The Guardian: Wamasai kufukuzwa kupisha Mwarabu (UAE) kuwinda Wanyama!

Tembo wa mwisho mwisho sasa ndio wamebaki.

Acha nifungue Zoo tu sasa maana watabaki kwenye picha tu.

Sasa kama ni hivyo watabeba mpaka watoto wa Tembo hawatasubiri wakue kwenye maisha ya kuwindwa

Ila waswahili wapole sana.

Mtawaangalia wakidunda na kuwanyanyasa kwenye ardhi yenu na hamfanyi kitu.

Maskini
 
Hilo nalo NENO!
 
labda mnieleweshe....kuna maeneo watu wameondolewa inachimbwa dhahabu na watu wamepata ajira na huku serikali ikiingiza mapato na miji imekua.... mfano pale Geita, Kahama, Bulyanhulu nk....
Una tatizo kichwani wewe, yaani kufukuza wamasai na kuleta waarabu wafanye ujangili unalinganisha na watu kuondolewa ili wachimbe dhahabu?, Watengeneze umeme?

Shida kweli haya kama hivyo ni sawa basi waondoeni tuu maana mna hoja ya kuwafukuza kwa kufananisha na miradi mingine.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Haya waliokuwa wanasema kufukuzwa kwa Wamasai ni kwa ajili ya kutunza Hifadhi wako wapi? Kwa mujibu wa Gazeti la Mzungu wenu The Guardian sababu ya kuwaondoa Wamasai kwa nguvu ni kupisha Mwarabu wa Dubai kuwinda Wanyama...
Wataanz kusafirisha tena wanyama hai inaumiza sna kuwafukuz masai tunaamini tukipata katiba mpya haki ya wamasai itakuj patikana
 
labda mnieleweshe....kuna maeneo watu wameondolewa inachimbwa dhahabu na watu wamepata ajira na huku serikali ikiingiza mapato na miji imekua.... mfano pale Geita, Kahama, Bulyanhulu nk...
baada ya futuru tuonane shekh nina pakti yako ya Tende
 

Swali ni kwamba kwa nini Serikali wanadanganya ? Kwa nini hawasemi sababu za kuwaondoa ni kupisha Mwarabu kuwinda ? Kama jambo ni jema kwa nini lifichwe?
 

kwa hiyo mkuu pale Serengeti, Selou, Mikumi nako watu wahamie maana waliowekeza kwa maana ya kuwinda na utalii ni majangiri..?.

Ujangiri kwa fikra zangu ni kuvai na kuua wanyama bila kibali na kuchukua nyara kama pembe, ngozi, meno nk.... lakini kinachofanyika kwa uelewa wangu ni uwekezaji na kulinda ecology ambavyo havina tofauti na uwekezaji mwingine kama kuchimba dhahabu nk...
 
Wamasai wameishi pale zaidi ya miaka elfu kumi, laki moja. Wanajua kuishi na wanyama wa asili.

Kuwafukuza leo tunakosea sana.
 
Ikiwa lengo ni hilo serikali inapaswa kuweka tu wazi, kuwa wanawaondoa ili kuwapa hao
 
utaweza kufanya hivi vitu Uarabuni, ulaya?
 
Mbali na katiba tuelewe tunawaita viongozi asilimia kubwa Ni Wezi tu
 
Unaamini habari za wazungu kuliko Serikali yako.
 
Tukiingiza siasa kwenye mambo ya msingi hatufiki popote.

Uwindaji kwenye mbuga zetu ni biashara ambayo inatupa forex zakutosha tu. suala la kuhamisha shughuli za kibidamu kutunza mbuga tukafanya biashara ya uwindaji tatizo liko wapi?

Angalia hawa wanalia waruhusiwe kufanya kilimo waendelee kuharibu uoto wa asili, kumbuka ukimruhusu kufanya kilimo eneo la acre moja leo, baada ya Miaka kumi ataongeza eneo maradufu.

Kama Serikali imewaandalia makazi mbadala sioni tatizo.

Dunia imebadilika. hatuwezi kuishi kama wanyama tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…