The Illuminati is real, and it's everywhere

Inaonekana wewe hujui kitu hapa!!!

kwahiyo wewe unayejua kitu umenufaika na nini ? porojo tupu , eti unasema fulani ni illuminant kisa aliwahi kufiwa na ndugu yake ?!!
nami nauliza nani hajawahi kufiwa ?
 
Mkuu Eiyer, sidhani kama ni sahihi kwamba kinapotokea kifo cha kutisha au kushtua tunatakiwa kuhusianisha na mambo yasiyokuwa ya kawaida kama hayo ya freemason na illuminati.

Kwenye maelezo yako yale mengi nimeyapenda, yanavitu ambavyo vinafikirisha kwa kweli, binafsi ninaamini ni coincidence tu,

Hii dunia mkuu ina watu wengi wengi akili nyingi mno, wanaweza wakakuunganishia matukio hadi ukaona ni ukweli,

Lakini mwanafalsafa wa kale Aristotle, anaueleza ukweli kwa namuna tofauti, Yeye anasema ukweli ukichanganya na uongo, unapata uongo, na pia uongo ukichanganya na ukweli, unapata uongo vilevile, hii haijalishi hata kama uongo ni kidogo na ukweli ni mwingi, ukichanganya tu, unapata uwongo. ni sawa na sumu uchanganye na chakula, unapata sumu.

Inawezekana ni kweli kuna hivi vitu vinavyoitwa freemason au illuminati, lakini vimetiwa chumvi na kupambiwa uongo mwingi kiasi kwamba habari nzima ishakuwa uwongo.

Aristotle anaendelea kuelezea ukweli, kwa kimombo anasema Truth is agreement with facts and reality.

Ndio maana Kiranga ameshangaa baada ya Nicholas kudai kuwa familia ya Jackson walimtoa kafara Michael Jackson eti ili kupata utajiri, unaweza kuona hakuna agreement ya facts and reality hapo.

Ule mfano wako wa ile miaka mia moja mia moja, kwamba Licoln alinanii sijui miaka mia moja akaja tena Kennedy nae miaka mia moja, nayo inaweza kuwa coincidence,

Chukulia mfano, Yesu alifunga siku 40, Mvua ilinyesha kipindi kile cha safina ya Nuhu siku 40,wana wa Israel walikaa sijui jangwani miaka 40, Wanasema hata za mwizi nazo ni 40. Mtu mjanjamjanja anaweza akashawishi watu kwamba kuna ufreemason hapo na watu wakamuamini.

Labda nikuchekeshe kidogo mkuu, Mimi nimezaliwa July 6, Hii ni siku ambayo amezaliwa Rais George W. Bush pamoja na mwanamziki 50 cent, mbele ya safari, kwa sababu tu ya coincidence ya tarehe ya kuzaliwa naweza kuambiwa mimi ni freemason.

Kuna mwingine nilimkuta amejaza watu akiwahubiria habari ya freemason, nilimsikia akisema kuwa hata shirika la fedha la kimataifa IMF eti nalo ni freemason, Uthibitisho anaoutoa ni kwamba ukigeza herufi IMF unapata FMI, eti FreeMason International.

Kwa hiyo mkuu kwangu mimi story hizi ni abraakabra.
 
..hawana hofu ya Mwenyezi Mungu hawa!!!inasikitisha sana aisee!!!
 
..hawana hofu ya Mwenyezi Mungu hawa!!!inasikitisha sana aisee!!!

Sidhani km hata wanaihtaji hofu yake..si unajua kwao wanamwona km tunavyomuona mungu kuwa ni Shetani....ni km kusema kuwa akina Ritz wamhofie Mungu waache kebehi kwa Yesu, na Wakristu.
 
Huyo #9 Suge Knight sasa hivi hata Ali Kiba kampita kwa hela maana yupo BankRupt mbaya,,,si angetajirika lakini?
 
kwahiyo wewe unayejua kitu umenufaika na nini ? porojo tupu , eti unasema fulani ni illuminant kisa aliwahi kufiwa na ndugu yake ?!!
nami nauliza nani hajawahi kufiwa ?

Unaendelea kuthibitisha namna usivyojua lolote!!!
 
Mkuu Eiyer, sidhani kama ni sahihi kwamba kinapotokea kifo cha kutisha au kushtua tunatakiwa kuhusianisha na mambo yasiyokuwa ya kawaida kama hayo ya freemason na illuminati.
Mkuu inaonekana labda hujamuelewa Nic,hajasema kuwa kila kifo cha kutisha kimehusishwa na hawa jamaa ila ni baadhi ya vifo tu!

