The Lema Verdict: Did the Court of Appeal encroach on litigation rights of a voter?

EMT Are u sure?

A fiduciary person is a person bound to act for another's benefit, as a trustee in relation to his beneficiary

Yes, I'm sure. Under what basis can you ague that the relationship between an election candidate and a constituent is fiduciary in nature? A candidate does not have a fiduciary duty until s/he is elected or appointed to the relevant position. Otherwise, those who apply to become directors of companies will have fiduciary duty even before being offered the directorship.

It is only when once elected or appointed that such person will have a fiduciary duty to act in the best interests of the constituent. A fiduciary is a person who has a duty to act on behalf of and for the benefit of another with the utmost in good faith, loyalty, candor, and care. As soon as a candidate is elected as an MP, s/he is trusted as a fiduciary of the constituent to represent its people in their best interest, above any personal interests.

However, you should note that even where a person is elected as an MP, there is no a job description for MPs. Political scientists, civil servants and politicians themselves have long struggled to define the complex combination of moral and ethical obligations that make up the relationship between constituents and elected politicians.

Nonetheless, fiduciary relationships have expanded beyond the original application to trustees and beneficiaries. Thus, there is a case for extending fiduciary duty to elected MPs (not election candidate) due to the deeper relationship that exists, or which should exist, between an MP and a citizen.

Unataka kutuambia anayegombania nafasi ya uongozi tena ya uwakilishi hana uwajibikaji kwa wapigakura wake na anaweza kujifanyia vyovyote atakavyo?

An election candidate has fiduciary duties to the party that nominate him/her at the beginning of the electoral process. Hataweza kujifanyia vyoyote atakavyo simply because such candidate makes a pledge – sometimes implicitly and sometimes explicitly – to follow party rules.

Once elected, s/he may have additional fiduciary duties to the constituent as well as to the country. But before the election, s/he does not have fiduciary role to the constituent. If s/he had, there would be no need to conduct the election in the first place.
 
umenijibu vyema sana mie hapa hapa nataka kupata jibu la swali hili hapa
kama Lema alimtusi mgombea mwenzie hadharani, na ikathibitika kwamba ametusi mtu hivi ni kosa kwa aliyemskia kumshtaki hata kama hatukanwi yy?? na je hivi kama mtu anaiba nyumba ya jiran mm ambaye sio jiran sipaswi kuita mwizi simply kwamba sina faida yyte ama hasara kwa anayeibiwa??

Kuna mtu nafikiri ni Gaijin amehoji kitu kama hicho nikauliza kama Kaunga akikutukana wewe kwa hiyo mie niwahi fasta mahakamani kumshtaki? Kuna tofauti kati ya makosa ya madai na makosa ya jinai. Kwenye makosa ya madai yanahusisha zaidi private individuals; kwa hiyo mwenye haki ya kushtaki ni yule ambaye haki yake binafsi imevunjwa. Kwenye makosa ya jinai anayeshtaki ni Jamhuri kwa sababu kosa la jina linatendeka against the public.

Pia nikufahamishe kuwa kama umemwona mwizi anaiba kwa jirani huna jukumu la kisheria kupiga yowe. Unaweza ukakaa kimya tuu na wala hutakuwa umetenda kosa lolote. Kama ukipiga yowe halafu huyo mwizi akakupiga na kitu chenye nje kali hutaweza kumshtaki aliyekuwa anaibiwa eti kwa sababu ulikuwa unamsaidia kupiga yowe asiibiwe.

Ni hivyo hivyo kama umemkuta mtoto mdogo anazama kwenye dimbwi la maji na kuamua kupita bila kumwokoa. Huna wajibu wa kisheria kumwokoa na hakuna ambaye atakushtaki kwa kutomwokoa huyo mtoto unless labda alikuwa ni mtoto wako.

"Thou shall not kill but needst not strive, officiously, to keep another alive."

Kuna exceptions lakini. Kwa mfano, kama kuna sheria ambayo imepitishwa na bunge ikisema kuwa kama ukimwona mwizi anaiba basi piga yowe halafu wewe usipige yowe, then utakuwa umetenda kosa. Pia pale ambapo ume-create hali hatari inayoweza kusababisha madhara kwa watu au mali za watu una duty ya kuchukua reasonable steps to avert the danger.

Pia daktari ana duty ya kukupa the appropriate medical care unayostahili na aki-omit kufanya hivyo atakuwa ametenda kosa. Na pia kama umeajiriwa kimkataba pale Mzimbazi kufunga geti ili treni ipite halafu were ukaacha kufunga geti treni ikapita na kugonganza na magari na kusababisha vifo au madhara, then utatakuwa umetenda kosa la jinai.

I miss Dr. Harrison Mwakyembe.
 
love you too swthrt.

asante kwa kumfundisha mama yako manake leo niko kwenye hili darasa hadi kieleweke sichez mbali hadi nielewe sheria ya uchaguzi.

Una mpango wa kutangaza nia hivi karibuni?
 
una mpango wa kutangaza nia hivi karibuni?

hahahhaha! Sasa ndo wanaokula nchi bana mie na ualim nimebaki msaga mashine tu ngoja nijaribu upande wa pili nione lol!
 
  • Thanks
Reactions: EMT

Haya bana. Ila ukitangaza nia kuwa makini maana huyu aliyemfungulia kesi Lema ( aka Mussa Mkanga) ana tabia ya kuwafungulia kesi wabunge walioshinda hasa wale wa upinzani.

Kama sijakosea, katika uchaguzi wa mwaka 1995 alimfungulia kesi Makongoro Nyerere aliyekuwa ameshinda ubunge jimbo la Arusha kupitia NCCR-Mageuzi na kusababisha Makongoro kupoteza ubunge.

