The earth is flat and is not rotating

The earth is flat and is not rotating

Pengine kweli
kwani

Geraldine “Jerrie” Mock, who has died at the age of 88, was the first woman to fly solo around the world. She was 38 on 19 March 1964 when she took off from Columbus, Ohio in a 1953 Cessna 180 single-engine monoplane named the Spirit of Columbus

Ilikuja fahamika hakuizunguka Dunia kwani njia alizopita ni sanaa tosha.
 
Hizi law zote zimejaa assumptions tupu , kiti hakiko katika motion lazima idondoke hapo hapo , panda piki piki piga mafuta ya kutosha rusha hiyo pesa juu kama utaidaka tena , lazima itadondoka nyuma tu

Lile swala la ndege naliunga mkono 100% hasa inapokua inaenda uelekeo tofaut na dunia , lazima umbal upungue , na ikienda sambamba na dunia umbal lazima uongozeke

Dunia ina mwendo wake

ndege ina wake , Sidhan kama universe inazunguka , hili n jipya nalisikia kwako nitajitahd kulifuatilia

Kweli kabisa broo! Ona kinetic energy = Mass x Velocity. Lakini kama velocity ni zero yaani unapoishika shilingi basi kinetic energy huwa zero! Sasa unapoirusha juu unakuwa unaipatia final velocity kwa height fulani na hapo unatengeneza potential energy which is PE = Mass x g x height ambapo g ni acceleration due to gravity. Sasa kwa kuwa dunia hufanya circular motion then acceleration yake inatakiwa kuwa constant ili tusiyumbe barabarani so at any time t velocity ya shilingi itategemea initial velocity yaani Vf = Vi + at sasa kama a = g huoni t ndio itafanya utofauti!? Na uliona wapi g na a zikawa moja usione tofauti ukizingatia moja ina circular motion? Dunia haizunguki bana sawa na Geoncentric Theory of Gravimetric

Pangu Pakavu
 
Habarini,

Katika pitapita zangu za kujua vitu nikakuta hii kitu kuhusiana na dunia kutokuwa ni duara na ni tambarale pia haizunguki katika muhimili wake kama tulivofundishwa huko shule za awali.

Kuna baadhi ya ushahid unaotokana na mazingira jinsi yalivo pamoja na udini kidogo...

1. kwa mazingira jinsi yalivyo:

Kwanza kuhusu "earth is not rotating" .... kawaida dunia inazunguka jua kwa muda siku 365 na hujizungusha katika muhimil wake kwa muda wa masaa 24 kumaliza mzunguko wake, na ndipo tunapata usiku na mchana.... (hivi ndivo navojua mm na wewe)

lakini kuna maelezo yanayo onyesha kuwa dunia haijizungushi bali jua na vilivo juu vinaizunguka dunia. proof wanaosema kwamba dunia haizunguki ni hii ya usafiri wa ndege.

Tuanze kwa kusema kwamba dunia inajizungusha katika muhimili wake kwa speed ya 6070 km/hr kutokea magharibi kwenda mashariki, ndio maana tunapata kuona jua linachomoza kutokea mashariki na kuzama magharibi.

Sasa tuchuke mfano ndege inatokea marekani (Washington DC) kwenda uingereza (London). Hivyo ndege inatoka magharibi kwenda mashariki. Umbali kutoka marekani mpaka uingereza ni 5934.6 km na inachukua masaa 7 na dakika 39, hivyo ndege husafiri katika umbali huo kwa 775.76 km/hr. Hivyo kama dunia inakuwa katika speed yake ya 1675 km/hr basi huu umbali ungeongezeka zaid maana dunia ingekuwa inazidi kwenda mbele kutoka magharibi kwenda mashariki na ndege hiyo kwa speed hiyo ya 775.76 km/hr. [lets assume kwamba umbali huo unatokana na speed ya dunia na speed ya ndege kutoka magharib kwenda mashariki]

JE, KAMA NDEGE INATOKA UINGEREZA KWENDA MAREKANI UMBALI UTAKAO KUWA COVERED NA NDEGE UTAKUWA SAWA NA WA MWANZO (5934.6 KM) KAMA DUNIA INAJIZUNGUSHA KUTOKA MAGHARIBI KWENDA MASHARIKI?