Kwenye maelezo yako yale mengi nimeyapenda, yanavitu ambavyo vinafikirisha kwa kweli, binafsi ninaamini ni coincidence tu,
Duh!mkuu hebu fikiria upya,yaani hiyo ni bahati mbaya???????????????????????????????????????

Hii dunia mkuu ina watu wengi wengi akili nyingi mno, wanaweza wakakuunganishia matukio hadi ukaona ni ukweli,

Hilo linawezekana
Lakini sio kwenye ishu hii ya Lincoln na Kennedy
Wachaguliwe tarehe zinazofanana,wazae watoto wenye idadi sawa,madaktari wao wawe na majina sawa,marafiki zao hivyo hivyo,mahali walipouwawa hivyo hivyo,n.k???????????
Hapana hii sio bahati mbaya!!!!

Mh! hapa nakiri kutokukubaliana na Aristotle,labda nipewe maelezo ya kutosha!!!

Inawezekana ni kweli kuna hivi vitu vinavyoitwa freemason au illuminati, lakini vimetiwa chumvi na kupambiwa uongo mwingi kiasi kwamba habari nzima ishakuwa uwongo.

Hapa inaonekana sasa unaanza kupata mwanga
Endelea kutafiti tu mkuu utaujua ukweli!

Hilo la kutiwa chumvi linawezekana kuwa kweli!

Hapa labda unifafanulie ni kivipi na kwanini
Maana naona inawezekana tu na hakuna tatizo hapo!

Ule mfano wako wa ile miaka mia moja mia moja, kwamba Licoln alinanii sijui miaka mia moja akaja tena Kennedy nae miaka mia moja, nayo inaweza kuwa coincidence,
Mkuu hapa nakuomba upasome upya halafu ufikiri tena
Naona kama umelirahisisha sana jambo hili!

Inawezekana hii lakini atakaemuamini huyu ni yule asietafiti kuhusu hawa jamaa
Hawa watu wana namba zao,pia wana kanuni yao ya kufanya jambo au mambo,hivyo unatakiwa kwanza ukague kama jambo husika limefanywa kwa kanuni au laa
Kama hakuna kanuni basi hilo tukio chanzo chake kitakuwa kingine!
Halafu hayo matukio uliyotaja hapo sio bahati mbaya kumbuka yalipangwa na Mungu!

Labda nikuchekeshe kidogo mkuu, Mimi nimezaliwa July 6, Hii ni siku ambayo amezaliwa Rais George W. Bush pamoja na mwanamziki 50 cent, mbele ya safari, kwa sababu tu ya coincidence ya tarehe ya kuzaliwa naweza kuambiwa mimi ni freemason.

Hapana

Mkuu kuna kanuni ya haya mambo!

Kuna mwingine nilimkuta amejaza watu akiwahubiria habari ya freemason, nilimsikia akisema kuwa hata shirika la fedha la kimataifa IMF eti nalo ni freemason, Uthibitisho anaoutoa ni kwamba ukigeza herufi IMF unapata FMI, eti FreeMason International.

Kuna watu wana uelewa mdogo kwenye mambo haya,hivyo hawa huwadanganya watu au husema mambo ambayo hawana ushahidi wa kutosha mwisho wake huonekana vituko japokuwa huenda maelezo yao yanaweza kuwa na ukweli fulani

Kwa hiyo mkuu kwangu mimi story hizi ni abraakabra.

Kuna jamaa yangu mmoja niliwahi kumueleza uwezekano wa kuwepo hawa watu mwaka 2010
Huyu jamaa aliniangalia sana halafu hakusema kitu

Siku zilivyoenda siku moja alikuja kuniuliza kuhusu kile nilichomuambia,kabla sijamjibu nilitaka kujua kilichosababisha aje kuniuliza tena wakati siku ya kwanza namuambia hakujibu kitu na alionekana kudharau maelezo yangu

Aliniambia kuwa amekutana na utafiti kuhusiana na tetemeko la ardhi la Haiti na kuna mambo yalimshangaza kidogo na yanaonekana kufanana na kile nilichokuwa namuambia

Sasa inawezekana mkuu kwa muda huu ukawa unaona hivyo lakini ngoja muda uzungumze,sio wewe tu wapo wengi sana waliokuwa wanasema kama wewe na baadae walikuja kukutana na ukweli!
 
Upuuzi tena unarudi wa hizi habari za kufikirika. How comes wengine watoe mama zao wengine watoe marafiki?