Hii inafanya mtu ajiulize hivi ni kwani nini haki za Mkanga tuu ndiyo huwa zinazoathirika kila kunapofanyika uchaguzi jimbo la Arusha na mbunge wa upinzani akashinda? Why always him? Nafikiri Mahakama ya Rufaa iliangalia hilo na kuamua labda ku-interpret strictly the relevant provision on public policy grounds.

Otherwise, ingekuwa ni fasheni kwa mpiga yoyote kumshtaki aliyeshinda uchaguzi. Pia baadhi ya wapiga kura waliofungua kesi wangeweza kutumia hiyo sheria kudai rushwa kwa waliofunguliwa kesi ili ku-drop kesi.

Halafu ukiangalia kwa mapana zaidi wanaofunguliwa kesi na wapiga kura ni wagombea wa upinzani walioshinda kwenye majimbo yao. Tundu Lissu alifunguliwa kesi na wapiga kura. Mnyika nae alifunguliwa kesi na aliyeshindwa pamoja na wapiga kura.

Labda tuangalie ni kwa nini kuna sheria inayoruhusu wa wapiga kura kushtaki walioshinda uchaguzi. Kwa kawaida sheria huwa zinapitishwa kwa sababu fualani.

Sheria ya kuruhusu wapiga kura kumshtaki aliyeshinda uchaguzi tumeitoa kwa mkoloni wetu Mwingereza. Sheria hii ilianzishwa Uingereza mwaka 1868 ili kuimarisha system ya kurithi vyeo.

Mtoto alikuwa anarithi ubunge kutoka kwa baba yake kama mali vile. Sasa ili kuendeleza huyo urithi ilikuwa ni muhimu kuruhusu wapiga kura kushtaki. Lakini kuruhusu wapiga kura kushtaki ilikuwa ni cover tuu maana wapiga kura wa kaiwaida hawakuwa na uwezo wa kuendesha kesi zenye gharama kubwa kama za uchaguzi.

Kwa hiyo, hapo ilikuwa ni kuwawezesha warithi (ambao of course walikuwa na uwezo) kushtaki kama waliyetegemea kumrithi akishindwa uchaguzi. Kwa maana nyingine, kuruhusu mpiga kura kumshtaki aliyeshinda uchaguzi ilikuwa ni ku-maintain chain ya inheritance.

Sisi tume-copy na ku-paste hiyo sheria ya mwaka 47 bila kuangalia kama inaweza kutumika effectively kwenye mazingira yetu.
 
Haya bana. Ila ukitangaza nia kuwa makini maana huyu aliyemfungulia kesi Lema ( aka Mussa Mkanga) ana tabia ya kuwafungulia kesi wabunge walioshinda hasa wale wa upinzani.

Kama sijakosea, katika uchaguzi wa mwaka 1995 alimfungulia kesi Makongoro Nyerere aliyekuwa ameshinda ubunge jimbo la Arusha kupitia NCCR-Mageuzi na kusababisha Makongoro kupoteza ubunge.

Hii inafanya mtu ajiulize hivi ni kwani nini haki za Mkanga tuu ndiyo huwa zinazoathirika kila kunapofanyika uchaguzi jimbo la Arusha na mbunge wa upinzani akashinda? Why always him? Nafikiri Mahakama ya Rufaa iliangalia hilo na kuamua labda ku-interpret strictly the relevant provision on public policy grounds.

Otherwise, ingekuwa ni fasheni kwa mpiga yoyote kumshtaki aliyeshinda kesi. Pia baadhi ya wapiga kura waliofungua kesi wangeweza kutumia hiyo sheria kudai rushwa kwa waliofunguliwa kesi ili ku-drop kesi.

Halafu ukiangalia kwa mapana zaidi wanaofunguliwa kesi na wapiga kura ni wagombea wa upinzani walioshinda kwenye majimbo yao. Tundu Lissu alifunguliwa kesi na wapiga kura. Mnyika nae alifunguliwa kesi na aliyeshindwa pamoja na wapiga kura.

Labda tuangalie ni kwa nini kuna sheria inayoruhusu wa wapiga kura kushtaki walioshinda uchaguzi. Kwa kawaida sheria huwa zinapitishwa kwa sababu fualani.

Sheria ya kuruhusu wapiga kura kumshtaki aliyeshinda uchaguzi tumeitoa kwa mkoloni wetu Mwingereza. Sheria hii ilianzishwa Uingereza mwaka 1868 ili kuimarisha system ya kurithi vyeo.

Mtoto alikuwa anarithi ubunge kutoka kwa baba yake kama mali vile. Sasa ili kuendeleza huyo urithi ilikuwa ni muhimu kuruhusu wapiga kura kushtaki. Lakini kuruhusu wapiga kura kushtaki ilikuwa ni cover tuu maana wapiga kura wa kaiwaida hawakuwa na uwezo wa kuendesha kesi zenye gharama kubwa kama za uchaguzi.

Kwa hiyo, hapo ilikuwa ni kuwawezesha warithi (ambao of course walikuwa na uwezo) kushtaki kama waliyetegemea kumrithi akishindwa uchaguzi. Kwa maana nyingine, kuruhusu mpiga kura kumshtaki aliyeshinda uchaguzi ilikuwa ni ku-maintain chain ya inheritance.

Sisi tume-copy na ku-paste hiyo sheria ya mwaka 47 bila kuangalia kama inaweza kutumika effectively kwenye mazingira yetu.
kiukweli siasa ina mambo??

unajua nini kama watu wanaweza kuwa bribed ili wampigie kura fulan basi watu hao hao wanaweza kauwa bribed ili kupinga matokeo ya uchaguzi na kiswahili rahisi ni kwamba huu ni mtaji kwa huyu Mussa Mkanga.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Yes, unaweza kupitia katiba to defend the constitution and the legality.

