The Lema Verdict: Did the Court of Appeal encroach on litigation rights of a voter?

quote_icon.png
By Mzee Mwanakijiji

Hili naweza kusema jibu litakuwa ni kuwa Chama cha Siasa kina locus standi kwenye kesi ya uchaguzi........hili la Arusha Mjini Chama cha Mapinduzi hakikuwa mlalamikaji na wala hakikujiweka kama amicus curie na hivyo hatujui msimamo wake kwenye ile kesi ni nini.

Batilda Buriani alitakiwa kufungua hiyo kesi yeye mwenyewe na kama kulikuwa na kundi la wanawake ambao nao waliamini kuwa kweli Lema alisema maneno ya kuwadhalilisha basi na wao wangejiunganisha kwenye kesi hiyo. Lakini halikufanyika hilo.
Ahsante,umefafanua vema sana. Hii ndio hasa hoja niliyomaanisha katika bandiko langu la awali.
Key words, locus standi and amicus curiae.

Kwa wale wenye hoja kuwa hili ni suala la public interest na kwamba there's infringement of voters right, nina panua mjadala kidogo kwa kuuliza kwanini mbunge anayechaguliwa na wananchi (kwa public interest) anaweza kupoteza ubunge kwa kupitia chama chake na si wananchi ! Je, hapo public interest imelindwa na voters wamepewa haki kama tunaoyoona wamenyimwa na CA of Tz.

Nguruvi3 Pamoja na kumshukuru Mzee Mwanakijiji kuwa kajibu swali lakoo ukweli ni kuwa hajalijibu na majibu yake hayajazingatia uamuzi husika hakuna mahali ambapo Mahakama ya Rufaa imesema jinsi Mzee Mwanakijiji kasema! Nimefafanua awali wakati ninamjibu.

Pili huwezi kutumia mapungufu yaliyomo kwenye sheria zetu kuhalalisha wapigakura kunyang'anywa haki yao ambayo tayari kwenye katiba kama kifungu cha ibara ya 26(2).
 
Ngoja niwaambie miye ninachoona kizuri hapa - na CDM wanaweza kukitumia vizuri - ni suala la kutoandikisha wapiga kura kwa uchaguzi mdogo. Wale wanaofikisha miaka 18 au wengine ambao hawakuwemo kwenye daftari hilo tangu 2010 wanaposhindwa kupiga kura kwa sababu ya kutokuandikishwa wanaweza kufungua kesi mahakamani kwani haki yao kama wapiga kura inavunjwa.
[MENTION]
Mzee Mwanakijiji[/MENTION] Kuna faida gani ya kujiandikisha kam akura yako uliyoipiga Mahakama ya Rufaa inakuzuia kudai iheshimiwe kulingana na Ibara 26(2)? What is the use of voting anyway?
 
As it stands, sheria ya uchaguzi inaruhusu chama cha siasa kufungua kesi kama mgombea wao ameshindwa kesi?

Kifungu cha 111(1)(a) cha sheria ya uchaguzi kinasema kuwa mtu ambaye wanaweza ku-petition ni:

(a) mtu ambaye alipiga kura au alikuwa na haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi husika;

(b) mtu ambaye anadai kuwa alikuwa na haki ya kuwa-nominated au kuchaguliwa kwenye huo uchaguzi;

(c) mtu anayedai kuwa alikuwa mgombea kwenye huo uchaguzi; na

(d) Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Nakumbuka baada ya Kafumu kusema hatakata rufaa, CCM walisema watakata rufaa kama chama.

Unless kuna sheria ningine itakayowaruhusu, CCM will be facing the same problem.

HAlafu kwenye hii kesi ya Lema kama kweli kesi ilikuwa na public interest, si ingekuwa bora zaidi kama mwanasheria mkuu wa serikali angefungua kesi?

EMT Umefanya vizuri kuibandika sheria ya uchaguzi hapa. Haki ya kwanza kulalamika ni ya mpiga kura sasa kama mpigakura katupiwa virago vyake na Mahakama ya Rufaa hicho chama ambacho umauzi huu unasema kwa uwazi kabisa ni mgombea tu unafikiri uhalali wake unatoka wapi?

Kufuatana na uamuzi huu ni mgombea tu ndiye mwenye mahali pa kusimamia kisheria na ndiyo maana ninasema hii Mahakama ya Rufaa imeturudisha nyuma kwenye zoezi zima la kuendeleza utawala bora...........
 