JIBU NI HAPANA, MAANA KAMA NDEGE INATOKA MASHARIKI KWENDA MAGHARIBI NA DUNIA INAZUNGUKA KUTOKA MAGHARIBI KWENDA MASHARIKI BASI UMBALI UTAPUNGUA MAANA DUNIA NA JUA ZITAKUWA OPPOSITE DIRECTION.

View attachment 216726

Lakini kiuhalisia umbali utakuwa ni huohuo na masaa ya kusafiri yatakuwa ni hayohayo... HIVYO HII INAONESHA KUWA DUNIA HAIZUNGUKI.

Pili kuhusu "the earth is flat and not round".... bado kuna debate zinaendelea kuelezea kivipi dunia ni flat na sio duara kama tunavojua. Ila katika hili kuna maswali mengi sana, maana kuna issues za horizon, light, space and sky ceiling, land curvature ambazo mm mwenyewe binafsi naendelea kuzifatilia ila kwa sasa sina clue ambazo zitani support kuelezea kivip dunia ni tambarale.

Ila inasemekana dunia ina umbo la flat disk kama hii.

View attachment 216727

Hii ni bendera ya United Nations na ramani yake ya dunia iko tofauti na ramani ambazo tunazozijua. Hivyo inasemekana kuna siri katika shape ya dunia. flat earth society wanaamini kuwa dunia iko hivyo ila kwa pande nne sio round kama inavoonekana kwenye hiyo picha juu.

Pia kuhusu maji ya bahari kuna kuta za barafu zinashilia hayo maji. Hii inawezekana baada ya ile mada ya kuto kuwepo kwa south pole kule Antarctica.

Kunasemekana Antarctica ni kubwa kuliko tunavoiona katika ramani, pia ndiko kunakoaminika kuwa ni kitovu kitakocho onyesha kuwa dunia sio duara bali ni tambarale.

Maana hakuna ndege inayoruhusiwa kipita katika anga la Antarctica. Jiulize, Kina "NASA" wanadai wameenda mwezini, wametuma vifaa vya kisasa huko sayari mars na vyengine mbali zaid lakini wameshindwa kupita juu ya Antarctica kisa ni baridi kali... JIULIZE!!!!!!

2. Udini:

Katka udini nitazungumzia katika upande wa imani ya kikristo.

1. katika agano la kale yoshua alisimamisha jua. Yoshua 10: 12-13 "12 Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni;

Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
13 Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao."

hii inaonyesha kuwa Jua ndilo linalozunguka dunia na sio dunia linazunguka Jua, Hivyo dunia haizunguki na iko stationary

2. katika agano jipya shetani alimchukua Yesu mpaka mahali pa juu na kumuonyesha ulimwengu wote:
Luka 4 : 5 -8

5 Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,

6 Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza. 7 Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."

8
Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake."

kama dunia ingekuwa duara basi ingekuwa haiwezekani kwa falme zote za ulimwengu kuonekana kwa mara moja.

3. malaika wanne katika kona za nchi:

Ufunuo 7 : 1

"1 Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote."

hii inaonesha kuwa dunia pia sio duara, maana kama ni round hizo pembe nne za nchi zitapatikanaje?. Hivyo dunia might be square or rectangle.

TUJADILI ZAID NI HAYA NILIYOYAKUTA KATIKA KUJUA ZAID...... THANKS

Hahaha! mtanzania naona lugha ya picha inakuchanganya kidogo! imeandikwa "watu kama panzi" sio "watu ni panzi" LOL! wazungu wanaiita "simile" bahati mbaya kiswahili nilikua nadodge darasa mwalimu alikua anatandika sana siikumbuki inaitwaje...

kutokana na fixed time and distance za destinations mbili inaonesha kuwa hakuna mzunguko wa dunia... kama mzunguko wa dunia ungekuwepo basi time na distance zingebadilika...