Lakini pia kuna mechanisms za kumripoti kiongozi ambaye unadhani au una ushahidi kuwa siyo raia wa Tanzania.

Why don't use those mechanims na kuachia vyombo husika kushughulikia hilo suala?

Kama kuna kiongozi ambaye hana uraia wa Tanzania haina maana kuwa lazima hilo suala liamuliwe na mahakama.

The court should always be used as the last resort.

EMT;

Hapana mkuu. Kwa maoni yangu na huku nje ninakokaa mahakama ni lazima iwe chombo cha kutoa haki. Tukiendelea kutegemea vyombo vya kiserikali kutenda haki, serikali yenyewe itaanza kuwa-abuse haki za watu. Huku nje nina uhuru wa kufungua kesi kupinga penati za kuendesha gari kwa spidi. Hiki ni kitu kidogo sana ukilinganisha na haki za kikatiba.

Unapokwenda kutumia mechanisms za kuripoti kiongozi, unategemea polisi, wakili wa serikali na vyombo vingine vikutendee haki. Lakini mara kwa mara kutokana na sababu nyingi nyombo hivyo vinashindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi. Kwa mfano vyombo hivyo vinaweza kuwa havina bajeti au nia ya kufanya uchunguzi wa malalamiko. Je inabidi wananchi wabaki kuwa at mercy of the government? Hapana. Hivyo katika masuala ya katiba, tuachie wananchi waweze kutumia resources zao kutafuta haki.

Chukua mfano wa uraia wa Jenerali Ulimwengu alikuwa mbunge na waziri mdogo. Alitumia haki zote za kiraia hakiwa sio raia watanzania. Na kuna watanzania waliofahamu kuwa hakuwa raia.

Kutokana na yeye kuwa na ukaribu na viongozi wa juu wa serikali, je kulikuwa na uwezekano wa mtu wa kawaida kumripoti kwenye hizo mechanisms unazotaja na kupata haki zake za kiraia? Ni pale alipoanza kushambulia hivyo hizo mechanisms ndipo suala lake la uraia lilipozungumzwa.

Tukirudi kwenye mada, kwa maoni yangu binafsi mtanzania yoyote mwenye haki za kikatiba awe na uwezo wa kupinga matokeo ya uchaguzi katika jimbo lolote lile bila kujali wapi amejiandikisha. Nature ya malalamiko yake ndio yaangalie kama yeye ni locus standi na sio kadi ya kupiga kura.
 
Zakumi,

I know lakini kabla ya kufungua kesi mahakamani huwa wanashauri kujaribu kwanza kutumia njia nyingine kutatua tatizo, ikishindikana then unaweza kuchukua hatua za kisheria. Sijui hii inaweza kutumika vipi kwenye masuala ya chaguzi lakini nafikiri kuna mechanisms za kufanya hivyo. At the end of the day ni uamuzi wa mlalamikaji mwenyewe.

Kuhusu kila mtu kuwa na uwezo wa kupinga matokeo katika jimbo lolote bila kujali ni wapi amejiandikisha, well itategemeana na sababu za kufungua kesi yenyewe. Itategemea aliyeshinda alifanya kosa gani. Sidhani kama wanaoshtaki walioshinda uchaguzi wanafanya hivyo based on the same reasons. Each case varies and should be decided on its own circumstances.

You may be right to argue that standing in challenges to the outcome of elections should be granted as widely as possible. However, kama hakuna safeguards za hiyo right it is likely to be abused. Kwa mfano, kuna mtu ameghusia kuwa kama kila mpiga kura akiruhusiwa kufungua kesi basi awe anaweka security for costs mahakamani. Vingenevyo kuna watu watawafungulia wabunge kesi ambazo they are unlikely to be successful halafu wakishindwa kesi hawawezi kulipa hata gharama za kesi.

Of course, irregularities in elections should not be regarded as a private wrong which an individual must come forward to remedy, but as attempts to wreck the machinery of representative government and as an attack upon national institutions which the nation should concern itself to repel.

On one hand, tunaweza kusema kuwa there is an important public interest in clarifying the legitimacy of the ballot. Therefore, given the clear public interest, it seems appropriate to place the burden to initiate petitions solely on individuals.

However, the election petition brought by a voter is both inadequate and inappropriate as a method of controlling fraud, corruption and irregularities in elections. For electoral policy to be policed by what are, in effect private civil law actions brought at the expense of the litigant (plaintiff) cannot be acceptable.

If there is a public interest, then the relevant authorities should take over badala ya kumbebesha mzigo mtu mmoja. Kwa mfano, hao waliomshitaki Lema watalipaje hizo milioni 400 kama gharama za kuendesha kesi? Wewe unaona ni fair kabisa kwa mtu binafsi kufungua kesi ya public interest halafu anaishia kulipa gharama zote hizo? Is it worth?

On the other hand, the essential features and structure our law has not developed and so election petitions should still remain a private matter.
 
Ronn M Katika hoja za rufani za Lema imo khoja ya kuomba mahakama itathmini ushahidi wa video ambao mahakama kuu iliupuuza na haikuutumia katika maamuzi yake...............Mahakama ya Rufaa inayo mamlaka ya kutathmini ushahidi na hata kuagiza ushahidi uchukuliwe upya.

Mahakama ya Rufaa kosa lao kubwa kuliko yote ni kusema ya kuwa hii kesi haina masilahi kwa umma wakati hata ushahidi uliomo kwenye video hawakuuchunguza! Mahitimisho yao juu ya hii kesi kuwa haina masilahi kwa umma hayana msingi wowote ule wa kisheria

Ndugu, hapa ndipo ninaona unakosea. Nitafafanua

1) Kwanza hoja unayoshikilia ni kwamba ushahidi wa CD ambao Lema aliiomba mahakama iichunguze mahakama haikufanya hivyo. Bila shaka kama Lema alitaka ushahidi wa CD hiyo upitiwe maana yake alikuwa na uhakika kuwa hakusema yale washtaki wake walikuwa wamemshutumu. Kwa vyovyote vile, iwe kwa faida ya Lema, ama washtaki wake, usikilizaji wa ushahidi huo usingeathiri kwa vyovyote vile haki ya mpiga kura ambayo ndio hoja yako.