Last edited by a moderator:
Zakumi Hizi zako ni porojo za kisiasa hazina uhusiano na mada. Mengi unayoyaongelea tayari huu uamuzi umeyakataza lakini wewe unatoa maoni jinsi unavyotaka iwe wakati Mahakama ya Rufaa maamuzi yake yatagusa kesi nyinginezo ambazo wapigakura watazipeleka mahakamani kupinga matokeo na walalamikiwa wataitumia hii hukumu kuiomba mahakama kuu kuzifuta kwa kutumia uamuzi huu na kesi hizo zitafutwa tu hakuna jinsi hadi pale Mahakama ya Rufaa itakapovadili msimamo huu ambao unawazuia wapigakura kuhoji uhalali wa matokeo ya uchaguzi kama yalizingatia sheria ya uchaguzi.

Nakubali kuwa ni porojo lakini nilikuwa namjibu EMT na yeye ametoa ufafanuzi wake mzuri. Pili ni kweli maamuzi ya mahakama ya rufaa yana-set precedent za kesi nyingi. Lakini sio kwa kesi hii.

Sababu ni hii: Hii ni kesi ya haki ya kikatiba. Lakini mahakama imetoa hukumu bila kuangalia haki za kikatiba za kupiga kura kwa sababu waliotoa tuhuma hawakuthibitisha kikamilifu au hawakuonyesha kuwa wataumia vipi kisheria au vitendo vya mtuhumiwa vimewaumiza vipi wao - Locus Standi.

Nimeisoma hukumu na sikuona imehusisha watu kunyimwa haki zao za kikatiba za kupiga kura au ukiukwaji wa zoezi la kupiga kura. Hivyo hukumu ya kesi hii haitatumika kama masuala ya uchaguzi.

Na kama itatumika, basi itatumika katika masuala ya Locus Standi. Hivyo mjadala mzima huu ungekuwa na uzito zaidi kama tungeuliza ni nani Locus Standi? Kwa mfano Nyani Ngabu unauliza je mpiga kura wa Igunga anaweza kumshitaki Mnyika?
 
Kufungua kesi ni tofauti na kushinda hiyo kesi. Mtanzania yoyote anaweza kufungua kesi kama hii, but whether his/her claims will be successful is entirely a different matter.

You’re absolutely right. This is all to do with the adversarial system we use. Tofauti na inquisitorial system in which the role of the judge is central, in adversarial system, the judge’s role ni kama ya refa tuu. The parties plays the game. Atakayeshinda ni yule ambaye ana strong legal argument and robust evidence.

In adversarial system, kinachotafutwa siyo ukweli. The judge is not interesting on who is saying the truth, but who has strong legal arguments backed up with robust evidence.

Kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa walalamikaji kwenye kesi ya Lema walikuwa wanasema ukweli, but lacked legal arguments to support their claim, i.e. locus standi.

Ni kweli hii kesi ilifunguliwa katika mazingira ya kisiasa. Kama walalamikaji wangeileta kisheria zaidi, wala isingefika Mahakama ya Rufaa.

Sidhani kama kinachoangaliwa ni whether mlalamikaji ni mwanachama wa chama fulani. Kinachoangaliwa ni whether mlalamikaji was a registered voter. Otherwise, kama wakichukua kigezo cha malalamikaji kuwa mwanachana wa chama cha siasa, vipi wale ambao hawana vyama?

EMT;

Shukrani kwa majibu na nyongeza zako, shule tosha. Ni kweli kufungua kesi si lazima ushinde. Lakini kuna manufaa makubwa kwa kesi kwenda mahakamani. Chukulia mfano wa hii kesi ya Lema. Kwa wanachama wa CDM, watakuwa wanashangilia. Na wengi watachangilia bila kujua jinsi hukumu ilivyohitimishwa.

Ukichukulia wanafunzi wa sheria walipo vyuoni au wahitimu walio kwenye intern, mijadala itakuwa ni kwenye kiini cha hitimisho la kesa, locus standi.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
JokaKuu Tatizo siyo kesi ilifunguliwa chini ya kifungu kipi pekee. Ni kweli wahusika ili kudai haki chini ya Ibara 26 (2) ilitoa mwanya kwa Mahakama ya Rufaa kuwabeza lakini kwa manufaa ya umma walipaswa wapitie vielelezo vya ushahidi ambavyo Jaji Mujulizi hakuvipiti kama zile video ili tujue madai ya walalamikaji wa mwanzo yalikuwa ni nini?

