The Emperor Jean-Bedel Bokassa

The Emperor Jean-Bedel Bokassa

yaan dunian tunapita!! tujiangalie!! weng wanadhan mambo yatakua kama jana. hawajui ya kwesho. tutende hak kwa wote
 
Miongoni mwa watawala waliokuwa na visa na vituko vingi katika bara hili la Afrika ni mfalme wa kujipachika wa Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa.

Jean Bedel Bokassa akiwa anaongoza nchi masikini kabisa duniani, alifanya sherehe ya kujisimika kama mfalme mwaka 1977 kwa kutumia kiasi cha sawa na shilingi bilioni 32 za Kitanzania za wakati huu. Lile taji lake la Ufalme peke yake liligharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu!.

Jean Bedel Bokassa alikuwa dikteta wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Alikuwa na wake kumi na saba (17) na watoto hamsini (50).

Alifanywa yatima wafaransa walipomuua baba yake akiwa na miaka sita (6) baada ya baba yake kufa mama yake naye alijiua.

Alipata kupigana vita ya pili ya dunia chini ya Wafaransa. Baadaye alikuja kumpindua rais aliyekuwa ndugu yake mwaka 1965. Alijipa cheo cha field marshall na kutengeneza uniform maalumu sababu ya wingi wa medals alizojipa. Akienda kutembelea nchi alikuwa anagawa almasi.

Alikuwa ana majumba zaidi ya sita Ufaransa. Pia alikuwa na majumba mengine nchi mwake, katika majumba yake mengine yaliyokuwa nchini mwake, Jumba lake mojawapo lilikuwa na bwawa la mamba na simba wa kufugwa, alitumia mamba hao na simba kuulia wapinzani wake.

Wake zake walikuwa Mchina, Mjerumani, Msweden, Mtunisia na Mromania. Aliwaweka nyumba tofauti na alikuwa akiwatembelea kila siku na kusababisha foleni kubwa barabarani kutoka na wingi wa safari hizo huku akiambatana na misafara.

Alipinduliwa na wafaransa baada ya kuua wanafunzi waliokua wanaandamana. Alifungia wanafunzi 30 kwenye jela ya mtu mmoja.

Walipompindua kwenye friji yake walikuta nyama za watu.

Mwishoni mwa maisha yake alitumia kusoma bible na huku akiwa anajiita mtume wa yesu. Hatimae alifariki mnamo mwaka 1996 kutokana na ugonjwa wa moyo.
 
Alifungwa
Huyu aliletwa na wafaransa wenyewe Afrika kumpindua ndugu yake awe kibaraka wao.
Alikuwa na cheo kikubwa tu jeshini Ufaransa alipoenda Africa kupindua.
Baada ya kuwa rais kaponda mali sana mpaka wafaransa wakaogopa na kuandaa mapinduzi mengine apinduliwe.
Ila wafaransa walimchukua na familia yake yote kuhamishiwa Ufaransa kwenye mijumba yake.
Ila sasa wakamtosa akawa analipwa pensheni tu ya jeshi alitumikia zamani.
Almas zote alizoweka huko wamhifadhie zikalambwa .
Jamaa akaona isiwe tabu kawafosi wamrudishe kwao wakamrudisha.
Akijua ataonewa huruma, wakamfunga miaka 2 kwenye kachumba kaduchu kwenye giza wakimtupia msosi tu.
Badae kaanza kuumwa wakamwachia hata hakukaa sana akafa.
 
Maisha haya ni mafupi sana usipoyafaidi yenyewe hua na tabia ya kutufaidi.....
Well done Bokasa umepitia ugumu wa uyatima kisha ukaponda raha sana, ukapiga kila papa uliyotaka then ukazeeka katika umasikini tena, ila raha na tabu za dunia umezifaidi kenge wewe kula tano [emoji109][emoji109]
[emoji12] [emoji12] [emoji12] moja kati ya post bora Kabisa,
 
Mleta mada hukumalizia kuwa alifikisi nchi mpaka ikakosa pesa ya kujiendesha. Bokassa aliomba msaada wa hela kwa Gadafi, masharti aliyopewa ilikuwa kubadili dini.
Rais alislimu Libya, alirudi nchini kwake anaitwa Mohamed Saladine Bokassa

Alirudia u Katoliki kabla mauti hayajamfika
 
Haya ni mabaki ya swimming pool inavyoonekana leo aliyojenga kwenye jumba lake kijijini alikozaliwa... imejaa maji ya mvua yameota mpaka ukurutu wa kijani kwa sababu hakuna mfanyakazi wa kusafisha hiyo swimming pool. Hivi vyeo vinapita tu jamani...

images

Source: Daily Mail Newspaper

Dah, sijui Chato international airport itakuwa hivi!!! Nawaza tu.
 
Huyu aliletwa na wafaransa wenyewe Afrika kumpindua ndugu yake awe kibaraka wao.
Alikuwa na cheo kikubwa tu jeshini Ufaransa alipoenda Africa kupindua.
Baada ya kuwa rais kaponda mali sana mpaka wafaransa wakaogopa na kuandaa mapinduzi mengine apinduliwe.
Ila wafaransa walimchukua na familia yake yote kuhamishiwa Ufaransa kwenye mijumba yake.
Ila sasa wakamtosa akawa analipwa pensheni tu ya jeshi alitumikia zamani.
Almas zote alizoweka huko wamhifadhie zikalambwa .
Jamaa akaona isiwe tabu kawafosi wamrudishe kwao wakamrudisha.
Akijua ataonewa huruma, wakamfunga miaka 2 kwenye kachumba kaduchu kwenye giza wakimtupia msosi tu.
Badae kaanza kuumwa wakamwachia hata hakukaa sana akafa.
Ni kweli alipigana WWII kama Askari wa Ufaransa lakini jamaa alikuwa katili
 
Hii inaitwa Masikini akipata........ Huku kwetu viiipi sio dalili hizi
 
Wanawake weupe hapa Afrika lazima watakuwa majasusi tu hao,kupinduliwa inakuwa kazi rahisi sana
Nalog off
 
Udikteta ni ugonjwa.....sio wa kufanyia mzaha!

Hapa bongo umeingia,inatakiwa mtu atibiwe,like,seriously!
 
Mleta mada hukumalizia kuwa alifikisi nchi mpaka ikakosa pesa ya kujiendesha. Bokassa aliomba msaada wa hela kwa Gadafi, masharti aliyopewa ilikuwa kubadili dini.
Rais alislimu Libya, alirudi nchini kwake anaitwa Ahmed Saladine Bokassa

Alirudia u Katoliki kabla mauti hayajamfika
Gadaffi shetani tu
 
Hivi kwanini wanamapinduzi wengi wa Afrika walipenda sana kujiita Field marshal?
•Na ma notorious warlords wengi walikula nyama za watu?
 
Back
Top Bottom