2) Pili, kama umenifuatilia vyema toka awali kuna mambo ambayo kama mahakama ikijiridhisha nayo, haihitaji tena kuingia katika undani wa hoja zilizowasilishwa. Mathalani, nilitoa mfano kuwa kama mahakama ikigundua na kuthibitisha kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi fulani, haitaendelea kujishughulisha na hoja zilizowekwa mbele zake hata kama ni nzuri kiasi gani. Katika kesi hili swala la kwamba waliofungua kesi hii walikuwa na haki hiyo lilikuwa ni la muhimu ili ama kuendelea au kutokuendelea. Mahakama inapojiridhisha kuwa hawakuwa na haki hiyo, haiwezi kuendelea na hoja nyingine. Ni hivi, A amempiga B. C hawezi kwenda kushtaki kuwa A amempiga B hata kama anao ushahidi wa moja kwa moja. Mahakama ikiridhika kuwa C hakuvunjiwa haki yeyote, haiwezi kuendelea kusikiliza ushahidi.

3) Swala la kwamba kesi ile ilikuwa na maslahi kwa umma (public interest) halikuwa na nguvu ya kuamua suala lile. Ili mtu aweze kufungua kesi ambayo yeye haimuhusu au hajadhurika, lakini yenye maslahi ya umma lazima atumie Ibara ya 26(2) pamoja na Basic Rights and Duties Enforcement Act ya mwaka 1994. Sasa hawa hawakufungua kesi hii kama shauri la kikatiba badala yake wamefungua kama shauri la uchanguzi chini ya sheria ya uchaguzi. Waheshimiwa majaji walejielekeza katika hoja hii katika kuthibitisha kuwa wale mabwana hawakuwa na locus stand. Kwamba chini ya sheria ya uchaguzi hawakuwa na locus stand na hata kama wangetumia Ibara ya 26(2) kama shauri la kikatiba bado wasingefanikiwa kwa sababu jambo hilo siyo la public interest.

Hivyo,

Hoja pekee ambayo tunapaswa kuijadili kisheria ni kama hawakuwa na locus stand! Sasa ukisoma sheria ya uchaguzi inaonesha mtu yeyote aliyepiga kura au aliyekuwa na haki ya kupiga kura anaweza kufungua shauri la kipinga matokea ya ubunge. Mahakama ndio imepewa mamlaka ya kutafsiri sheria. Kama tukisema kila mtu anaweza kufungua kesi, this will be an abuse of court process. Na kama ikitafsiriwa hivyo it will be real absurd. Ndio maana majaji wakaamua kuitafsiri sheria hii taking into account general doctrine of locus stand. Mimi kwa upande wake naweza kwenda mbali kidogo.Kitendo cha sheria kuruhusu mtu aliyepiga kura au aliyestahili kupiga kura kufungua shauri la uchaguzi kinanifanya nione kuwa ni lazima mtu huyo awe ameathirika na uchaguzi huo. Hebu tujiulize, ni kwanini mtu ambaye alistahili kupiga kura lakini hakupiga kura aruhusiwe kufungua mashtaka? Lazima mtu huyu haki yake iwe imeathiriwa, mathalani alizuiwa kupiga kura isivyo halali. Linapokuja swala la lugha chafu, hapo lazima mtu yule aliyefanyiwa hivyo afungue mashtaki. Labda tujiulize, kwanini sheria impe haki ya kufungua kesi mtu yeyote hata kama alipiga kura na aliyempigia kashinda? Hatuoni kama tukitafsiri sheria namna hii wapenzi wa vyama vinavyoshindwa kesi watakuwa wanajiendea tuu mahakamani kushtaki hivyo kupoteza muda wa yule aliyeshinda? Naungana na majaji wa mahakama ya rufaa kwamba bunge halikukusudia hivyo. Mara nyingi hukumu za mahakama za rufaa huwa zina utata. Its more of a political court so to speak. But in this case, they have made it, at least to my understanding. Copy to Mzee Mwanakijiji aliyeuliza swali sehemu fulani.
 
I am not a lawyer or an expert in legal procedures. Lakini naelewa kuwa legal systems nyingi duniani zinatumia alama ya mizani kuonyesha haki na uwiano. So it's a mockery of our legal system iwapo tutawambia walalamikaji walipe zaidi ya gharama ya kile kilichotumika? Wawikili wa Lema anaweza kuomba fidia ya milioni 400, lakini Jaji asitoe hukumu ya kukubali kiwango hicho kwa sababu hakuna vigezo vyovyote vile vya kufanya walalamikaji kulipa shillingi milioni 400.

Pili kiwango hicho cha pesa kinaonyesha umuhimu wa kutotumia uandkishaji wa wapiga kura katika jimbo husika kama kigezo cha kufungua mashtaka. Kupunguza gharama, entities kama vyama vya siasa au vya kutetea haki viwe vinafungua kesi kwa niaba ya wapiga kura na watu kuvichangia vyama hivyo. Hiyo inapunguza gharama na vilevile kuondoa financial liabilities ambazo zinaweza kutokea baada ya kesi.

Legal system itaendelea sio kwa wabunge kupitisha sheria na kuwepo kwa mahakama. Itaendelea kwa watu kuwa na interests na haki ya kutumia mahakama.