Walichofanya Mahakama ya RUfaa ni kutunyima nafasi ya kuelewa Mahakama ya Rufaa ina msimamo upi kuhusiana na matumizi ya lugha zenye mushkeli kwenye kampeni..........mamlaka ya kuutathmini ushaidi husika wanayo lakini sijui ni uvivu hata haieleweki............na mbaya zaidi sasa wansema hata kama kesi hiyo ingefunguliwa chini ya Ibara 26(2) bado wapinga rufani hawana mahali pa kusimamia kwenye suala hilo kutokana na tafsiri ambazo walizitoa....................hii ni aibu na kuna kila sababu ya wapinga rufani kuirudia mahakama ya Rufaa kurekebisha hii hukumu kwa manufaa ya jamii nzima.....................Mahakamani siyo mahali pa kutunga sheria au kzitafsiri sheria visivyo
Rutashubanyuma,

..nadhani tatizo ni la upande wa hao wapiga kura watatu wa CCM.

..makosa yao ya "kiufundi" ndiyo yaliyosababisha mahakama ikaamua hivyo ilivyoamua.

..unachopendekeza wewe, kwa mtizamo wangu, ni sawa na mahakama kujipa jukumu la wapinga rufani[wapiga kura wa CCM].

..zaidi, nashangaa unapoangalia maslahi ya hawa wapiga kura watatu, huku ukiwapuuza malaki ya wapiga kura waliompa Lema ushindi.

NB:

..je, kuna uwezekano wa kumshtaki Lema kwa matamshi yake kwa kutumia kesi ya madai, bila kuilazimisha mahakama kubatilisha matokeo ya uchaguzi huu?
 
..kitendo hicho kingeifanya mahakama ya rufaa kupoteza heshima yako na kuonekana wanapendelea upande mmoja.

naomba EMT na Nyani Ngabu wanieleweshe jambo hapa.

hivi kwa mfano mm nimetoa hela yangu inunue kitu kwaajili ya jamii na mimi ni jamii iyo iyo, ila aliyeipokea ni mhazini wa jamii husika je asipofanya kama madhumuni ya hela yalivyokuwa nani anapaswa kumshtaki??

je mm mtoa hela naweza kumshtaki?? na je jamii husika inaweza kushtaki??

nauliza hayo manake inaposemekana kwamba mtu asitafute huruma ya jamii bali aende kushtaki yeyey kama yeye ilihali jamii ahusika ndo mashahidi napata utata hapa. anyway mm sio mtaalam wa sheria labda ndo mana nachukua muda zaid kuelewa mantiki husika.
 
Kama nimekuelewa hapa kama vile unaongelea fiduciary relationship, ambapo a fiduciary takes care of another’s property for the benefit of others

Anayetoa pesa ni settlor, anaye-take care hizo pesa ni trustee na anayenufauka na hizo pesa ni beneficiary (mnufaika).

Kisheria, beneficiary hana legal title kwenye hizo pesa, lakini ana kitu ambacho, in equity, kinaitwa equitable interest.

Sidhani kama nitaweza kukulezea ukaelewa maana hii ni course ya mwaka mzima kwa mwanafunzi wa sheria. Inaitwa Equity and Trusts.

Kimsingi, sidhani kama ina uhusiano wowote na masuala ya uchaguzi kwa sababu wakati Lema anamwaga hayo "matusi" sidhani kama alikuwa na fiduciary duty kwa mtu yoyote yule.
 
