"The Iron Dome" Kama Taifa tunajifunza nini kwenye Teknolojia hii ya Israel?

"The Iron Dome" Kama Taifa tunajifunza nini kwenye Teknolojia hii ya Israel?

Haujambo Mwana Jamvi, Heri na hongera sana kwa sikukuu ya Eid-Al-fitr. Kwa niaba yangu binafsi nakutakia sherehe njema, ikawe heri na amani kwa upande wako. Eid Mubarak!!!!

Mwaka 2006 viliibuka vita kati ya Israel na Lebanon. Lebanon ( Hezborah) ilivurumisha maelfu ya makombora katika anga ya Israel. Mwaka uliofuata Israel iliutangazia Ulimwengu kwamba chombo chake cha kujilinda "RAFAEL ADVANCED DEFENCE SYSTEM" kwa kushirikiana na Taasisi ya Technologia ya anga ya Israel (Israel Aerospace Industries) ziko mbioni kuvumbua na kutengeneza technologia mpya na ya uhakika ya kukabiliana na uvamizi wa anga kwa kutumia makombora ya masafa mafupi na kati, helcopter na zana nyinginezo za kivita.


Mwaka 2011, Israel ilikamilisha uvumbuzi wake na kutambulisha mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora ya masafa mafupi uitwao "The Iron Dome".

The Irone Dome ni mfumo wa kisasa wa kujilinda kutokea ardhini kwenda angani dhidi ya makombora ya masafa mafupi mpaka kilometer 70. Mfumo huu unatumia msaada wa radar na makombora ya Tamir Interceptors ambayo yanafuatilia na ku-neutalize makombora kutoka upande wa adui katika anga linalo-lindwa. Mfumo huu unazuia Makombora, silaha za kivita za C-RAM, ndege, helecopter na ndege zisizo na rubani.

Ufanisi wa mfumo huu unakadiriwa kuwa ailimia 90, na ina uwezo wa kuzua makombora kutoka pande tofauti tofauti kwa wakati mmoja. Kwa lugha nyepesi ni kuwa, Israel inaweza kuzuia Makombora kutoka Lebanon, Misri, Jordan, Syria na Hamas(Palestina) kwa wakati mmoja.

Gharama ya Kombora moja ni mpaka dola elfu 40 za kimarekani ( Sawa na TZS 92,000,000) na betri ya system moja ni sawa na billion 115 za kitanzania.

Ndani ya juma hili, kumekuwa na mvutano mkubwa sana kati ya Israel na Palestina(Hamas). Huku kila upande ukitupa lawama kwa mwenzake kuwa chanzo cha ugomvi huu. Hamas mpaka sasa wamerusha zaidi ya makombora 1000 na kati ya hayo ni moja tu ndiyo limeweza kufika ardhini. Bila shaka hayo mengine yamekuwa neutralized na mfumo thabiti wa "The Iron Dome".

Kama taifa, Israel wamewekeza sana kwenye technologia ya ulinzi wa kisasa. Na wanafanya biashara kubwa sana na mataifa makubwa ikiwemo Marekani na Uingereza hasa kwenye Technologia ya Ulinzi. Kwa sasa hakuna nchi duniani yenye uwezo na uvumbuzi mzuri kama taifa hili dogo mashariki ya kati. Wamejipambanunua katika taaluma hii, na hakika wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa sasa hakuna nchi ya Kiarabu yoyote inayotaka vita na hawa jamaa. Palestina anashambuliwa na kuuliwa kama kuku huku majirani zao wametoa macho. Nadhani hawapendi kiwakute kilichotokea 1967 (A six day War) ambapo Israel iliwachapa waarabu ndani ya siku sita tu na kunyakua sehemu kubwa ya ardhi yao.


Kama taifa TEULE la Tanzania. Tunajifunza nini kutoka kwa hawa wenzetu wa Israel? Kuna lolote tunaloweza kujivunia nalo zaidi ya umbea na ushambenga kwenye mitandao ya kijamii ya wazungu na wachina? Je, tuko tayari kuendelea kuletewa kila kitu bila kufanya mapinduzi ya kitaaluma na kiviwanda? Hakika tunalo la kujifunza na kuchukua hatua kutoka kwa hawa wenzetu.
Kabla ya kuulizia nchi wewe kwanza jiulize umeifanyia/ unaifanyia nini Tanzania?