Kwa kumalizia ningependa kuuliza ni nani ana mamlaka ya kuuliza uteuzi wa mbunge wa kuteuliwa? Mwanachama wa chama?
 
Kama Lema anaweza kujustify kuwa aliingia gharama ya milioni 400, then sijui kwa nini mahakama imkatalie. May be he hired the most expensive lawyers in the country. Pia na appeal kusikilizwa Dar imeongezea gharama.

Kumbuka anaweza pia kuwadai walalamikaji fidia ya posho na malipo mengine ambayo angestahili kulipwa kama angekuwa bungeni. Loss of earnings. Halafu bado hujaongeza interests hapo. Ndiyo maana siungi mkono wapiga kura kushtaki. Ni wachache sana wataweza na watakaoweza itawawia vigumu sana kushinda kesi due to limited resources and knowledge.

Kwenye nchi nyingine kama Ningeria mgombea au chama chake ndicho kinaweza kumshtaki mgombea aliyeshinda. Wapiga kura wa kawaida hawaruhusiwi. Ni bora vyama vya siasa viruhusiwe kushtaki badala ya wapiga kura. Exceptionally, mpiga kura wa kaiwaida aruhusiwe kushtaki tuu pale ambapo mgombea amepita bila kupingwa kama Waheshimiwa Mizengo Pinda au January Makamba.

Kwa haraka haraka nadhani kila raia anayo haki chini ya Ibara ya 26(2) unless litigation dhidi ya mbunge wa kuteuliwa is also not a public interest litigation. lol.
 
Wakuu wasomi Ronn M na EMT nawashukuruni sana kwa kuniongezea uelewa fulani wa sheria.

Nimeshiba na ahsanteni sana.

Mbarikiwe na muwe na usiku mwema.
 
Last edited by a moderator:
Kama Lema anaweza kujustify kuwa aliingia gharama ya milioni 400, then sijui kwa nini mahakama imkatalie. May be he hired the most expensive lawyers in the country. Pia na appeal kusikilizwa Dar imeongezea gharama.

Kumbuka anaweza pia kuwadai walalamikaji fidia ya posho na malipo mengine ambayo angestahili kulipwa kama angekuwa bungeni. Loss of earnings. Halafu bado hujaongeza interests hapo. Ndiyo maana siungi mkono wapiga kura kushtaki. Ni wachache sana wataweza na watakaoweza itawawia vigumu sana kushinda kesi due to limited resources and knowledge.

Kwenye nchi nyingine kama Ningeria mgombea au chama chake ndicho kinaweza kumshtaki mgombea aliyeshinda. Wapiga kura wa kawaida hawaruhusiwi. Ni bora vyama vya siasa viruhusiwe kushtaki badala ya wapiga kura. Exceptionally, mpiga kura wa kaiwaida aruhusiwe kushtaki tuu pale ambapo mgombea amepita bila kupingwa kama Waheshimiwa Mizengo Pinda au January Makamba.

Kwa haraka haraka nadhani kila raia anayo haki chini ya Ibara ya 26(2) unless litigation dhidi ya mbunge wa kuteuliwa is also not a public interest litigation. lol.

EMT;

Kwenye nyekundu, ni majibu yanayoturudisha katika maswali ya awali kuhusu raia wa Tanzania ambae anaishi jimbo jingine la uchaguzi kufungua mashtaka.

Mbunge wa kuteuliwa au wa taifa ana haki na sifa zote kama mbunge wa kuchaguliwa na wananchi katika jimbo. Kama raia yoyote anaweza kufungua mashtaka kupinga uteuzi wa mbunge wa kuteuliwa, kinadharia anayo haki ya kupinga kuchaguliwa kwa mbunge yoyote wa mbunge la jamuhuri.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
quote_icon.png
By Rutashubanyuma

Ronn M Katika hoja za rufani za Lema imo khoja ya kuomba mahakama itathmini ushahidi wa video ambao mahakama kuu iliupuuza na haikuutumia katika maamuzi yake...............Mahakama ya Rufaa inayo mamlaka ya kutathmini ushahidi na hata kuagiza ushahidi uchukuliwe upya.

Mahakama ya Rufaa kosa lao kubwa kuliko yote ni kusema ya kuwa hii kesi haina masilahi kwa umma wakati hata ushahidi uliomo kwenye video hawakuuchunguza! Mahitimisho yao juu ya hii kesi kuwa haina masilahi kwa umma hayana msingi wowote ule wa kisheria
Ndugu, hapa ndipo ninaona unakosea. Nitafafanua

1) Kwanza hoja unayoshikilia ni kwamba ushahidi wa CD ambao Lema aliiomba mahakama iichunguze mahakama haikufanya hivyo. Bila shaka kama Lema alitaka ushahidi wa CD hiyo upitiwe maana yake alikuwa na uhakika kuwa hakusema yale washtaki wake walikuwa wamemshutumu. Kwa vyovyote vile, iwe kwa faida ya Lema, ama washtaki wake, usikilizaji wa ushahidi huo usingeathiri kwa vyovyote vile haki ya mpiga kura ambayo ndio hoja yako.

2) Pili, kama umenifuatilia vyema toka awali kuna mambo ambayo kama mahakama ikijiridhisha nayo, haihitaji tena kuingia katika undani wa hoja zilizowasilishwa. Mathalani, nilitoa mfano kuwa kama mahakama ikigundua na kuthibitisha kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi fulani, haitaendelea kujishughulisha na hoja zilizowekwa mbele zake hata kama ni nzuri kiasi gani. Katika kesi hili swala la kwamba waliofungua kesi hii walikuwa na haki hiyo lilikuwa ni la muhimu ili ama kuendelea au kutokuendelea. Mahakama inapojiridhisha kuwa hawakuwa na haki hiyo, haiwezi kuendelea na hoja nyingine. Ni hivi, A amempiga B. C hawezi kwenda kushtaki kuwa A amempiga B hata kama anao ushahidi wa moja kwa moja. Mahakama ikiridhika kuwa C hakuvunjiwa haki yeyote, haiwezi kuendelea kusikiliza ushahidi.