[h=2]Maswali manne katika hukumu ya lema[/h]
1. Waheshimiwa majaji wa mahakama ya Rufaa wanaanza na kuhoji kama kweli palikuwa na ushahidi wowote katika Mahakama Kuu kama walalamikaji walikuwa ni wapiga kura? Inajitokeza katika faili la Mahakama Kuu na mwenendo mzima kwamba katika Hati yao ya madai (Petition) waliambatanisha card zao za kupigia kura. Mahakama ya Rufaa inajiridhisha baada ya kupitia rejea mbalimbali za sheria kwamba card ya kupigia kura ni ushahidi kwamba mwenye kadi ni mpiga kura. Majaji hawasemi kwamba katika Hati zao za Majibu (Reply to the Petition) walalamikiwa waliwahi kukanusha madai kwamba walalamikaji walikuwa ni wapiga kura au kutilia shaka nakala za kadi za kura zilizoambatanishwa katika Hati ya Madai. Hivi kisheria mtu anatakiwa adhibitishe nini? Sheria ya Mwenendo wa Madai kama ilivyo sheria ya Mwenendo wa Jinai inampa jukumu mtu kutoa ushahidi juu ya mambo yanayobishaniwa. Kama suala la upiga kura wa wajibu rufani haikuwa moja kati ya mambo ya kimantiki yaliyokuwa yanabishaniwa wakati wa trial ni jambo gani lililowapa dhima ya kiudhibitishi 9burden of proof) wajibu rufaa kudhibitisha upiga kura wao?

2. Tujalie kwamba suala la wao kuwa wapiga kura lilikuwa katika issue. Je uwepo wa nakala za hati walizoambatanisha ulikuwa katika issue? Mwenendo wa kesi na pia hukumu ya Mahakama ya Rufaa haioneshi hivyo. Kinachojitokeza ni ubishi wa kisheria kama kuwa tu mpiga kura kunampa mtu mguu wa kusimamia katika kesi (locus). Sina tatizo lolote na waheshimiwa majaji wa mahakama ya Rufani kujielekeza katika hili hata kama haikuwa moja ya sababu za rufani. Tatizo langu ni kupinga uwasilishwaji wa nyaraka na sheria kwa sababu ya walichokiita mazoea ya kimahakama. Kanuni
za mwenendo wa mashauri ya uchaguzi za 2010 ambazo kimsingi ndio sheria mahususi zinazoratibu kesi za uchaguzi zinataka nyaraka ambazo uwepo wake na uhalali wake haubishaniwi zipokelewe mahakamani kabla kesi haijaanza kusikilizwa kwa kuletwa mashahidi. Sasa kwa hali ya kawaida ni nani anapaswa kuleta documents hizo kama ushahidi? Hivi kwenye kesi za jinai zinazosikilizwa na mahakama kuu nyaraka ambazo hazibishaniwi uwepo na uhalali wake hutolewa na nani na kwa wakati gani? Wenzangu mtanikosowa, nijuavyo mimi hutolewa na mawakili wakati wa
usikilizwaji wa awali. Ni utaratibu huo huo sheria imeweka katika mashauri ya uchaguzi. Nadhani majaji hawakupaswa kulitolea maamuzi suala hili kwa mtindo walioutumia wa kuibua wenyewe na kutolea majibu. Wangetumia utaratibu wa kawaida wa kirefa wa kuwapa nafasi mawakili wote walizungumzie suala hilo wangepata faida zaidi. Maana, mawakili wangeweza kuwapa ukweli huu wa kisheria. Tukubaliane kwamba sheria zetu za uchaguzi bado mpya sio rahisi kuona vitu vyote.

3. majaii wanasema msingi wa locus ni common law. Mimi nasema msingi wa locus utabaki kuwa ni common law kama sheria zetu ziko kimya (kama kuna lacunae). Usahihihi, kwa maoni yangu, msingi wa locus katika kesi za uchaguzi Tanzania ni Sheria ya Uchaguzi. Sheria hiyo inatamka wazi wazi kwamba locus ya kufungua kesi za uchaguzi inatokana na mtu kuwa mgombea au mpiga kura au Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hekima ya sheria kumpa mpiga kura haki hiyo
sio ngumu kuibaini. Kwamba kupiga kura kama ilivyo kupigiwa kura ni haki ya msingi ya kikatiba na kidemokrasia. Maana, kama mtu alieshinda kwa kuvunja sheria atashinda, mpiga kura ataathirika kwa mtu asio chaguo lake kuchaguliwa. Sioni ni kwa nini majaji wa mahakama ya rufaa waliongeza maneno katika kifungu cha sheria ya uchaguzi wakati hakina utata wowote na wala maneno yaliyomo katika kifungu hicho yakitafsiriwa na msingi mzima wa sheria ya uchaguzi hayaleti picha ya kama bunge lilikuwa na nia nyingine zaidi ya kumpa haki mpiga kura kutetea kura zake.

