuliona tatizo husika.

Mkuu Imany John hapa jamvini kuna maada nzuri sana kama hizi ila wachakachuaji ni wengi hasa wale wa ku-PROVE THAT BLAAH-BLAAH IS/ISN'T BLAAH-BLAAH ndio wanaotukosesha utam wa 3D

.made in mby city.
 


Wewe utakuwa umesahau ulivyofundishwa na mwalimu wako..
Fikiria tena
 
Mkuu soma Ayubu 26:10 " Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana"

Hivyo mkuu kama dunia ni duara kama shape basi isingekuwa na mipaka... ndo mana nikasema iko as disk... yani kana "cd" au kama ramani ya dunia katika bendera ya UN
 
Unaposema dunia ni flat una maanisha 2D (x,y) na kwa mtazamo wako kusingekuwa na milima ndani yake. Kimahesabu dunia inakuwa flat kama unachukua dunia kuwa kama tufe ikiwa na radius sawa kutoka katikati kwenda kwenye uso wa dunia (Tanget). Hii ni kwa ajili ya kurahisisha mahesabu. Lakini kiuhalisia Dunia haiko kama tufe dunia ina umbile la "Geoid" (sielewi kiswahili chake, labda u-google). Geoid inachukua umbile la duni kama unavyoona kwenye uso wa dunia kukiwa na mabonde, milima, nk. Kajifunze somo linaitwa Geodesy (Physical Geodesy and Geometrical Geodesy).
 


Kamanda naamini mleta mada na wengine washaelewa somo..
Big up
 
Tunapotengeneza ramani tunatengeneza ramani ikiwa katika 2D, yaani imebadilishwa kutoka 3D (Curved surface) kwenda 2D (Flat surface). Hii nafanyika kimahesabu zaidi kwa kutumia kile tunaita projection, na zipo projection za aina mbalimbali.
 

Mkuu jaribu kuangalia ramani ya dunia katika bendera ya UN... dunia sio flat as rectangle au mraba ni "duara flat" labda niseme hivyo
 

kutokana na fixed time and distance za destinations mbili inaonesha kuwa hakuna mzunguko wa dunia... kama mzunguko wa dunia ungekuwepo basi time na distance zingebadilika...
 

as UN Flag inavoonekana ndivo dunia ilivyo....ndilo umbile lake... katka kingo sijapata clues ambazo hata mm znazoni convince zaid... ila kuna hii ya Antarctica kuwa ni longest block of ice inayoaminika kuwa ndio mpka wa bahar....
nina weza nikaikubali hii kwa kutumia bible katika Ayub 26:10 " Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana"
 
Bado mtoa mada ana hoja za kufanyia kazi. ndege inaporuka inakua imeacha uso wa dunia hivyo ni kweli kama inaelekea mashariki basi umbali ungeongezeka na kama ingeelekea magharibi umbali ungepungua.
 
Acha uvivu wa kufikiri, kwa hiyo ulitegemea kuwa ndege inayotoka UK kwenda US inaweza tu kuganda hewani na baada ya muda wakatua USA? Ingekuwa hivyo hawa ndege warukao angani kama vile njiwa na kunguru ingekuwa shida sana kulenga (ku-aim) destinations zao, maana warukapo kutoka mti mmoja kwenda mwingine wasingeweza kuufikia maana speed ya dunia ni kubwa kuliko speed yao. Jibu ni kwamba vyote hivyo vyote ni sehemu ya dunia na tupo kwenye mzungo muda wote. Ili usiwe sehemu ya mzunguko huu unatakiwa utoke duniani na uende anga za mbali. Utafaidi kuona dunia ikizunguka kwa speed ya hatari.

Haya niliyajua nikiwa darasa la tano.
 
Kama ingekuwa flat si ingekuwa na mwisho au tutadai na yenyewe ni infinite....!? Nimewaza tu

Unapodai earth not round naweza nikakuunga mkono sababu shape ya earth ni irregular na siyo regular ila huwa inafanyiwa approximation kui-cover ionekane iko spherical ili iweze kufanyiwa mathematical computation hapa nahusisha survey of the earth kwa kuingiza concept ya Ellipsoid na Geoid ambapo kwenye survey huwa wana assume the earth distance is horizontal so slunt huwa haziwi considered so kwa kuwa shape of earth ina kuwa approximated hivyo ni rahisi kusema siyo round BUT THE EARTH IS NOT FLAT

Nimejaribu kukumbuka wakat nipo darasa la tatu/nne katika kipind cha sayansi tulifundishwa jinsi ya kupata mchana na usiku kwa kutumia round world map na torch sasa hii concept ukijaribu kui-apply kwenye flat earth tutapataje usiku na mchana?

Hapa najaribu kuhusisha na kuchelewa kwa mawio na macheo ya jua mfano hata hapa Tanzania mtu wa mtwara na kigoma wanatofautiana hata Marekani state zao zinatofauti ya masaa. Je ikiwa flat tutatofautiana kama hivi?

Jaribu kusafiri na meli/mtumbwi/mashua wakati wa alfajiri au jioni exactly utaona how the earth is spherical not flat kwa sababu ya mawio/ macheo ya jua na hii huwa ni Moja ya theory inayo-prove the earth is spherical
 

LITTLE HULK, it's OK nazidi kufungua mind yangu bado!!
Kama ni hvyo, Dunia imejishikisha au imeunganika nanini kwenye ncha zake???
Je waliowahi kufika huko kwenye ncha hzo kama za UN flag kama ulivyodai walishuhudia nn au shimo refuuu ambalo MTU au vitu huweza dumbukia???
 
Last edited by a moderator:

Sioni haja ya kujadili vitu ambavyo viko wazi kabisa. Kigezo cha kupima dunia does not ratate on its own axis kwa kutumia ndege sio sahihi kwa sababu ndege yenyewe imo kwenye mzunguko wa dunia. ni sawa na kusema ukiwa kwenye ndege economy class umekaa umbali wa mita nne kutoka chooni ambacho kiko nyuma halafu unasema eti kwenda chooni ni karibu sana kwa sababu unatembea opposite na elekeo wa ndege na kurudi kwenye kiti ni mbali sana eti kwa sababu ndege ina-speed kubwa kuliko kutembea. Wazo lako ni zuri la kuendelea kutafuta ukweli kwa wewe mwenyewe kwani wengine ukweli walishaujua siku nyingi!!!

Pila dunia ni flat, ili ni tatizo jingine la kukosa uelewa. Tayari naona una uelewa sijui kwa nini unashindwa kupata majibu. Kigezo cha bendera kusema dunia ni flat sio sahihi. Ulitaka bendera iwe na globe au mfano wa globe? Ikiwekwa kwenye bendera kama globe nchi nyingine zitaonekanaje? au globe liwe linazunguka au mtu azunguke, kitambaa chenyewe flat iweje picha isiwe flat? Hiyo ni another perspective of viewing the world kwa ajili ya purpose ya kuonyesha mataifa yote.

Dini ya Kikristo ilizinduliwa na Galileo kuwa dunia sio flat na wakaelewa, ila waislamu bado hawajazinduka, sijui dini za kijadi na wasiokuwa na dini wanamtazamoa gani. Ushauri: unaposhughulikia science usiingize dini au dini usiingize sayansi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…