3) Swala la kwamba kesi ile ilikuwa na maslahi kwa umma (public interest) halikuwa na nguvu ya kuamua suala lile. Ili mtu aweze kufungua kesi ambayo yeye haimuhusu au hajadhurika, lakini yenye maslahi ya umma lazima atumie Ibara ya 26(2) pamoja na Basic Rights and Duties Enforcement Act ya mwaka 1994. Sasa hawa hawakufungua kesi hii kama shauri la kikatiba badala yake wamefungua kama shauri la uchanguzi chini ya sheria ya uchaguzi. Waheshimiwa majaji walejielekeza katika hoja hii katika kuthibitisha kuwa wale mabwana hawakuwa na locus stand. Kwamba chini ya sheria ya uchaguzi hawakuwa na locus stand na hata kama wangetumia Ibara ya 26(2) kama shauri la kikatiba bado wasingefanikiwa kwa sababu jambo hilo siyo la public interest.

Hivyo,

Hoja pekee ambayo tunapaswa kuijadili kisheria ni kama hawakuwa na locus stand! Sasa ukisoma sheria ya uchaguzi inaonesha mtu yeyote aliyepiga kura au aliyekuwa na haki ya kupiga kura anaweza kufungua shauri la kipinga matokea ya ubunge. Mahakama ndio imepewa mamlaka ya kutafsiri sheria. Kama tukisema kila mtu anaweza kufungua kesi, this will be an abuse of court process. Na kama ikitafsiriwa hivyo it will be real absurd. Ndio maana majaji wakaamua kuitafsiri sheria hii taking into account general doctrine of locus stand. Mimi kwa upande wake naweza kwenda mbali kidogo.Kitendo cha sheria kuruhusu mtu aliyepiga kura au aliyestahili kupiga kura kufungua shauri la uchaguzi kinanifanya nione kuwa ni lazima mtu huyo awe ameathirika na uchaguzi huo. Hebu tujiulize, ni kwanini mtu ambaye alistahili kupiga kura lakini hakupiga kura aruhusiwe kufungua mashtaka? Lazima mtu huyu haki yake iwe imeathiriwa, mathalani alizuiwa kupiga kura isivyo halali. Linapokuja swala la lugha chafu, hapo lazima mtu yule aliyefanyiwa hivyo afungue mashtaki. Labda tujiulize, kwanini sheria impe haki ya kufungua kesi mtu yeyote hata kama alipiga kura na aliyempigia kashinda? Hatuoni kama tukitafsiri sheria namna hii wapenzi wa vyama vinavyoshindwa kesi watakuwa wanajiendea tuu mahakamani kushtaki hivyo kupoteza muda wa yule aliyeshinda? Naungana na majaji wa mahakama ya rufaa kwamba bunge halikukusudia hivyo. Mara nyingi hukumu za mahakama za rufaa huwa zina utata. Its more of a political court so to speak. But in this case, they have made it, at least to my understanding. Copy to Mzee Mwanakijiji aliyeuliza swali sehemu fulani.
Last edited by Ronn M; Yesterday at 23:31.​

Ronn M tatizo lako ni kuiona mahakama ya rufaa kama Mwenyezi Mungu........ na ndiyo maana unatetea hoja zao hata kama zina walakini........................kifupi tu mahakama hiyo haikuwa na ubavu wa kisheria kutengua haki ya wapinga marejeo kuwa wapigakura halali wa jimbo la Arusha bila ya kuwapatia nafasi ya kubeza hoja za kuwavua haki tajwa....................................huu ni ukiukwaji wa haki ya asili uliofanywa na mahakama ya rufaa................

Mahakama ya Rufaa ilibanwa na sheria ya uchaguzi kuchunguza videos na kwa kutofanya hivyo haikuwa na mamlaka ya kisheria kudai na kuamua kesi hiyo haikuwa na masilahi kwa taifa kwa sababu ni video tu ambazo zingeliwaongoza pale..................

Siyo lazima ufungue kesi ya kikatiba wakati sheria za kawaida zipo na zinakulinda...................teteeni dhuluma lakini dhuluma haibagui kesho itakuwa zamu yako kudhulumiwa na hapo ndipo utajua nini maana ya usemi usemao....................."Ukiona ananyolewa wewe tia maji kichwa chako........"
 
Mkuu can I step in? I strongly believe that you opened this thread so we can share our opinions which may not necessarily reflect yours.

Kwa hiyo, sidhani kama ni vyema kusema kuwa kwa vile mtu amekubaliana na hukumu ya mahakama basi anaiona mahakama kama Mwenyezi Mungu.

I think that is wrong. When you respect others, you respect yourself. We should respect the opinions of others even if we disagree with them.

Respecting others' opinions is part of a larger attitude of respect - respect for the whole person that we are expected to develop as we grow up.

Of course, respect for opinions is not an easy art at all. It requires self-esteem, self-control, sensitivity, tolerance, fairness, and generosity. And it applies both to stated opinions and to opinions that are unspoken.

Respecting others' opinions does not mean being untrue to our own. It simply requires us to recognize that others are entitled to look at issues differently and that when they share their views with us, they can expect a fair hearing.

What we believe is an integral part of who we are. Therefore, we tend to perceive criticism directed at our opinions as rejection. When that happens, defensiveness and resentment can put an end to dialog.

The decision of the Court of Appeal in Lema is controversial and has attracted conflicting opinions even in the legal field. So, lets respect each other's opinion to avoid putting this interesting debate to an end.

After all this thread is in the Great Thinkers Forum. We need to lead by examples here.
 
