Mkuu,
Hebu rudi kwenye hoja
Nadhani wewe na timu yako mngeeleweka sana kama mngetolea maelezo hivyo vifo hapo juu,uzuri Nic ameweka na video hapo na ukiangalia hizo video utaona kuna mambo ya kustua
Kama umeamua kuchagua kubisha bila kusema ni kwanini unabisha na kwa ushahidi gani nitakuelewa!
Mkuu
Eiyer, sidhani kama ni sahihi kwamba kinapotokea kifo cha kutisha au kushtua tunatakiwa kuhusianisha na mambo yasiyokuwa ya kawaida kama hayo ya freemason na illuminati.
Kwenye maelezo yako yale mengi nimeyapenda, yanavitu ambavyo vinafikirisha kwa kweli, binafsi ninaamini ni coincidence tu,
Hii dunia mkuu ina watu wengi wengi akili nyingi mno, wanaweza wakakuunganishia matukio hadi ukaona ni ukweli,
Lakini mwanafalsafa wa kale Aristotle, anaueleza ukweli kwa namuna tofauti, Yeye anasema ukweli ukichanganya na uongo, unapata uongo, na pia uongo ukichanganya na ukweli, unapata uongo vilevile, hii haijalishi hata kama uongo ni kidogo na ukweli ni mwingi, ukichanganya tu, unapata uwongo. ni sawa na sumu uchanganye na chakula, unapata sumu.
Inawezekana ni kweli kuna hivi vitu vinavyoitwa freemason au illuminati, lakini vimetiwa chumvi na kupambiwa uongo mwingi kiasi kwamba habari nzima ishakuwa uwongo.
Aristotle anaendelea kuelezea ukweli, kwa kimombo anasema Truth is agreement with facts and reality.
Ndio maana
Kiranga ameshangaa baada ya
Nicholas kudai kuwa familia ya Jackson walimtoa kafara Michael Jackson eti ili kupata utajiri, unaweza kuona hakuna agreement ya facts and reality hapo.
Ule mfano wako wa ile miaka mia moja mia moja, kwamba Licoln alinanii sijui miaka mia moja akaja tena Kennedy nae miaka mia moja, nayo inaweza kuwa coincidence,
Chukulia mfano, Yesu alifunga siku 40, Mvua ilinyesha kipindi kile cha safina ya Nuhu siku 40,wana wa Israel walikaa sijui jangwani miaka 40, Wanasema hata za mwizi nazo ni 40. Mtu mjanjamjanja anaweza akashawishi watu kwamba kuna ufreemason hapo na watu wakamuamini.
Labda nikuchekeshe kidogo mkuu, Mimi nimezaliwa July 6, Hii ni siku ambayo amezaliwa Rais George W. Bush pamoja na mwanamziki 50 cent, mbele ya safari, kwa sababu tu ya coincidence ya tarehe ya kuzaliwa naweza kuambiwa mimi ni freemason.
Kuna mwingine nilimkuta amejaza watu akiwahubiria habari ya freemason, nilimsikia akisema kuwa hata shirika la fedha la kimataifa IMF eti nalo ni freemason, Uthibitisho anaoutoa ni kwamba ukigeza herufi IMF unapata FMI, eti FreeMason International.
Kwa hiyo mkuu kwangu mimi story hizi ni abraakabra.