#COVID19 THE GUARDIAN: Madaktari Tanzania hawaruhusiwi kupima COVID-19 wala hata kutamka mgonjwa ana COVID-19

Wataalam wa afya Duniani, wana hofu kuwa Tanzania kitakuwa ni kiwanda cha kuzalisha maambukizi ya Covid 19 variant.
 
Yaani magufuli ana dhambi isioelezeka. Kutotambua uwepo wa ugonjwa wakati watu wanakufa na wanapata huu ugonjwa ni dhambi na uuaji wa halaiki
 
Tofauti na nchi zingine, Tz tuna rais jiwe kweli kweli. Hadi Kagme ni soft tissue tu
 
Hii maana yake, tuache kuchukua tahadhari ya magonjwa sababu MUNGU Yupo. Hebu Rais asimjaribu MUNGU.
 
Tuanze na wewe una ndugu yakokafa?
 
Tatizo letu hatuna serikali bali kuna mtu mmoja anayeamua kila kitu. Akisema covid haipo wote wanatakiwa kuimba na kumtukuza nk
 
Wataalam wa afya Duniani, wana hofu kuwa Tanzania kitakuwa ni kiwanda cha kuzalisha maambukizi ya Covid 19 variant.
COVID-19 inaweza kumletea mTanzania ukombozi; hata kama ukombozi huo utatokana na upotevu na gharama kubwa ya maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia?

Hili ni swali.
 
Silver lining ya kipindi hiki ni jinsi kilivyodhihirisha uwezo wa kifikra wa wananchi.

Nadhani hakutakuwa tena na mjadala wa kujiuliza wastani wa uwezo wa akili hapa nchini.
Huu uzi namna ''umevamiwa'' na watu wanaojielewa. Wewe ni mtu wa tatu kwenye hii thread ku-comment ukweli mtupu lakini ulio mchungu kwa nchi yetu
 
Mkuu kuna member mmoja post zilizotangulia amekuja na ule msemo usemao ''Every nation gets the government it deserves.''. Huu ni ukweli mchungu. Unajua nchi inapochukuliwa ''mateka'' kama ulivyosema na wananchi wakashindwa kujikomboa kutoka kwenye hayo mateka basi wamekuwa wamehalalisha kutekwa kwao. Tukubali tukatae yanayotokea Tanzania, wananchi hatuwezi kukwepa lawama. Kwanza sisi wananchi ndiyo tunachukuwa ''share'' kubwa ya lawama.
 
Nakubaliana na wewe ka asilimia zote.
Aaaaah!.

Mkuu 'macho', sikubaliani nawe na huyo jamaa. Tokea mwanzo nilitaka kumkatalia nikaona nipite tu kimya kimya.

Kukuona nawe unaungana naye kwenye mawazo potofu ya namna hii kumenilazimu niweke haya niliyoweka.

Kwamba, "A country deserves a ruler that it gets"? - kwa vipi! Hiyo 'country' kama imevamiwa je; imempata 'ruler' kwa njia ambazo wananchi hawakushiriki, au walilazimishwa; bado tuwalaumu kuwa 'wanastahili kumpata huyo mtawala hata kama hawana njia za kuzuia utawala wake?

"Who rules the country is a reflection of the kind of people he rules"?

Wakati waTanzania walipokuwa na Kikwete, wali-'reflect' haiba ya Kikwete? Mkapa, Ruksa?

Mbona wote hawa ni watu wenye haiba tofauti tofauti sana; hawa waTanzania wanabadilika kila mara?

Hivi inawezekana kusema waTanzania waliokuwa na Mwalimu Nyerere, ndio hawa hawa wanao-'reflect' kiongozi wa sasa?

In short, nakataa moja kwa moja dhana hii potofu inayorahisisha na kufikia hitimisho lisilokuwa na msingi wowote.
 
Mmmh, tusihitimishe mara moja hii.

Elewa kwamba watu bado wamegawanywa kwenye makundi. Aliyewateka kaja na mbinu na propaganda zake za kulaghai baadhi yao.

Mtekaji kafanya kila juhudi kudhoofisha viongozi wale wachache ambao ndiko mzizi wa mfukuto wa kukataa 'utekaji' kungeanzia. Hakuna kiongozi wa kusimamia watu wajiondoe kwenye umateka.

Lakini kama ilivyo kwa ukandamizaji wote, mbinu zote hizi haziwezi kudumu kabla ya wananchi kujua ukweli ulivyo. Taratibu, watu wameanza kuona hadaa zinazotumika kuwakandamiza, na watazikataa.
Vuta subira.
 
Saa zingine unaweza ukafikiria mpaka ukachoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…