#COVID19 THE GUARDIAN: Madaktari Tanzania hawaruhusiwi kupima COVID-19 wala hata kutamka mgonjwa ana COVID-19

#COVID19 THE GUARDIAN: Madaktari Tanzania hawaruhusiwi kupima COVID-19 wala hata kutamka mgonjwa ana COVID-19

Habari yenyewe ni utopolo tu sisi watz tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida angalia hapa chini tulipokuwa kwenye Kilimarathon jana. Kwa TZ mmeshakwama na propaganda zenu uchwara!

View attachment 1714692
Hata kwenye campeni uchaguz mkuu u lopita tulijazana hivyohivyo kusikiliza sera.Ulisikia Nan anakosoa? Walidhan watapata nchi,ila hii wanaikosoa Eti itasambaza Corona. Kwan CORONA ndio janga pekee lililowahi kuikumba dunia na Tanzania?Majanga yalikuwepo ,waliokufa walikufa na waliobaki walibaki wakatuzaa na Leo tupo sisi. Wait tuchukue tahadhari huku tukipiga kazi.
 
) Rais Magufuli ameeleza kuwa covid 19 itaondoka kwa sala
Unatakiwa kuwa roho ngumu kusema hili, tukumbuke kuwa;
1.Mungu alitupa akili za kupambana na changamoto ktk maisha yetu.
2. Hata hao waliosomea haya maandiko wanatuasa tuweke kwanza 'milango ktk nyumba zetu' kisha ndio tumuombe Mungu.
3. Kwa namna ambavyo wanasiasa 'wametupoteza' tuendelee kushuhudia maangamizi makubwa ktk nchii kwa uzembe wa wachache.
 
Kwetu hatuna Corona tuna "Nimonia", dalili zake zinafanana na inaua kweli, wazungu wanashindwa tu kutuelewa.
 
Silver lining ya kipindi hiki ni jinsi kilivyodhihirisha uwezo wa kifikra wa wananchi.

Nadhani hakutakuwa tena na mjadala wa kujiuliza wastani wa uwezo wa akili hapa nchini.
 
Unatakiwa kuwa roho ngumu kusema hili, tukumbuke kuwa;
1.Mungu alitupa akili za kupambana na changamoto ktk maisha yetu.
2. Hata hao waliosomea haya maandiko wanatuasa tuweke kwanza 'milango ktk nyumba zetu' kisha ndio tumuombe Mungu.
3. Kwa namna ambavyo wanasiasa 'wametupoteza' tuendelee kushuhudia maangamizi makubwa ktk nchii kwa uzembe wa wachache.
Maombi bila sayansi ni ushirikina!
 
Huyo Mungu mwenyewe mpaka keo hakuna aliyeweza kuthibitisha kwamba yupo kweli.

Ni hadithi tu tunapigiana.
 
Silver lining ya kipindi hiki ni jinsi kilivyodhihirisha uwezo wa kifikra wa wananchi.

Nadhani hakutakuwa tena na mjadala wa kujiuliza wastani wa uwezo wa akili hapa nchini.
Sasa sijui una maana gani hapa mkuu; lakini kama nilivyokuelewa, sidhani kama kuna 'silverlining' ya aina yoyote kutokana na yanayotokea sasa hivi hapa nchini..
Huwezi kamwe kuweka hitimisho lolote juu ya "uwezo wa kifikra wa waTanzania" kwa haya yanayotokea. Ni hitimisho ambalo sio sahihi, kwa sababu "fikra za wananchi" wa Tanzania hazijionyeshi kwa njia yoyote juu ya jambo hili. Unajua wananchi fikra zao huko vijijini na kwingineko zilivyo kwa sasa; umetumia njia gani kuzipima?

Linaloonekana dhahiri kwa sasa ni ukosefu wa busara wa watu waliojiweka madarakani kwa hila na nguvu za bunduki; na kutumia kila aina za mbinu kuwakandamiza na kuwahadaa wananchi. Hizi sio "fikra za wananchi."

Usiwalaumu wananchi. Hawa ni "MATEKA" tu kama wengine woote walivyotekwa na mtu mmoja aliyejua jinsi ya kutumia dola aliyokabidhiwa ili aitumie kuwatumikia wananchi, lakini yeye kaibadili na kuifanya kiwe chombo cha kuwateka wananchi hao.
 
Magu ni hatari sio Kwa TANZANIA pekeyake Bali Kwa dunia nzima
Anataka aitimize ile ahadi yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kuzalisha new varient za corona virus

Kama nawaona watanzania wakienda kuchezea real life ban sio hizi ban za akina melo
 
Sasa sijui una maana gani hapa mkuu; lakini kama nilivyokuelewa, sidhani kama kuna 'silverlining' ya aina yoyote kutokana na yanayotokea sasa hivi hapa nchini...
Nimekuelewa mkuu.

Nilimaanisha hawa puppets ambao hawafaidiki na chochote, yet wako tayari kurusha hata matusi kwa wananchi wenzao; kwa ajili kumuabudu binadamu.
 
Back
Top Bottom