Mkuu jaribu kuangalia ramani ya dunia katika bendera ya UN... dunia sio flat as rectangle au mraba ni "duara flat" labda niseme hivyo

Hujaielewa ile ramani ya UN.
Inajieleza vizuri. Itazame vizuri zaidi
Dunia ni mduara haina chembe ya ubishi.
 
labda tumuongezee tu kuhusu dunia kuzunguka na vitu vyote vilivyomo ndani.
mfano mzur ni pale nzi anapokuwa anafly ndani ya basi lililo kwenye mwendo, kwa idea ya mleta mada ilibidi nzi asiende sawa na basi na hvyo angejigonga kwenye kioo cha nyuma cha basi. but kama tunavyoshuhudiaga ni kuwa nzi nae huenda sawa na basi bila ya kujigonga.
Na kwa mkutadha huo huo abiria ambaye yuko siti ya nyuma akiamua kuhamia siti ya mbele karibu na dreva nadhani ingekuwa inamchukua muda mrefu sana maana kwa speed ya bus na speed ya abiria umbali kati ya hizo siti mbili ungeongezeka sana. Hapa nimechukulia bus ndo dunia na siti moja ni marekani na ya pili ni uingereza na huyo abiria ndo ndege yenyewe.
 
Mkuu nakuelewa sana unachomaanisha kwani niko hapo hapo

Suala la kuzunguka dunia liko kinadharia zaidi na hakuna uthibitisho wa kutosha

Suala la um bo la dunia kuna mdau hapo juu amezungumza dunia ni duara lakini ni kama CD hivi na sio kama ambavyo tunaambiwa

Haya mawazotofauti na yanayoonekana kama ya kizamani kuna wakati yana umuhimu mkubwa sana na ninayakubali baadhi kwa kutoa changamoto kwa wale ambao wameganda kwenye vitabu na dhana za wanasayansi

Ukiangalia mfano hoja ya mtoa mada ya ndege,tunaambiwa kuwa dunia inazunguka na "anga lake",sijui kwanza hii inakuwa inaashiria nini

Wanasema hii inatokana na gravity ya dunia,sijui ni kwa namna gani inaweza kuzungusha kijisehemu tu cha anga na sio anga yote

Mkuu haya mambo mimi siyaelewi na naendelea kujifunza,ngoja tuendelee kuwasoma wadau na watafiti lakini kuna uongo mkubwa sana humu duniani na watu wako tayari hata kufa wakiutetea huku wakidhani ni ukweli

N inachoweza kushauri ni kwamba if you continue to trust these people,proceed carefully!

Duuh,nipe aya mkuu nikasome nione hiyo Quraan inavosema.
Najua wengi tulisoma Geography,tatizo ni uafahamu wetu au walimu wetu walivyokuwa wanafundisha kama dunia ni duara aua la.
Kwa nilikopita na vitabu nilivyosoma dunia ni duara nami nilamini hivyo
Evidence ninazozikumbuka.
1😀unia ni duara na si tambarare kama meza,ingekuwa tambarare ukienda baharini ship inapo ondoka ingekuwa inaonekana muda wote kama haikati kona ,lakini kwa sababu kuna ellipse shape inapotea baada ya kwenda umbali fulani.Dunia ingekuwa tambarare meli zisingekuwa zinapotea zingekuwa zinaonekana muda wote.
2.Kama dunia ingekuwa tambarare na si spherical jua lingekuwa linachomoza na kuzama muda mmoja duniani kote,na time difference isingekuwepo.
3.Kama dunia ingekuwa ni tambarare duniani kote mchana ungekuwa ni mmoja na usiku ni mmoja,kwa sasa unakuta Tz ni mchana na nchi nyingine ni usiku.Kusingekuwa na kupoteza siku au kugain ukisafiri kutoka bara moja kwenda jingine.

