Kushinda 4:3 nyumbani ndio umachachari huo?
halafu ugenini tunaenda kula 3:1 ndo umachachari huo? ndio kumuwashia moto madrid hivyo?
group stage pekee tunaruhusu goli 10 ndani ya mechi 6 ndio umachachari huo?
Kwenye uefa haijalishi unafunga vp, kama nawew unafungwa ni mbovu tu, city ya msimu uliopita unayoiita machachali kwenye uefa ilikuwa mbovu mno, inafunga magoli meeengi huku na yenyewe inafungwa za kutosha.
We unaangalia ubora wa timu kwa kufunga magoli mengi pekeake? Hiyo sio epl bro ya 'cha muhim point tatu'.
City kushinda kwa leipzig leo hakuna maajabu yoyote, maajabu ni leipzig kushinda.
Team yetu Kwa Sasa Haina uwezo wa kupata hata goli 4 mbele ya Madrid....
Kutolewa mwaka Jana semi final na madridi mim nahesabu kama bad lucky kwetu ,maana Hadi dakika ya 90 tulikuwa na 2-0 ,yale magoli mawili ya Rodrigo ndio yalitumaliza ...
Kusema ukweli Kwa sasa hatuna team ya CL tuache kujipa matumain hewa ,mfano nitajie ni nan solid defence yetu ambayo ni uhakika kutulinda kwenye CL ,vip midifilder,vip winger ....
Mwaka Jana bernado alikuwa false nine mkali Sana ,foden alikuwa sio mchezo , Mahrez alikuwa ndio our hero ,walker alikuwa jiwe ,cancelo na mipass yake ilikuwa balaaa,zinchenko moto ulikuwa mkali ,Jesus , sterling walikuwa hatari huyo grealish tunaemtegemea Leo alikuwa anasugua bench ,kdb alikuwa sio wa Leo ,maana anaanza hata bench ....
Saizi tunamtegemea ake kama solid defender maana stone ,akanji ,Laporte ,dias wote hawaeleweki ni tia maji tia maji ,...
Usione pep anafanya rotation ukafikili anapenda hapana ukweli ni kuwa wachezaji ndio viwango vinapanda na kushuka ...
Mfano Leo nilikuambia nitajie first eleven ya Leo ? Unaweza ...
Lakin mwaka Jana ulikuwa unajua kabisa cancelo ---laporte -- dias --- walker ,,,,,hiyo back line ilikuwa solid mpaka walker wakasema anamsimamisha mbappe ,tupo group stage na psg na tunamuwashia moto ...
Leo unakuja na back line ya kina akanji --stone -- ake ,,,,....harafu et unataka CL .....
Kiufupi mim nasubili miujiza kufika hata semi final CL ....