4. Majaji pia wamesema kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi sio public interest ili kuangukia katika locus iliyomo katiba kuhusiana na public interest litigations. Sababu yao kubwa ni kwamba kesi za uchaguzi haziwaathiri sehemu yote ya jamii. Mengi yanaweza kusemwa juu ya hili. Lakini jaalia walalamikaji walikuwa wanalalamikia uchaguzi wa Raisi unayohusisha sehemu yote ya watanzania, source kuu ya locus ingekuwa ni katiba au sheria ya uchaguzi? Nionavyo mimi, maadamu sheria ya uchaguzi inatamka bayana kwamba mpiga kura anayo locus, hamna sababu yoyote ya kwenda kwenye sheria nyeti kama katiba. Majaji nionavyo mimi, walijielekeza sana kwenye common law na kusahau kwamba common law ni dhalili kwa sheria za nchi zilizopo.

Hayo ni maoni yangu tu kutokana na uamuzi wa mahakama ya rufaa. Naona uamuzi huu unaifanya mahakama kuwa na uwezo wa kurekebisha sheria wanayoiona kuwa mbaya kwa mlango wa nyuma. Hii inaingilia mgawanyo wa mamlaka baina ya mihimili mikuu ya dola. Kipimo pekee cha mahakama kurekebisha sheria ni kama sheria hiyo inakinzana na katiba. Mahakama inaweza kuifuta sheria hiyo kwa misingi kwamba ilikuwa haramu toka utotoni. Maana, kama Mahakama inavyopata uhalali wake wa kutafsiri sheria toka katika Katiba, Bunge pia linapata uhalali wake wa kutunga sheria toka katika Katiba. Sheria kama inapingana na katiba maana yake haitokani na katiba, kwa hiyo ni haramu. Sasa kama Mahakama itatoa hukumu zinazopingana na katiba ni nani atakaezitangaza hukumu hizo kuwa batili?
 
Rutashubanyuma,

..nadhani tatizo ni la upande wa hao wapiga kura watatu wa CCM.

..makosa yao ya "kiufundi" ndiyo yaliyosababisha mahakama ikaamua hivyo ilivyoamua.

..unachopendekeza wewe, kwa mtizamo wangu, ni sawa na mahakama kujipa jukumu la wapinga rufani[wapiga kura wa CCM].

..kitendo hicho kingeifanya mahakama ya rufaa kupoteza heshima yako na kuonekana wanapendelea upande mmoja.

..zaidi, nashangaa unapoangalia maslahi ya hawa wapiga kura watatu, huku ukiwapuuza malaki ya wapiga kura waliompa Lema ushindi.

NB:

..je, kuna uwezekano wa kumshtaki Lema kwa matamshi yake kwa kutumia kesi ya madai, bila kuilazimisha mahakama kubatilisha matokeo ya uchaguzi huu?

JokaKuu Hatujui hadi leo ni nini haswa Lema alisema kwenye hiyo mikanda ya kideo na ambacho ndiyo msingi wa kesi hii. Mahakama zote zilikwepa kuchunguza kiini cha mgogoro na hivyo hatuko kwenye nafasi ya kujua kama matamshi yake yanagusa makosa ya kesi ya jinai.

Kuhusu malaki ya waliopiga kura jimbo la Arusha...............hilo linaamana kama sheria ya uchaguzi ilizingatiwa kama haikuzingatiwa uchaguzi huo haukuwa huru wala wa haki kwa hiyo uwingi wa wapigakura hauwezi kufifilisha misingi ya kidemokrasia..............
 
Last edited by a moderator:
naomba EMT na Nyani Ngabu wanieleweshe jambo hapa.

hivi kwa mfano mm nimetoa hela yangu inunue kitu kwaajili ya jamii na mimi ni jamii iyo iyo, ila aliyeipokea ni mhazini wa jamii husika je asipofanya kama madhumuni ya hela yalivyokuwa nani anapaswa kumshtaki??

je mm mtoa hela naweza kumshtaki?? na je jamii husika inaweza kushtaki??

nauliza hayo manake inaposemekana kwamba mtu asitafute huruma ya jamii bali aende kushtaki yeyey kama yeye ilihali jamii ahusika ndo mashahidi napata utata hapa. anyway mm sio mtaalam wa sheria labda ndo mana nachukua muda zaid kuelewa mantiki husika.

gfsonwin naona wengine umetuzuia tusichangie................
 