Tunachotakiwa kujua dunia ni kubwa sana kama sikajahau radius ya ni kama km 6370( am not sure long time) kwa hiyo unaweza kuwa sehemu ukaona tambalale na kuhisi dunia ni tambalale kwa sababu uko kwenye eneo dogo kati ya eneo kubwa.Fikiria sisimizi yuko juu ya mpira unazani anaona kama ni duara?

Ni kweli kabisa tatizo linaweza kuwa ni walimu waliofundisha baadhi ya watu hawakueleweka.

Picha inatafsiriwa kwa kuangalia front view,side view na top view.

Picha zote za dunia kwa upande wa side ,front na top view zinaonekana katka umbo la duara.
Hivyo Hakuna ubishi kuwa dunia ina umbo la tufe. Anayebisha na aendelee kubisha lakini sayansi imeprove hivyo na itaendelea kuwa hivyo.
 
Je, mkithibitisha wenyewe pasi na shaka kwamba dunia ni duara mtakuwa tayari kukiri vitabu vyenu(Bible/Quran) vimeandikwa uongo?
 
Hi kitu inayoitwa usawa WA bahari ni Kitu gani ? Maana Kama bahari ndiyo inatumika kuthibitisha umdwara WA dunia ni kwa vipi itumike Kama rejea ya miinuko ya sehemu nyingine ?
Mkuu toka kwenye box ulilowekwa na elimu / walaamu observe dunia ilivyo, nenda pwani ya bahari jiulize maswali kwamba hatuioni Zanzibar kwa kuwa Kati ya Zanzibar na Pwani ya pana maporomoko Kama ya mlima kitonga ndiyo yanazuia sisi bara na Zanzibar tusionane.
Tatizo sio la upeo na nguvu za amcho Bali ni nundu ya bahari ?
Ukiangalia meli iendayo Zanzibar bado utaona Kama inazama Ina maana ni kweli kuna maporomoko baharini ?
 
Je, mkithibitisha wenyewe pasi na shaka kwamba dunia ni duara mtakuwa tayari kukiri vitabu vyenu(Bible/Quran) vimeandikwa uongo?

Dunia inazunguka ? Duara likoje hadi lifananishwe na dunia yenye milima mirefu na mabonde makubwa ? Au Mimi ni zuzu kiasi cha kutojua hata maana ya duara ?
Zungumzia na kuzunguka mkuu , wapi maelezo yake ...
Kuhusu dunia kuzunguka kwangu itasalia kuwa ni moja ya scientific hoaxes zinazoaminiwa na wasomi mpaka itapothibitika vingenevyo.
 
Monstgala maoni yako tafadhali

Mkuu asante, ukweli usio na shaka ni kwamba Dunia ni duara na ina-rotate. There is overwhelming evidence and the opposing arguments are unjustifiable and might be due to ignorance or other unknown motives. With the technology and advancement in the field of Astronomy today the argument don't stand a chance. Infact, the focus is about universe and no longer Earth's shape and motion.
 
Ni kweli kabisa tatizo linaweza kuwa ni walimu waliofundisha baadhi ya watu hawakueleweka.

Picha inatafsiriwa kwa kuangalia front view,side view na top view.

Picha zote za dunia kwa upande wa side ,front na top view zinaonekana katka umbo la duara.
Hivyo Hakuna ubishi kuwa dunia ina umbo la tufe. Anayebisha na aendelee kubisha lakini sayansi imeprove hivyo na itaendelea kuwa hivyo.

utaaminije kila kitu kuwa ni kweli as long ushaambiwa imekuwa proved with science evidence???
Ngoja nikupe mfano.. wewe najua umesoma geography unajua kuhusu the earth crust.... right?.... sasa angalia mchoro huu
download.jpg ..... unaambia kuna layer sijui tatu ufike katika inner core of the earth... na kuna sijui mental laye na crust layer... swali linakuja wamejuaje kama kweli beneath the earth kuna structure za namna hii kama sio kutunga tu...

kama unafahamu kola borehole ya russia ambayo ilianza miaka ya 1970s mwishon na kufungwa mwaka 1992 walichimba shimo or a hole lenye urefu wa kilometer 12 na ndilo shimo kubwa kuchimbwa na mwanadamu... sasa swali je, from the crust to the center of the earth "core" wameijuaje wakati mwisho walifikia 12km....

so kama haujanielewa vizuri jaribu kutafuta hii issue ya kola borehole utaelewa kuwa tunadanganywa vingi....
 
