The earth is flat and is not rotating

Pengine kweli
kwani

Geraldine “Jerrie” Mock, who has died at the age of 88, was the first woman to fly solo around the world. She was 38 on 19 March 1964 when she took off from Columbus, Ohio in a 1953 Cessna 180 single-engine monoplane named the Spirit of Columbus

Ilikuja fahamika hakuizunguka Dunia kwani njia alizopita ni sanaa tosha.
 

Kweli kabisa broo! Ona kinetic energy = Mass x Velocity. Lakini kama velocity ni zero yaani unapoishika shilingi basi kinetic energy huwa zero! Sasa unapoirusha juu unakuwa unaipatia final velocity kwa height fulani na hapo unatengeneza potential energy which is PE = Mass x g x height ambapo g ni acceleration due to gravity. Sasa kwa kuwa dunia hufanya circular motion then acceleration yake inatakiwa kuwa constant ili tusiyumbe barabarani so at any time t velocity ya shilingi itategemea initial velocity yaani Vf = Vi + at sasa kama a = g huoni t ndio itafanya utofauti!? Na uliona wapi g na a zikawa moja usione tofauti ukizingatia moja ina circular motion? Dunia haizunguki bana sawa na Geoncentric Theory of Gravimetric

Pangu Pakavu
 

Hahaha! mtanzania naona lugha ya picha inakuchanganya kidogo! imeandikwa "watu kama panzi" sio "watu ni panzi" LOL! wazungu wanaiita "simile" bahati mbaya kiswahili nilikua nadodge darasa mwalimu alikua anatandika sana siikumbuki inaitwaje...

kutokana na fixed time and distance za destinations mbili inaonesha kuwa hakuna mzunguko wa dunia... kama mzunguko wa dunia ungekuwepo basi time na distance zingebadilika...

Mkuu jaribu kuangalia ramani ya dunia katika bendera ya UN... dunia sio flat as rectangle au mraba ni "duara flat" labda niseme hivyo




Hujaielewa ile ramani ya UN.
Inajieleza vizuri. Itazame vizuri zaidi
Dunia ni mduara haina chembe ya ubishi.
 
Na kwa mkutadha huo huo abiria ambaye yuko siti ya nyuma akiamua kuhamia siti ya mbele karibu na dreva nadhani ingekuwa inamchukua muda mrefu sana maana kwa speed ya bus na speed ya abiria umbali kati ya hizo siti mbili ungeongezeka sana. Hapa nimechukulia bus ndo dunia na siti moja ni marekani na ya pili ni uingereza na huyo abiria ndo ndege yenyewe.
 







Ni kweli kabisa tatizo linaweza kuwa ni walimu waliofundisha baadhi ya watu hawakueleweka.

Picha inatafsiriwa kwa kuangalia front view,side view na top view.

Picha zote za dunia kwa upande wa side ,front na top view zinaonekana katka umbo la duara.
Hivyo Hakuna ubishi kuwa dunia ina umbo la tufe. Anayebisha na aendelee kubisha lakini sayansi imeprove hivyo na itaendelea kuwa hivyo.
 
Je, mkithibitisha wenyewe pasi na shaka kwamba dunia ni duara mtakuwa tayari kukiri vitabu vyenu(Bible/Quran) vimeandikwa uongo?
 

Hi kitu inayoitwa usawa WA bahari ni Kitu gani ? Maana Kama bahari ndiyo inatumika kuthibitisha umdwara WA dunia ni kwa vipi itumike Kama rejea ya miinuko ya sehemu nyingine ?
Mkuu toka kwenye box ulilowekwa na elimu / walaamu observe dunia ilivyo, nenda pwani ya bahari jiulize maswali kwamba hatuioni Zanzibar kwa kuwa Kati ya Zanzibar na Pwani ya pana maporomoko Kama ya mlima kitonga ndiyo yanazuia sisi bara na Zanzibar tusionane.
Tatizo sio la upeo na nguvu za amcho Bali ni nundu ya bahari ?
Ukiangalia meli iendayo Zanzibar bado utaona Kama inazama Ina maana ni kweli kuna maporomoko baharini ?
 