Hivi kuna mtu nweusi anaweza kugeuza mchanga/ udongo kuwa mashine?
 
Na hata Mimi mkuu zitto junior, sikatai kuhusu hiki, Ila wale jamaa wananguvu nyingine isiyoonekana, ingawa nguvu hiyo pia iko kila mahali, Lakini Mungu mwenyewe alishaga apa hivyo kuwalinda na kuwapiga maadui zao

Jifunze Kwa Daud na Goliati ndio utapata jibu, Umewahi kujiuliza katika jiwe alilolitupa Daud Kwa Goliath Hadi likasababisha umauti wa mwamba Goliath??

Ndani ya Hilo jiwe mlikuwa na nguvu ya ziada,

Licha ya hivyo, Biblia pia haisemi Kwamba wao Israeli watakapopigwa hawatakufa kabisa, watakufa Ila ushindi watapata
Kwahiyo Tanzania haina nguvu isyoonekana? Au Mungu anawapendelea tu wayahudi afu sie wengine anatupotezea.

Mungu mnayemuabudu kweli yupo hivyo? Kwamba wayahudi wakikutana na Goliath awalinde ila TZ tukikutana na Goliath wetu atupotezee?

Kila binadamu ana muujiza wake ambao ana ucredit kwa Mungu ila haimaanishi yeye ndio anapendwa zaidi na Mungu kuliko wengine. Sidhani kma ni sahihi
 
Muisraeli hayupo juu ya Waarabu tu bali yupo juu ya dunia yote.---- ni mahali gani ambapo kuna uchumi au maslahi haramu au halali duniani hukuti "mkono" wa Muisreali???!
USITULETEE POROJO HAPA.
UNATAKA KUNAMBIA CHINA ISRAEL YUPO?
KWA USHAWISHI GANI HASA?
 
USITULETEE POROJO HAPA.
UNATAKA KUNAMBIA CHINA ISRAEL YUPO?
KWA USHAWISHI GANI HASA?


Hivi wewe unaelewa uchumi wa dunia??--- au unataka ubishani wa vijiwe vya kahawa!!?.

Kwa mfano, Kampuni ya Huawei ni kampuni ya wapi na imefanywaje na Marekani??--- au hujui mahusiano ya kiuchumi kati ya Amerika na Israeli??!.

Huwezi kuzungumzia uchumi wa America bila kuihusisha Israeli moja kwa moja au kwa mbali.
 
Hivi wewe unaelewa uchumi wa dunia??--- au unataka ubishani wa vijiwe vya kahawa!!?.

Kwa mfano, Kampuni ya Huawei ni kampuni ya wapi na imefanywaje na Marekani??--- au hujui mahusiano ya kiuchumi kati ya Amerika na Israeli??!.

Huwezi kuzungumzia uchumi wa America bila kuihusisha Israeli moja kwa moja au kwa mbali.
hivi kauli yako umeielewa?
umesema kila sehem Israel ana mkono wake fafanua.
maana inavyofahamika aliyeiwekea vikwazo huawei ni USA japo yeye mwenyewe kaathirika na vikwazo alivyoweka.
Unataka kunambia anchofanya USA ni shauri ya Israel?
Leta ufafanuzi.
 
Palestina/Waislamu hawakuamini macho yao 😂😂😂 unapigwa mpaka unachanganyikiwa unajitangaza mshindi.
 
hivi kauli yako umeielewa?
umesema kila sehem Israel ana mkono wake fafanua.
maana inavyofahamika aliyeiwekea vikwazo huawei ni USA japo yeye mwenyewe kaathirika na vikwazo alivyoweka.
Unataka kunambia anchofanya USA ni shauri ya Israel?
Leta ufafanuzi.


Go and read, "Israel in the orbit of America; The political Economy of dependency relationship".
 
Back
Top Bottom