Kama Lema anaweza kujustify kuwa aliingia gharama ya milioni 400, then sijui kwa nini mahakama imkatalie. May be he hired the most expensive lawyers in the country. Pia na appeal kusikilizwa Dar imeongezea gharama.

EMT malipo ya fidia za gharama za kesi zinaongozwa na sheria yake na lipo jedwali na gharama zake ziko chini ili kuhahaklisha haki isiwe ni ya wenye nazo tu......Lema anazidi kuuthibitishia umma jinsi alivyo mbumbu mbu wa sheria fidia yake anayostahili haiwezi kuvuka milioni tano kulingana na jedwali tajwa............na ndiyo maana kwenye sheria ya uchaguzi hudai walalamikaji kuweka hicho kiwango kabla kesi haijaanza........
 
Unaweza kutupa breakdown of what is and is not included kwenye fidia ya gharama za kesi za uchaguzi?
 
Mkuu can I step in? I strongly believe that you opened this thread so we can share our opinions which may not necessarily reflect yours.

Kwa hiyo, sidhani kama ni vyema kusema kuwa kwa vile mtu amekubaliana na hukumu ya mahakama basi anaiona mahakama kama Mwenyezi Mungu.

I think that is wrong. When you respect others, you respect yourself. We should respect the opinions of others even if we disagree with them.

Respecting others' opinions is part of a larger attitude of respect - respect for the whole person that we are expected to develop as we grow up.

Of course, respect for opinions is not an easy art at all. It requires self-esteem, self-control, sensitivity, tolerance, fairness, and generosity. And it applies both to stated opinions and to opinions that are unspoken.

Respecting others' opinions does not mean being untrue to our own. It simply requires us to recognize that others are entitled to look at issues differently and that when they share their views with us, they can expect a fair hearing.

What we believe is an integral part of who we are. Therefore, we tend to perceive criticism directed at our opinions as rejection. When that happens, defensiveness and resentment can put an end to dialog.

The decision of the Court of Appeal in Lema is controversial and has attracted conflicting opinions even in the legal field. So, lets respect each other's opinion to avoid putting this interesting debate to an end.

EMT unaposhindwa kujibu khoja za kimsingi unafikiri nitakuonaje? Mahakama ya Rufaa haikuwa na mamlaka ya kukataa kuwatambua wapinga rufani kama wapigakura halali wa jimbo la Arusha bila ya kuwapatia nafasi ya kuwauliza juu ya mapungufu ambayo wao waliyaibua..............................na hiyo ndiyo msingi wa kutoa haki. Sasa ukisema Mahakama ya Rufaa hutoa maamuzi waonavo tu na hata kama wanabeza sheria za msingi kama rules of natural justice........................

Mengineyo uliyaongea naona ni blah-blah tu yako nje ya khoja sanasana unagusa hisia zako ambazo mimi naona hazinhusu..........................Nakushauri utafute na ulisome Mwananchi la leo.........................utaona khoja zangu zinaungwa mkono na Profesa Shivji lenye kichwa cha khabari "Mengi yaibuka hukumu ya Lema."
 
Unaweza kutupa breakdown of what is and is not included kwenye fidia ya gharama za kesi za uchaguzi?

EMT sasa unanipa kazi ambayo iko nje ya mada. La msingi tafuta jedwali la Mahakama ya RUfaa leny kuonyesha viwango vya malipo............................kwa mfano gharma zinazoruhusiwa ni pamoja na kuandika majibizano zipo ankara zake, gharama za usafiri na malazi...........kulinga na public transport, etc etc.........
 
Last edited by a moderator:
[h=1]Hukumu kesi ya Lema yaibua mapya[/h]
ico_plus.png
Share
ico_bookmark.png
bookmark
ico_print.png
Print
ico_email.png
Email Rating
glema.jpg
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema
Na James Magai (email the author)

Posted Ijumaa,Decemba28 2012 saa 24:17 AM
Kwa ufupi

Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama Kuu Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Walalamikaji walishinda.

SHARE THIS STORY

0
inShare​

MWANAZUONI aliyebobea katika sheria, Profesa Issa Shivji na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stolla wamekosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, wanasheria hao walisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu wakiongozwa na Nathalia Kimaro, Salum Massati na Bernard Luanda, inapingana na sheria.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa Lema, Method Kimomogoro amepinga madai hayo akisema wanaoipinga pengine hawajapata nafasi ya kuliangalia kwa undani suala la haki ya mpiga kura kupinga matokeo mahakamani.

Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
Alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi, Katiba ya nchi na Mahakama, vinampa haki mpiga kura kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi.

"Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura," alisema Profesa Shivji.

Katika shauri hilo namba 84 la mwaka 1980 lililofunguliwa na William Bakari na mwenzake dhidi ya Mgonja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mahakama Kuu Tanzania iliamua kuwa, mpiga kura ana haki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Walalamikaji walishinda.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani katika kesi ya Lema, iliamua kwamba hukumu katika kesi ya Mgonja ilikosewa kwani si sahihi kwamba mtu yeyote bila kujali mahali alipojiandikisha na kupiga kura anaweza kupinga matokeo katika jimbo lolote nchini hata kama haki zake hazijakiukwa kwa namna yoyote.

Lakini Profesa Shivji aliitetea hukumu hiyo ya Mgonja akisema imekuwapo kwa zaidi ya miaka 30 sasa na kwamba kwa muda wote huo imekuwa ikifuatwa katika uamuzi wa mashauri mbalimbali, huku akisisitiza kuwa Mahakama haiwezi kuifuta kirahisi tu.