Na kwa mkutadha huo huo abiria ambaye yuko siti ya nyuma akiamua kuhamia siti ya mbele karibu na dreva nadhani ingekuwa inamchukua muda mrefu sana maana kwa speed ya bus na speed ya abiria umbali kati ya hizo siti mbili ungeongezeka sana. Hapa nimechukulia bus ndo dunia na siti moja ni marekani na ya pili ni uingereza na huyo abiria ndo ndege yenyewe.

mkuu hebu angalia .... je jibu litafanana endapo mtu akitoka kiti cha nyuma na kwenda kiti cha dereva kwa kutembea .... na mti akitoka kiti cha nyuma kwenda kenywe kiti cha dereva kwa kupaa?
 
kuna hii kuwa kila jicho litamuona..... so atakuja in different time to different location?.... myself I dont know..

unajua katika kutafuta ukweli tusi base upande mmoja kwamba we need to prove scientifically kila kitu... tuangalie pande zote.... maana inawezekana ikafika point vika balance na ukweli ukapatikana
 
Ni kweli kabisa tatizo linaweza kuwa ni walimu waliofundisha baadhi ya watu hawakueleweka.

Picha inatafsiriwa kwa kuangalia front view,side view na top view.

Picha zote za dunia kwa upande wa side ,front na top view zinaonekana katka umbo la duara.
Hivyo Hakuna ubishi kuwa dunia ina umbo la tufe. Anayebisha na aendelee kubisha lakini sayansi imeprove hivyo na itaendelea kuwa hivyo.

Hi kitu inayoitwa usawa WA bahari ni Kitu gani ? Maana Kama bahari ndiyo inatumika kuthibitisha umdwara WA dunia ni kwa vipi itumike Kama rejea ya miinuko ya sehemu nyingine ?
Mkuu toka kwenye box ulilowekwa na elimu / walaamu observe dunia ilivyo, nenda pwani ya bahari jiulize maswali kwamba hatuioni Zanzibar kwa kuwa Kati ya Zanzibar na Pwani ya pana maporomoko Kama ya mlima kitonga ndiyo yanazuia sisi bara na Zanzibar tusionane.
Tatizo sio la upeo na nguvu za amcho Bali ni nundu ya bahari ?
Ukiangalia meli iendayo Zanzibar bado utaona Kama inazama Ina maana ni kweli kuna maporomoko baharini ?

Kutokana na vitabu na tafiti za kisayansi ni kwamba dunia wakati ilipokuwa inameguka kutoka kwenye jua ilikua ktk hali ya gesi kutokana na joto kali sana. Huku kurushwa kwa umbali mrefu na kwa speed kubwa kuliifanya dunia iliyokua inaendelea kupoa na kuwa kama uji iwe na umbo la mviringo.Ilipoanza kupoa ilibadilika nakuanza kufanya mvuke uliokua unasababisha mvua nyingi sana.Hii mvua ndiyo iliyosababisha dunia ifunikwe na maji maeneo yote. Hapakuwa na eneo la nchi kavu . Wakati huo presha na joto ndani ya dunia ilikuwa ni kubwa mno hivyo kusabisha ndani yake kuwe na hali ya uji au magma. Huu uji ulikua unagandamizwa hivyo ukawa unatafuta eneo lenye udhaifu na kulisukuma kwenda juu na wakati mwingine ulikua unaoenya na kumwagika nje kama volkeno.Pale uliosukuma eneo fulani juu ulisababisha mlima kutokea. Na pale ulipotoka ukasababisha bonde.Ndio maana mpaka baharini kuna milima na mabonde.
Milima mirefu sana baharini inakuwa ni visiwa.
 