Je, mkithibitisha wenyewe pasi na shaka kwamba dunia ni duara mtakuwa tayari kukiri vitabu vyenu(Bible/Quran) vimeandikwa uongo?

Dunia inazunguka ? Duara likoje hadi lifananishwe na dunia yenye milima mirefu na mabonde makubwa ? Au Mimi ni zuzu kiasi cha kutojua hata maana ya duara ?
Zungumzia na kuzunguka mkuu , wapi maelezo yake ...
Kuhusu dunia kuzunguka kwangu itasalia kuwa ni moja ya scientific hoaxes zinazoaminiwa na wasomi mpaka itapothibitika vingenevyo.
 
Monstgala maoni yako tafadhali

Mkuu asante, ukweli usio na shaka ni kwamba Dunia ni duara na ina-rotate. There is overwhelming evidence and the opposing arguments are unjustifiable and might be due to ignorance or other unknown motives. With the technology and advancement in the field of Astronomy today the argument don't stand a chance. Infact, the focus is about universe and no longer Earth's shape and motion.
 

utaaminije kila kitu kuwa ni kweli as long ushaambiwa imekuwa proved with science evidence???
Ngoja nikupe mfano.. wewe najua umesoma geography unajua kuhusu the earth crust.... right?.... sasa angalia mchoro huu
..... unaambia kuna layer sijui tatu ufike katika inner core of the earth... na kuna sijui mental laye na crust layer... swali linakuja wamejuaje kama kweli beneath the earth kuna structure za namna hii kama sio kutunga tu...

kama unafahamu kola borehole ya russia ambayo ilianza miaka ya 1970s mwishon na kufungwa mwaka 1992 walichimba shimo or a hole lenye urefu wa kilometer 12 na ndilo shimo kubwa kuchimbwa na mwanadamu... sasa swali je, from the crust to the center of the earth "core" wameijuaje wakati mwisho walifikia 12km....

so kama haujanielewa vizuri jaribu kutafuta hii issue ya kola borehole utaelewa kuwa tunadanganywa vingi....
 

mkuu hebu angalia .... je jibu litafanana endapo mtu akitoka kiti cha nyuma na kwenda kiti cha dereva kwa kutembea .... na mti akitoka kiti cha nyuma kwenda kenywe kiti cha dereva kwa kupaa?
 
kuna hii kuwa kila jicho litamuona..... so atakuja in different time to different location?.... myself I dont know..

unajua katika kutafuta ukweli tusi base upande mmoja kwamba we need to prove scientifically kila kitu... tuangalie pande zote.... maana inawezekana ikafika point vika balance na ukweli ukapatikana
 




Kutokana na vitabu na tafiti za kisayansi ni kwamba dunia wakati ilipokuwa inameguka kutoka kwenye jua ilikua ktk hali ya gesi kutokana na joto kali sana. Huku kurushwa kwa umbali mrefu na kwa speed kubwa kuliifanya dunia iliyokua inaendelea kupoa na kuwa kama uji iwe na umbo la mviringo.Ilipoanza kupoa ilibadilika nakuanza kufanya mvuke uliokua unasababisha mvua nyingi sana.Hii mvua ndiyo iliyosababisha dunia ifunikwe na maji maeneo yote. Hapakuwa na eneo la nchi kavu . Wakati huo presha na joto ndani ya dunia ilikuwa ni kubwa mno hivyo kusabisha ndani yake kuwe na hali ya uji au magma. Huu uji ulikua unagandamizwa hivyo ukawa unatafuta eneo lenye udhaifu na kulisukuma kwenda juu na wakati mwingine ulikua unaoenya na kumwagika nje kama volkeno.Pale uliosukuma eneo fulani juu ulisababisha mlima kutokea. Na pale ulipotoka ukasababisha bonde.Ndio maana mpaka baharini kuna milima na mabonde.
Milima mirefu sana baharini inakuwa ni visiwa.
 