Kimsingi, sidhani kama ina uhusiano wowote na masuala ya uchaguzi kwa sababu wakati Lema anamwaga hayo "matusi" sidhani kama alikuwa na fiduciary duty kwa mtu yoyote yule.

EMT Are u sure?

A fiduciary person is a person bound to act for another's benefit, as a trustee in relation to his beneficiary

Unataka kutuambia anayegombania nafasi ya uongozi tena ya uwakilishi hana uwajibikaji kwa wapigakura wake na anaweza kujifanyia vyovyote atakavyo?
 
Last edited by a moderator:
Maswali manne katika hukumu ya lema

1. Waheshimiwa majaji wa mahakama ya Rufaa wanaanza na kuhoji kama kweli palikuwa na ushahidi wowote katika Mahakama Kuu kama walalamikaji walikuwa ni wapiga kura? Inajitokeza katika faili la Mahakama Kuu na mwenendo mzima kwamba katika Hati yao ya madai (Petition) waliambatanisha card zao za kupigia kura. Mahakama ya Rufaa inajiridhisha baada ya kupitia rejea mbalimbali za sheria kwamba card ya kupigia kura ni ushahidi kwamba mwenye kadi ni mpiga kura. Majaji hawasemi kwamba katika Hati zao za Majibu (Reply to the Petition) walalamikiwa waliwahi kukanusha madai kwamba walalamikaji walikuwa ni wapiga kura au kutilia shaka nakala za kadi za kura zilizoambatanishwa katika Hati ya Madai. Hivi kisheria mtu anatakiwa adhibitishe nini? Sheria ya Mwenendo wa Madai kama ilivyo sheria ya Mwenendo wa Jinai inampa jukumu mtu kutoa ushahidi juu ya mambo yanayobishaniwa. Kama suala la upiga kura wa wajibu rufani haikuwa moja kati ya mambo ya kimantiki yaliyokuwa yanabishaniwa wakati wa trial ni jambo gani lililowapa dhima ya kiudhibitishi 9burden of proof) wajibu rufaa kudhibitisha upiga kura wao?

2. Tujalie kwamba suala la wao kuwa wapiga kura lilikuwa katika issue. Je uwepo wa nakala za hati walizoambatanisha ulikuwa katika issue? Mwenendo wa kesi na pia hukumu ya Mahakama ya Rufaa haioneshi hivyo. Kinachojitokeza ni ubishi wa kisheria kama kuwa tu mpiga kura kunampa mtu mguu wa kusimamia katika kesi (locus). Sina tatizo lolote na waheshimiwa majaji wa mahakama ya Rufani kujielekeza katika hili hata kama haikuwa moja ya sababu za rufani. Tatizo langu ni kupinga uwasilishwaji wa nyaraka na sheria kwa sababu ya walichokiita mazoea ya kimahakama. Kanuni
za mwenendo wa mashauri ya uchaguzi za 2010 ambazo kimsingi ndio sheria mahususi zinazoratibu kesi za uchaguzi zinataka nyaraka ambazo uwepo wake na uhalali wake haubishaniwi zipokelewe mahakamani kabla kesi haijaanza kusikilizwa kwa kuletwa mashahidi. Sasa kwa hali ya kawaida ni nani anapaswa kuleta documents hizo kama ushahidi? Hivi kwenye kesi za jinai zinazosikilizwa na mahakama kuu nyaraka ambazo hazibishaniwi uwepo na uhalali wake hutolewa na nani na kwa wakati gani? Wenzangu mtanikosowa, nijuavyo mimi hutolewa na mawakili wakati wa
usikilizwaji wa awali. Ni utaratibu huo huo sheria imeweka katika mashauri ya uchaguzi. Nadhani majaji hawakupaswa kulitolea maamuzi suala hili kwa mtindo walioutumia wa kuibua wenyewe na kutolea majibu. Wangetumia utaratibu wa kawaida wa kirefa wa kuwapa nafasi mawakili wote walizungumzie suala hilo wangepata faida zaidi. Maana, mawakili wangeweza kuwapa ukweli huu wa kisheria. Tukubaliane kwamba sheria zetu za uchaguzi bado mpya sio rahisi kuona vitu vyote.