Kwa maelezo yako umviringo WA dunia ni WA kabla ya milima ? Mimi sikuuliza namna dunia ilivyoumba milima yake. Nimezungumzia hoja ya mwonekano WA meli kwa mbali ati inathibitosha kuwa dunia ni mviringo.
Achana na ulivyofundishwa angalia dunia then tafakari kujiridhisha ukweli WA Elimu uliyopewa kuhusu dunia.
 
Mkuu asante, ukweli usio na shaka ni kwamba Dunia ni duara na ina-rotate. There is overwhelming evidence and the opposing arguments are unjustifiable and might be due to ignorance or other unknown motives. With the technology and advancement in the field of Astronomy today the argument don't stand a chance. Infact, the focus is about universe and no longer Earth's shape and motion.

Ungedokeza hizo "overwhelming " evidence tuone namna zinavyojibu maswali yetu ya kijinga.

Duara likoje kwa mujibu WA huo utafiti ? Au dunia inayohusika kuwa duara mabonde na milima haimo ?
Ama kuhusu ukweli usio shaka ? Ni ukweli gani katika sayansi ambao unakuwa hauna Shaka ?
Hauna Shaka kwa nani ? Ina maanisha baada ya kupata huo ukweli usio na Shaka utafiti kwenye eneo husika umefungwa ?
Ni kweli yaweza kuwa ni Ujinga Tu au sababu zingine kwa upande WA wanaopinga dunia kuwa duara na kuzunguka kwake.
Vivyo hivyo yaweza kuwa pia ni Ujinga au sababu za kimkakati kusema dunia ni duara na inszunguka kutoka upande WA wamasayansi ni ukweli ulio wazi mno kwamba kuna taafiti za kisayansi ambazo matokeo yanatangulia utafiti ili kukidhi haja ya wadhamini WA tafiti husika.
Focus hapa ni dunia tuache kile astrology walichofocus
 
Kwa maelezo yako umviringo WA dunia ni WA kabla ya milima ? Mimi sikuuliza namna dunia ilivyoumba milima yake. Nimezungumzia hoja ya mwonekano WA meli kwa mbali ati inathibitosha kuwa dunia ni mviringo.
Achana na ulivyofundishwa angalia dunia then tafakari kujiridhisha ukweli WA Elimu uliyopewa kuhusu dunia.

Elimu tuliyopewa ni sahihi sana.
Hata unapotaka kusomea urubani au nahodha wa meli ni lazima atumie longitudo ,latitudo na mistari ya grid reference ambayo ni mistari ya kubuni kisayansi.Ni vigumu kutumia mistari hiyo kwa umbo lisilofanana na tufe.

Suala la meli na bahari ni kwamba uwiano wa ukubwa wa eneo unaloliona na ukubwa wa mduara wa dunia ni mdogo sana .Ni kama chembe ya vumbi kwenye mpira. Ndio maana kwa haraka unaona kama bahari ni tambarare. Ni ukweli kuwa sababu ya kuiona meli na jua likiwa linazama ni moja ya sababu zilizopelekea watafiti kuwa na mtizamo zaidi wa kutafiti umbo halisi la dunia.

Na moja ya ushahidi wa umbo la dunia ni picha zinazopigwa kwa kutumia satelite.
Mfano unapotaka kujenga nyumba kwa kutumia picha na ramani ni lazima utumie picha zilizopigwa pande zote ili upate umbo kamili la nyumba.
Ni lazima upate picha zinayoonyesha frot elevation/frot view, side elevation/side view na plan elevation/top elevation.Kwa kutumia utaalam huu wa picha ni ukweli kuwa huwa tunajenga nyumba inayofanana kabisa na kusudio letu.