Profesa Shivji alisema mpiga kura ni mwananchi na kwa vyovyote ana masilahi katika uchaguzi husika na hivyo anatarajia kuona uchaguzi ambao ni huru na wa haki.
"Hivyo huwezi kusema hahusiki na nani kashinda au kashindwa kwa kuwa uchaguzi ni muhimu katika kujenga na kukuza demokrasia," alisema Profesa Shivji.

Chama cha Wanasheria
Kwa upande wake, Stolla alisema: "Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutofurahishwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge' (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani," alisema na kuongeza:
"Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, sababu ya kuwa mpiga kura ni ipi nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?"

Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

"Mwaka 2002, sheria zote zilifanyiwa marekebisho na baadaye mwaka 2005, Bunge likatunga sheria mpya inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ikafuta ya mwaka 1985. Sheria hiyo na marekebisho yake, ndiyo inayotawala uchaguzi hadi sasa," alisema.

Alisema hata kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo ya Uchaguzi ya mwaka 1985, tayari kulikuwa na uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja ambayo iliamua kuwa mpiga kura ana haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

"Uamuzi wa kesi ya Mgonja ulikuja ‘ku-reflect' (kuakisi) hata kwenye Sheria ya Bunge ya mwaka 1985. Tangu hukumu hiyo ya Mgonja hakuna uamuzi mwingine wa Mahakama ambao umeshautengua huo, ndiyo maana hata wanasheria wanashangaa uamuzi huu wa Mahakama ya Rufani," alisema.

Alisema kumekuwa na kesi nyingi mahakamani za wapiga kura kupinga matokeo na kwamba nyingine hata yeye amezisimamia na hakuna wakati ambao Mahakama imewahi kusema kuwa hawana haki hiyo.

Alitoa mfano wa kesi iliyofunguliwa na wapiga kura dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Mbulu, Phillip Marmo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Alisema kesi hiyo ilishindwa kuendelea kutokana na wapiga kura hao kushindwa kuweka mahakamani fedha ya amana kwa ajili ya kuiendesha na si kwa sababu hawakuwa na haki.

Akizungumzia hoja ya Mahakama ya Rufani kuwa hapakuwa na ushahidi kama walalamikaji walikuwa wapiga kura, Stolla alisema hilo halikuwa na ulazima kwa kuwa halikuwa jambo lililokuwa likibishaniwa.

"Hata hivyo, kabla ya kuanza kesi Mahakama Kuu, Jaji Mujulizi (Aloyce) aliitisha vithibitisho ili kujiridhisha kama ni wapiga kura," alisema Stolla na kuongeza:
"Lakini Mahakama ya Rufani wenyewe walianza kutafuta kama liliibuka Mahakama Kuu na licha ya Mahakama Kuu kuonyesha kuwa ilijiridhisha katika hilo, wao wakakosoa kuwa uthibitisho huo ulipaswa uwe sehemu ya mwenendo."

Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.

Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.

Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.

Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake.

Mugway ashangaa
Wakili Alute Mughway aliyekuwa akiwatetea wajibu rufaa katika rufaa hiyo, alisema Mahakama imeacha jukumu lake la kutafsiri sheria na badala yake ikatunga sheria mpya ambayo inapingana na Sheria ya Bunge na Katiba ya nchi, Ibara ya 26 (2).

Alisema Kifungu cha 111 (1) cha Sheria ya Uchaguzi, Hukumu ya kesi ya Mgonja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinampa haki mpiga kura kufungua shauri mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.

Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, miongoni mwa watu wanaoweza kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi ni aliyepiga kura au aliyekuwa na haki ya kupiga kura na kwamba tangu wakati huo kifungu hicho hakijawahi kufanyiwa marekebisho.

Wakili wa kujitegemea, Vedasto Audax alikaririwa na gazeti dada la The Citizen akisema: "Swali langu ni kwamba ni lini uamuzi wa kesi ya Mgonja ulionekana kuwa na makosa kisheria? Ni kuanzia leo baada ya Mahakama ya Rufani kutamka kuwa una makosa?"

Wakili wa Lema
Kimomogoro alisema hukumu ya kesi ya Mgonja haijitoleshelezi kwa sababu haikusema ni katika mambo gani mpiga kura ana haki ya kufungua kesi kupinga matokeo mahakamani huku akisema kwa maoni yake, anakuwa na haki pale tu haki zake kama mpiga kura zinapokiukwa.

"Mpiga kura hawezi kuwa na haki sawa na mgombea. Mgombea haki zake ni kubwa kuliko mpiga kura kwa sababu kwanza yeye ni mpiga kura na pili ni mgombea," alisema na kuongeza:

"Ndiyo maana mpiga kura anaruhusiwa kupiga kura katika kituo kile alichojiandikisha tu lakini mgombea huweza kupiga kura katika kituo chochote."

Alisema mwananchi wa kawaida tu ambaye hajajiandikisha hata kama akimwona mgombea akitoa rushwa hadharani, hana haki ya kufungua kesi mahakamani, lakini alipoulizwa kwa upande wa mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura alisema hakuwa na rejea za sheria kwa kuwa alikuwa Karagwe kwa mapumziko.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Buriani.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Lema alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kuikubali.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.
"Hivyo mpiga kura hana haki ya kisheria kufungua kesi kuhoji matokeo ya uchaguzi pale ambapo haki zake hazikukiukwa," ilisema Mahakama ya Rufani.

Ilisema kwa mujibu wa Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Tanzania, raia anakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi kwa masilahi ya jamii, kama ilivyotokea katika kesi ya Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa SerikaIi ya mwaka 1995.

Ilisema kesi dhidi ya Lema haikufunguliwa chini ya Ibara ya 26 (2) ambayo inampa fursa na haki raia yeyote kufungua shauri mahakamani lenye masilahi ya umma, huku ikisisitiza kuwa madai ya wajibu rufani katika kesi hiyo hayagusi masilahi ya jamii yote.
 
Back
Top Bottom