The Guardian (UK)- UAE owns 8% of Tanzania’s forest

Salute mingi sana Mkuu....
 
Cha mjinga huliwa na mwenye akili

Halafu eti tuna usalama wa Taifa. Usalama wa Taifa gani unaweza kukubali 10% ya nchi iwe chini ya umiliki wa mgeni mmoja?

Useless na Hopeless Intelligence Community.
Nadhani wao wameshajiridhisha kwamba mkataba una manufaa kwa Nchi !!
Sisi mihemko yetu ni kwa Dili limefanywa na wa kutoka Kwa Dipiwedi tena 😅😅🙏🙏
 
Carbon Tanzania ni madalali wawili waingereza waswahili....wajanja wa janja sana....wanapiga % kubwa ya mauzo ya Carbon huko kwenye vijiji....Kiteto...mbulu yaeda chini na Mpanda Mwese...
Hili soko kifupi lina utapeli tapeli na rushwa haswa kwa Madalali na wachaje hapo juu...
Msitu ni mali ya kijiji ana kuja mtu anakwaambia nina kampuni ..kumbe ni dalali wa kupokea fedha za makampuni kama Total kwenda kwa wananchi wanakijiji....fedha hizo hupitia akaunti yake then huzitowa kidogo kwa vijiji na Serikali....sasa hivi biashara hii IMEVAMIWA NA WANYONYAJI
 
Mkuu ila bora Dunia imeanza kulimulika hilo.....

Carbon markets ...kuna wizi wenye mlolongo kati ya madalali(Makampuni) Wahakiki na Wanunuzi...
Wenyewe wapo huko majuu kwenye Dunia ya kwanza wanatuzoom tu !!
Wamewapa madalali wao Green light wakafanye mikataba hiyo !
Na hakuna mtu wa kupinga !
Si umeona hata huo mkutano wa kimataifa wa Mazingira unafanyika UAE 🇦🇪 !!
Na Mkuu wa Dunia yake Kingi Charles III yupo mkutanoni ! 🙏
 
Inauma nini? Mbona kina tundulissu na cousins wa mbowe (USA dual hidden passorts) wanamiliki 90% ya makanikia yote?
 
Hivi hamjasikia kuwa Mwarabu kaamua kuwatoa Wafugaji kwenye Mapori yake? oparesheni kabambe inakuja Mwafrika hana chake tena.

Ni mwendo wa Masultani kurudisha Tawala zao kwa kuwahonga hawa Wajinga (CCM)👎
 
Nilisha sema waisiharamu wasipewe uongozi kwa kuwa hawana akili yoyote kichwani ni wapumbavu haswa ...watu wakaniona mjinga
 
Kwa haya ya ufisadi mkubwa anaoufanya, kwa kweli ni wa hovyo kuliko mwingine yeyote. Huyu ni laana kubwa kwa nchi.
Anafuata taratibu za kisheria na ndio maana anakawia kutumbua mifisadi,tukitaka kwenda kwa haraka tunavyotaka,tushawishi watunga Sheria wabadili Sheria ili kuyabana mafisadi vilivyo,tuache kulaumu watu wasiohusika.
 
uwekezaji wowote Kama una faida ni jambo jema na faida zionekane unless otherwise
 
Mbaya zaidi yeye ana-own hio land kwa kuwapa peanuts (alafu anafanya deals na makampuni tofauti ku-offset carbon anapata faranga maradufu) which begs a question kwanini sisi kama UMMA tusingefanya hizo deals wenyewe na kupata faida na kuwafidia hao ambao huenda tutawakataza kutumia / kukata hizo sehemu...

Ndio hapo unajiuliza huu ni ukosefu wa fikra; ubinafsi; umimi au shortsightedness ya kupewa vijisenti leo na kuuza mtaji mzima (killing the goose which lays the golden eggs)
 
Lawama ziende kwa usalama wa taifa.
 
Hawamiliki Ardhi Bali biashara ya hewa ukaa Kupitia uoto wa Juu ya Ardhi wenye Ukubwa wa hiyo 8%

Hata hivyo inatakiwa kubainishwa wazi, uwekezaji huu unainufaishaje Tanzania ikizingatiwa Iko hivyo na Nchi zingine za Afrika.

Mwisho Kuna mradi huu hapa pia kutoka Tanapa👇

View: https://twitter.com/TheCitizenTz/status/1730254134601806014?t=dvTfBqZSQIJTzkEY8VU4Iw&s=19
 
Da Mie bado nipo nyuma sana Hivi mmeshafika Mwaka 2023 na mna Rais Mwingine!!
Aisee bado nipo 2021 na Sijajua Mwaka huu Utaisha lini maana kwangu bado Mzito na mrefu
 
eti Carbon deal, hahahahaha.

wenzenu wanafanya production kwa kukata miti yote na kugeuza maeneo viwanda, na projects mbalimbali zinazowapa return faster na faida kubwa, then wanakuja kuwawekea sheria za kulinda mazingira na kuwadanganya na vihela.

Hii ilipaswa kuwa silaha yetu pia, vijana wetu majasusi na wataalam wakae chini na kufanya hesabu makini ili tulipwe mahela mengi yatakayofidia gap kubwa la budget yetu kila mwaka na kuacha kukopakopa.
 
Urusi iko vitani na Ukrain, wanapigania Ardhi.
Israel iko katika vita na Palestina. Wanapigania Ardhi.
Mataifa huko duniani miaka nenda rudi, tangu zama za kale za mawe, watu walikwenda vitani kupigania Ardhi. Sio kwamba hawajui kwamba watakufa waiache hiyo ardhi, la, wanajiuliza ikiwa wao watalegalega, wajukuu zao na wana wa vitukuu vyao wataishi je?

Wenzetu wanaamini wakifa watalala vizuri ikiwa walio waacha nyuma watakuwa na maisha mazuri, sisi tunaamini tukifa kunapahala panaitwa peponi. Tutakwenda. F*ck whoever remains behind. Atapambana kivyake. Ila wakati wetu tunautumia kujaza matumbo yetu. Ndio maana viongozi wetu hawajali kuhusu Ardhi yetu. Wanagawa tu. Wakishastaafu wataandika vitabu kujutia uamuzi waliofanya then akilini mwao wanaamini wametubu, wako tayari kwenda peponi.

Kesho ya vizazi vyetu itakuwa ngumu kuliko tunavyodhani. Na hiyo dhambi tutaibeba mabegani mwetu.
 
Jiongeze....

Huruhusiwi kukata miti ndani ya eneo la mradi

Huruhusiwi Kulima

Mifugo marufuku

Mkataba 40 years

Makubaliano SIRI ..NO transparency

Indirect the land is owned by the PROJECT Investor's
 
Jiongeze....

Huruhusiwi kukata miti ndani ya eneo la mradi

Huruhusiwi Kulima

Mifugo marufuku

Mkataba 40 years

Makubaliano SIRI ..NO transparency

Indirect the land is owned by the PROJECT Investor's
Ukate mti kwenye maeneo yaliyohigashiwa Ili iwaje? Kwa saizi unaruhusiwa kukata mtu? Acha ujinga.

Swala la msingi Tanzania tunanufaikaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…