Tukirudi kwenye mada ni hali kama hiyo ya kutumia picha mbalimbali zilizopigwa kuzunguka dunia zinaonyesha kuwa dunia ni mviringo kwa kila upande uliopigwa picha.Side view ,front view na top view zote zinaonyesha mduara.Hivyo hata ukimpa fundi ujenzi kazi ya kujenga nyumba yenye umbo la dunia na kumpa picha na ramani ya dunia halafu wewe ukakaa kimya atakujengea nyumba yenye umbo la tufe.
 
Kutokana na vitabu na tafiti za kisayansi ni kwamba dunia wakati ilipokuwa inameguka kutoka kwenye jua ilikua ktk hali ya gesi kutokana na joto kali sana. Huku kurushwa kwa umbali mrefu na kwa speed kubwa kuliifanya dunia iliyokua inaendelea kupoa na kuwa kama uji iwe na umbo la mviringo.Ilipoanza kupoa ilibadilika nakuanza kufanya mvuke uliokua unasababisha mvua nyingi sana.Hii mvua ndiyo iliyosababisha dunia ifunikwe na maji maeneo yote. Hapakuwa na eneo la nchi kavu . Wakati huo presha na joto ndani ya dunia ilikuwa ni kubwa mno hivyo kusabisha ndani yake kuwe na hali ya uji au magma. Huu uji ulikua unagandamizwa hivyo ukawa unatafuta eneo lenye udhaifu na kulisukuma kwenda juu na wakati mwingine ulikua unaoenya na kumwagika nje kama volkeno.Pale uliosukuma eneo fulani juu ulisababisha mlima kutokea. Na pale ulipotoka ukasababisha bonde.Ndio maana mpaka baharini kuna milima na mabonde.
Milima mirefu sana baharini inakuwa ni visiwa.

bado dunia haijakibali kutoa siri zake... Ni sisi Tu tunaotunga tunga hizi assumptions
 
Elimu tuliyopewa ni sahihi sana.
Hata unapotaka kusomea urubani au nahodha wa meli ni lazima atumie longitudo ,latitudo na mistari ya grid reference ambayo ni mistari ya kubuni kisayansi.Ni vigumu kutumia mistari hiyo kwa umbo lisilofanana na tufe.

Suala la meli na bahari ni kwamba uwiano wa ukubwa wa eneo unaloliona na ukubwa wa mduara wa dunia ni mdogo sana .Ni kama chembe ya vumbi kwenye mpira. Ndio maana kwa haraka unaona kama bahari ni tambarare. Ni ukweli kuwa sababu ya kuiona meli na jua likiwa linazama ni moja ya sababu zilizopelekea watafiti kuwa na mtizamo zaidi wa kutafiti umbo halisi la dunia.

Na moja ya ushahidi wa umbo la dunia ni picha zinazopigwa kwa kutumia satelite.
Mfano unapotaka kujenga nyumba kwa kutumia picha na ramani ni lazima utumie picha zilizopigwa pande zote ili upate umbo kamili la nyumba.
Ni lazima upate picha zinayoonyesha frot elevation/frot view, side elevation/side view na plan elevation/top elevation.Kwa kutumia utaalam huu wa picha ni ukweli kuwa huwa tunajenga nyumba inayofanana kabisa na kusudio letu.

Tukirudi kwenye mada ni hali kama hiyo ya kutumia picha mbalimbali zilizopigwa kuzunguka dunia zinaonyesha kuwa dunia ni mviringo kwa kila upande uliopigwa picha.Side view ,front view na top view zote zinaonyesha mduara.Hivyo hata ukimpa fundi ujenzi kazi ya kujenga nyumba yenye umbo la dunia na kumpa picha na ramani ya dunia halafu wewe ukakaa kimya atakujengea nyumba yenye umbo la tufe.

Bado hoja za picha ni za kusadikika zaidi na mfano WA nyumba na dunia ni sawa na mfano WA usiku kwa mchana. Unakuwa upande gani wa dunia unapoipiga picha sides au wewe unasimama angani kusubiri mzunguko WA dunia ukulete sides tofauti ?
 
Back
Top Bottom