as UN Flag inavoonekana ndivo dunia ilivyo....ndilo umbile lake... katka kingo sijapata clues ambazo hata mm znazoni convince zaid... ila kuna hii ya Antarctica kuwa ni longest block of ice inayoaminika kuwa ndio mpka wa bahar....
nina weza nikaikubali hii kwa kutumia bible katika Ayub 26:10 " Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana"
ninaposoma madai ya mtu kuwa DUNIA INAZUNGUKA JUA, basi wala sina haja ya kucomment katika uzi kama huo,, mtu kama huyo anahitajika kurudi darasa la tatu.
Usikubali elimu ya darasa iwe funguo ya kukufunga usifikiri kinyume na ulivyofundishwa.
ki.ukweli elimu ya darasani imefisha uwezo wa kufikiri wa watu wengi sana.
jitahidi kujifunza kutokana na mazingira huku ukirejea uliyofundishwa darasani mkuu na kupata hitimisho lililotokana na kufikiri kwako.
Hakuna jipya hapo, nadharia za dunia bapa zilikuwapo toka zama, lakini katika dunia ya leo ndugu yangu na maendeleo ya sayansi na teknolojia mpaka kiganjani kwako unaweza kupata satellite za dunia hii na hata sayari zingine, binadamu ameweza kunyambua mpaka formation ya jua lenyewe, vilivyomo na safari zake, bado watu wanaibua theories zilezile za enzi hizo na kujaribu kuzilinda kwa ngao zilezile za kijima, dunia ni bapa na jua linazunguka dunia?! inahitaji moyo mgumu sana kushadadia nadhari kama hizo katika miaka ya 2000!
bado nasisitiza sayansi,technologia au elimu nyingine yoyote isitumike kuwa switch kuondoa haki yako ya kibinadam ya kuhoji na kujiuliza maswala. dunia umbo lake hakuna anayetoa kwa usahihi ndiyo sababu kuna maelezo tofauti.
dunia kuzunguka bado kuna maswali ambayo wengone tunajiuliza ili tupate majibu.
mimi sayansi sio mbadala ya ubongo wangu. mtazamo wangu sayansi kwa kiwango kikubwa imefisha uwezo wa binadam kuitazama dunia katika mapama yake ya kimfumo kwa kumega mifumo yenye utendaji unaoingiliana kana kwamba kila mfumo unajitegemea
Dunia ni round, hilo hata halihitaji ubishi, picha zipo nyingi zinapigwa kila siku kutoka angani.
Kila kitu kilichomo ndani ya atmosphere, binadamu na ndege vyote wakati dunia inazunguka, inazunguka navyo pia kwa hiyo usidhani ndege itaruka afu umbali upungue, ingekua hivo basi hata chini hapa tungekua tukiruka tunatua kwingine.. For as long as kitu kimo ndani ya atmosphere basi dunia inavozunguka na chenyewe kinazunguka vilevile kwa speed ileile...
Afu angalia satellites zilizoko angani, kuna satellite zinaitwa geostationery ambazo zenyewe hua zinaonekana kama zimesimama, zile satellite kwa kua ziko nje kiasi kwamba haziwezi kuzungushwa na dunia, hua zinapewa speed sawa na speed ya dunia, sasa kiukweli ni kama zinaanguka vile sema zinaonekana stationery sababu zinaenda kwa speed sawa na speed ya mzunguko wa dunia..
kama dunia ingekua flat hivi inategemea jua lingeonekana kama linazama kwenda chini?? si lingeonekana linapita tu kutoka kulia kwenda kushoto, sio kuonekana linatoka chini linakuja juu afu linaenda chini tena...
Afu watu NASA mnawaona kama mashetani, wanaofanya kazi pale ni watu ka wewe na mimi, yaweza kua ndugu yako au rafiki, sio watu walioletwa kutoka kuzimu wale kusema wanazuia ndege kupita Antarctica, mbona watu wanaenda kule kila mwaka, we aliyekwambia wanazuia ni akina nani?? hakuna evidence yoyote kule kua dunia haizunguki wala si duara..
Jamani nunueni hata telescope basi za bei nafuu mtumie kuangalia mwezi au sayari nyingine za karibu muone kua ni duara na hivi vitu vipo kweli sio kwamba vinaandikwa tu.. huwezi danganya science ambayo ndo leo hii inakusaidia wewe unatumia jamiiforums
Mtu kama huyu muulize kwanza elimu yake ni ipi na katika mwaka uliopita wote kasoma vitabu vingapi na vipi.
Mtu anabisha dunia haiendi kwa sababu ya mwendo wa ndege wakati dunia inakwenda na atmosphere yote pamoja na ndege?
Haya ndiyo matatizo ya kuamini kila neno la biblia kama ukweli mtupu.
Unataka kuniambia Anga nalo linazunguka?
Anga linaenda na dunia kama vile ikiwa kwenye ndege inayokqenda kasi na kujubeba unavyoweza kukaa na kurusha shilingi halafu ukaidaka mkononi palepale. Hata kama ndege inaenda 1000 km/hr, ile shilingi haiendi kianguka nyuma ya ndege, kwa sababu na yenyewe ina kinetic energy ya mwendo wa ndege.
Hivyo hivyo, anga linaenda na dunia kina kinetic energy inayofanya anga la dunia liende na dunia, halafu gravity inafanya anga libaki lilipo.
Unapoangalia suala la dunia kuzunguka jua unatakiwa kuangalia dunia na anga lake, aiyo dunia kwa kuanzia ardhi tu.
Upande mmoja nakubaliana na wewe hasa mfano , lakini nikifikiria nje ya ndege huu mfano ngumu sana , Ila itanibidi nisome zaid , shukran
Kanuni za fizikia ndani ya ndege na nje ya ndege ni zile zile, hazibadiliki.
Mfano ukirusha hiyo shiling ukiwa nje ya ndege itadondoka hapo hapo?