labda mnieleweshe....kuna maeneo watu wameondolewa inachimbwa dhahabu na watu wamepata ajira na huku serikali ikiingiza mapato na miji imekua.... mfano pale Geita, Kahama, Bulyanhulu nk..
Kule Mtwara msimbati na all the way to Dar es salaam, watu wamelipwa na kuhamishwa ili Bomba la gas lipite na limepita leo hii watu wanatumia gas.
Pale stieggler miti na msitu vimekatwa na wanakijiji kadhaa pals rufiji wamehama ili bwawa lijengwe umeme upatikane..
Barabara ya Morogoro ilikuwaga kichochoro miaka ya 90's, watu wapembezoni wakahama na familia zao kwa kulipwa na kuhamia kwingine na leo hii tunaenjoy barabara woote..
Pale Ubungo kimara majumba na maelfu walihamishwa kupisha ujenzi wa njia sita na makelele yoote wapi ...majumba yakaangushwa leo tunaona barabara....
Labda mnieleweshe, kipi ambacho ni special kwa wamasai kuendelea kubaki serengeti na shughuli nyingine zikaachwa ili wao waishi serengeti? tukumbuke pia sheria yetu inasema ardhi ni mali ya Serikali na wakati wowote wakiihitaki kuinadilishia matumizi wanachukua.