3. majaii wanasema msingi wa locus ni common law. Mimi nasema msingi wa locus utabaki kuwa ni common law kama sheria zetu ziko kimya (kama kuna lacunae). Usahihihi, kwa maoni yangu, msingi wa locus katika kesi za uchaguzi Tanzania ni Sheria ya Uchaguzi. Sheria hiyo inatamka wazi wazi kwamba locus ya kufungua kesi za uchaguzi inatokana na mtu kuwa mgombea au mpiga kura au Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hekima ya sheria kumpa mpiga kura haki hiyo
sio ngumu kuibaini. Kwamba kupiga kura kama ilivyo kupigiwa kura ni haki ya msingi ya kikatiba na kidemokrasia. Maana, kama mtu alieshinda kwa kuvunja sheria atashinda, mpiga kura ataathirika kwa mtu asio chaguo lake kuchaguliwa. Sioni ni kwa nini majaji wa mahakama ya rufaa waliongeza maneno katika kifungu cha sheria ya uchaguzi wakati hakina utata wowote na wala maneno yaliyomo katika kifungu hicho yakitafsiriwa na msingi mzima wa sheria ya uchaguzi hayaleti picha ya kama bunge lilikuwa na nia nyingine zaidi ya kumpa haki mpiga kura kutetea kura zake.

4. Majaji pia wamesema kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi sio public interest ili kuangukia katika locus iliyomo katiba kuhusiana na public interest litigations. Sababu yao kubwa ni kwamba kesi za uchaguzi haziwaathiri sehemu yote ya jamii. Mengi yanaweza kusemwa juu ya hili. Lakini jaalia walalamikaji walikuwa wanalalamikia uchaguzi wa Raisi unayohusisha sehemu yote ya watanzania, source kuu ya locus ingekuwa ni katiba au sheria ya uchaguzi? Nionavyo mimi, maadamu sheria ya uchaguzi inatamka bayana kwamba mpiga kura anayo locus, hamna sababu yoyote ya kwenda kwenye sheria nyeti kama katiba. Majaji nionavyo mimi, walijielekeza sana kwenye common law na kusahau kwamba common law ni dhalili kwa sheria za nchi zilizopo.

Hayo ni maoni yangu tu kutokana na uamuzi wa mahakama ya rufaa. Naona uamuzi huu unaifanya mahakama kuwa na uwezo wa kurekebisha sheria wanayoiona kuwa mbaya kwa mlango wa nyuma. Hii inaingilia mgawanyo wa mamlaka baina ya mihimili mikuu ya dola. Kipimo pekee cha mahakama kurekebisha sheria ni kama sheria hiyo inakinzana na katiba. Mahakama inaweza kuifuta sheria hiyo kwa misingi kwamba ilikuwa haramu toka utotoni. Maana, kama Mahakama inavyopata uhalali wake wa kutafsiri sheria toka katika Katiba, Bunge pia linapata uhalali wake wa kutunga sheria toka katika Katiba. Sheria kama inapingana na katiba maana yake haitokani na katiba, kwa hiyo ni haramu. Sasa kama Mahakama itatoa hukumu zinazopingana na katiba ni nani atakaezitangaza hukumu hizo kuwa batili?

George Jinasa

Khoja yako ya kwanza

Suala la uhalali wa wapinga rufani kama kweli walijiandikisha kama wapigakura wa jimbo la uchaguzi wa Arusha halikuwa kwenye hadidu za rejea za waleta rufani. Mahakama ya Rufani yenyewe ilikwisha kuagiza ya kuwa mahakama zishughulikie maeneo ambayo yanabishiwa tu isianzishe mazogo yake yenyewe. Hili ni zogo lilioanzishwa na mahakama yenyewe kinyume na maelekezo yao.

Ubishi ni kitambulisho cha mpigakura na ni nani anapaswa kukiwakilisha mahakamani na ukumbuke wengi hutumia vitambulisho takwa kama vitambulisho vya kawaida na siyo rahisi vibaki kwenye jarida la kimahakama. Kudai mashahidi ndiyo wakilishe ushahidi wenyewe badala ya mawakili wao huu ni utaratibu mpya kabisa...............na rekodi za kimahakama ambazo hazishindaniwi huwa hakuna sababu ya mahakama kuendelea kuzitunza.................kama vitmbulisho ambavyo wahusika walivihitaji kukabiliana na kero za kila siku kama kupata huduma mbalimbali kutoka kwenye jamii.....
 
