Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Jamani kushambulia taifa lenye nyukilia unatafuta kifo, sikio la kufa halisikii dawa, Iran amefuata njia ya Iraq enzi za Sadamu. Watu wanahisi Israel hana maandalizi na vita kwamba amekurupuka, atakuwa alishajiandaa muda mrefu sana kwa chochote kitakachotokea. Air force ya Iran bado sana ukilinganisha na Air force ya Israel, Iran anazidi Israel tu idadi ya wanajeshi, kwa upande wa technology Israel amezidi Iran kwa kila kitu, Israel ana ndege za kisasa , Iran ana ndege za zamani. Alichonacho USA Israel anacho.
Unapozungumzia nyuklia maana yake unaongelea silaha inayopaswa kumilikiwa na watu wenye uvumilivu na uwezo mkubwa sana wa vita na inatumika tu pale unapokuwa attacked na nyuklia powere mwenzio.
Kitendo cha kuachia Nyuklia dhidi ya Iran tutaitaka either ni ukurupukaji,uoga au ni kuzidiwa, maana unamiliki Nyuklia halafu unauza wenzio wasiwe nayo halafu ukiguswa unatishia kupiga nuke, hii ni dalili ya uoga.
USA angeachia wengine nao wamiliki nuke na sio kuwekeza watu vikwazo kumiliki nuke halafu unatishia kuwapiga wenzako nuke, Inachekesha Sana, tuweke usawa na kuacha kubase upande mmoja ili wote wamiliki silaha hata siku wakichapana kunakuwa na balance of power, sasa haiwezekani umuwekee mtu vikwazo since 1979 halafu leo tena unaanza kupigana naye vita, balance of power iko wapi hapo.
Wangemuacha naye Iran awe free kununua silaha atakako, kununua technolojia atakako, kumiliki atakacho ili naye aweze kulinda mipaka na watu wake.