Kwa maelezo yako umviringo WA dunia ni WA kabla ya milima ? Mimi sikuuliza namna dunia ilivyoumba milima yake. Nimezungumzia hoja ya mwonekano WA meli kwa mbali ati inathibitosha kuwa dunia ni mviringo.
Achana na ulivyofundishwa angalia dunia then tafakari kujiridhisha ukweli WA Elimu uliyopewa kuhusu dunia.
 

Ungedokeza hizo "overwhelming " evidence tuone namna zinavyojibu maswali yetu ya kijinga.

Duara likoje kwa mujibu WA huo utafiti ? Au dunia inayohusika kuwa duara mabonde na milima haimo ?
Ama kuhusu ukweli usio shaka ? Ni ukweli gani katika sayansi ambao unakuwa hauna Shaka ?
Hauna Shaka kwa nani ? Ina maanisha baada ya kupata huo ukweli usio na Shaka utafiti kwenye eneo husika umefungwa ?
Ni kweli yaweza kuwa ni Ujinga Tu au sababu zingine kwa upande WA wanaopinga dunia kuwa duara na kuzunguka kwake.
Vivyo hivyo yaweza kuwa pia ni Ujinga au sababu za kimkakati kusema dunia ni duara na inszunguka kutoka upande WA wamasayansi ni ukweli ulio wazi mno kwamba kuna taafiti za kisayansi ambazo matokeo yanatangulia utafiti ili kukidhi haja ya wadhamini WA tafiti husika.
Focus hapa ni dunia tuache kile astrology walichofocus
 




Elimu tuliyopewa ni sahihi sana.
Hata unapotaka kusomea urubani au nahodha wa meli ni lazima atumie longitudo ,latitudo na mistari ya grid reference ambayo ni mistari ya kubuni kisayansi.Ni vigumu kutumia mistari hiyo kwa umbo lisilofanana na tufe.

Suala la meli na bahari ni kwamba uwiano wa ukubwa wa eneo unaloliona na ukubwa wa mduara wa dunia ni mdogo sana .Ni kama chembe ya vumbi kwenye mpira. Ndio maana kwa haraka unaona kama bahari ni tambarare. Ni ukweli kuwa sababu ya kuiona meli na jua likiwa linazama ni moja ya sababu zilizopelekea watafiti kuwa na mtizamo zaidi wa kutafiti umbo halisi la dunia.

Na moja ya ushahidi wa umbo la dunia ni picha zinazopigwa kwa kutumia satelite.
Mfano unapotaka kujenga nyumba kwa kutumia picha na ramani ni lazima utumie picha zilizopigwa pande zote ili upate umbo kamili la nyumba.
Ni lazima upate picha zinayoonyesha frot elevation/frot view, side elevation/side view na plan elevation/top elevation.Kwa kutumia utaalam huu wa picha ni ukweli kuwa huwa tunajenga nyumba inayofanana kabisa na kusudio letu.

Tukirudi kwenye mada ni hali kama hiyo ya kutumia picha mbalimbali zilizopigwa kuzunguka dunia zinaonyesha kuwa dunia ni mviringo kwa kila upande uliopigwa picha.Side view ,front view na top view zote zinaonyesha mduara.Hivyo hata ukimpa fundi ujenzi kazi ya kujenga nyumba yenye umbo la dunia na kumpa picha na ramani ya dunia halafu wewe ukakaa kimya atakujengea nyumba yenye umbo la tufe.
 

bado dunia haijakibali kutoa siri zake... Ni sisi Tu tunaotunga tunga hizi assumptions
 

Bado hoja za picha ni za kusadikika zaidi na mfano WA nyumba na dunia ni sawa na mfano WA usiku kwa mchana. Unakuwa upande gani wa dunia unapoipiga picha sides au wewe unasimama angani kusubiri mzunguko WA dunia ukulete sides tofauti ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…