Kila mtu amewahi kufiwa, tukianza kusema kila aliyefiwa alimtoa nduguye/rafiki marehemu kafara basi wote sisi ni illuminati

Na ku-relate tarehe za misiba au umri na illuminat ni highest level ya upuuzi
 
BTW tuko era ya magaidi sasa.. tulianza na era ya mafisadi, ikaja era ya free masons, ikaja era ya unga, sasa ni era ya magaidi. Acha kurudisha wakati nyuma
 
wakaulizwa huko mbinguni wanawake km wao wameahaidiwa nini?mimacho ikawatoka wapo,eti mungu wao anajua, wakiulizwa mbona kwa wanaume alijua na kuwaambia mabiikra 72, huku wao wakiwa hawapo ktk list....jamaa wanavisha hadi punda mabomu ...

Mkuu hii umeua kabisa!!!!!!!!!!!!
 
BTW tuko era ya magaidi sasa.. tulianza na era ya mafisadi, ikaja era ya free masons, ikaja era ya unga, sasa ni era ya magaidi. Acha kurudisha wakati nyuma

Mkuu Bufa umefanikiwa kunifanya nicheke leo .....lol!!
 
Last edited by a moderator:
Eiyer, mimi siamini katika vinavyoelezwa kuhusu uwepo wa Freemason(huwa napenda kutamka filiimasoni)lakini napenda kujifunza.
Kama kuna mtu anaushahidi mwingine tofauti na ule wa vifo na utajiri atupatie. Wengine wanasema kusali jumapili ni mpango wa freemason ili kuelekea New World Order na kwamba itafika kipindi watu wote ulimwenguni watalazimishwa kusali jumapili, hawa ndio wanaodai eti Marekani, Papa na United Nations ni filiimasoni.
Wapo wanaosema wanasiasa na watu wengi sana maarufu, hasa wa Marekani na Israel ndio ukoo wa filiimasoni, Nicholas​, upi ni ukweli na ni upi upi ni uwongo hapo?
 
hizo tarehe za vifo zinanitatiza kidogo,inaonekana wanataka ziwe na jibu kama wanavyotaka ili kupata masonic namba.hebu chunguzeni vizuri jinsi zinavyojumlishwa.
 
Mimi ninavyojua kuchanganya kwa habari ni kutokujua na kutokuamini kuna msemo unasema " nyoka yupo morogoro!!! na Ajeeeeee,,,,nyoka yupo kibaha jamaniiiiiii!!!! ,,, na ajeeee,,, nyoka yupo ubungooooo,,,, na ajeeeee,,, @ na nikweli yule nyoka ika na kuwameza watu wote ambao hawakuhami ambao hawakuchukua tahadhali ya ujio wa nyoka, hapa ninataka kusema nini? ni kwamba haya mambo ya freemason na ushetani yapo na yanafanya kazi muhimu ni kuwa mwangalifu sikushauri kujiunga au kushabikia ukifanya hivyo ni kujiunga na upande wa pili wa setani na mabalaa yatakupata.

ebu pitia kwenye link hii Jicheki | Jicheki na uwe tayari kuja kwa mkombozi uone jinsi Jay-z alivyowaambukiza watoto na vijana wetu ufreemason na ushetani katika miziki yake.

Asante.

Kila aliye na sikio, asikie..................
 
Tatizo lingine ni hapari ppotofu zilziopo kwa watu mitaani na hata wasomi wetu walivyo hovyo ktk kutoa maelezo ya vitu.Hapa nchini mtanzania ana hakika ya asilimia zaidi ya 98 ,ya kupat amajibu ya hovyo toka msomi anayefuatia,huku mosmi huyo akiwa na ujasiri w ahali ya juu.
 
Illuminati ipo ila sio ikufanye uone kila msanii na mwenye hela ni illuminast, wewe hizo data hapo juu ulizocopy na kupaste hazina ukweli wowote, kila mkubwa akifa wewe unaona imetolewa sadaka, kijana naona conspiracy theories zinakukaba sana kichwa, sio kila unachosoma kwenye internet ni real, vipo ambavyo ni kweli na vipo ambavyo watu wamehisi tu, kwani mimi nikisikia sehemu unadhani ntashindwa kwenda kuandika article kwenye site yoyote? watu watacopy mwisho wa siku itasambaa kila kona.. Hiyo list wapo Illuminast na wapo ambao mmewaweka tu kwa kuhisi kwa kua walifiwa na fulani hapo mwanzo. Hahaha afu mlivo wa ajabu kila kitu mnatafuta relationship ya namba 9, kazi ndogo sana hiyo kukamata akili za watu kama nyie
 
Nitafutie majibu ya yale matukio niliyokuwekea kwanza

Isije kuwa hutaki tu kuamini kwasababu ya hofu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…