Last edited by a moderator:
The verdct is among the good judgement in our country,you cannot challenge anything that you were not injured,you have to show how the act your complaining affected you personally not to come complaining without reasonable course.

In short matters of locus stand were raised by both the ag and lemas advocate and we expected the trial judges to make a rulling on it favourable to the lema side but to the surporise it was different.

Election result are voice of perple which need be respected. this also is not new in the case of wilblod slaa against arusha kalwa the voters were asked to show injuries they suffered only to find that there vote was a problem they were adviced that they have to add there vote to person they want if he will win, automatically he failed and the case come to end.so this is not new, challenging election result you have to show the injury you sufferd.

Its costive to call another election on unreasonable ground,simply to sutisfy one or two or three person the hired gun.with this jurgement all the case like that of meatu and shinyanga are dead cases, i advice them to withdral.

The isssue of integrity of election are protected by the c ommision of election through established principles that give power to several organs to oversee the campaing process including the ag,police and obsevers we belive election which are not objected by them is genuine.
 
Nakubaliana na wewe Jokakuu, ila I would say katika hio ruling the most interesting part kwa upande wangu ni udadafuzi wao juu ya victim kushitaki mwenyewe akihisi/ona kaonewa as opposed to kushitaki on behalf of the victim na the fact ya namna inavyokuwa transparent jinsi gani sheria inaweza tafsiriwa in what ever way as long as unaweza simamia hicho kipengele.

Hii inafanya some how iwe aibu sana kwa aliye toa hukumu awali kwa case ambayo ilikuwa apparent kuwa haina uzito tokana na vielelezo na hoja zilizowakilishwa........

Unajua wanasheria mtaendelea kutusaidia na pia kutuchanganya. Hivi hoja kuu katika kesi ya Arusha ilikuwa ni nini hasa mgombea kukashifiwa?

Voting irregularity and unfair election. Kama ni kukashifiwa basi haki ya kutafuta repair siyo ya kila mtu isipokuwa aliyekashifiwa tu. Kama ni voting irregularity na unfair election basi mpiga kura anaweza kulalamika na ana haki ya kusikilizwa.
 
Kaka Rutashubanyuma, mimi naona si haki kwa mtu ambaye haki yake haijaathiriwa na kampeni za uchaguzi kwenda kupinga matokeo mahakamani kwani hii inawanyima haki wapiga kura wengi ambao walikuwa na haki ya kumchagua waliyekuwa wanamtaka.
 
Last edited by a moderator:
Kama nimekuelewa hapa kama vile unaongelea fiduciary relationship, ambapo a fiduciary takes care of another's property for the benefit of others

Anayetoa pesa ni settlor, anaye-take care hizo pesa ni trustee na anayenufauka na hizo pesa ni beneficiary (mnufaika).

Kisheria, beneficiary hana legal title kwenye hizo pesa, lakini ana kitu ambacho, in equity, kinaitwa equitable interest.

Sidhani kama nitaweza kukulezea ukaelewa maana hii ni course ya mwaka mzima kwa mwanafunzi wa sheria. Inaitwa Equity and Trusts.

Kimsingi, sidhani kama ina uhusiano wowote na masuala ya uchaguzi kwa sababu wakati Lema anamwaga hayo "matusi" sidhani kama alikuwa na fiduciary duty kwa mtu yoyote yule.

umenijibu vyema sana mie hapa hapa nataka kupata jibu la swali hili hapa
kama Lema alimtusi mgombea mwenzie hadharani, na ikathibitika kwamba ametusi mtu hivi ni kosa kwa aliyemskia kumshtaki hata kama hatukanwi yy?? na je hivi kama mtu anaiba nyumba ya jiran mm ambaye sio jiran sipaswi kuita mwizi simply kwamba sina faida yyte ama hasara kwa anayeibiwa??
 
This matter is a done deal; Lissu did not make any rulling here he was only an appelant consel; your cries of the wolf do not matter and will not change the decision; why didnt you apply to appear in matter as a friend of the court so you could make your voice heard and make a positive intervention?! if you want you may appeal to the law reform commission. The US election law has no bearing on our law of the land; it is not a matter of copy paste.
 
Back
Top Bottom