Adipoz
JF-Expert Member
- Jan 24, 2023
- 527
- 459
Kimahesabu hii game arsenal anaitaka zaidi kuliko tunavyoitaka sisi.Usiku wa deni haukawii, wavulana wa arteta leo watakuja kujaribu kufufua matumaini yao ya kuchukua ubingwa wa EPL.
Wanakuja kukutana na wanaume wababe wa hizi kazi na mabingwa watetezi, the Cityzens ambao wana kiu ya kutetea taji kwa mara ya tatu mfululizo.
NB: Etihad kila goti litapigwa na hii haitokiukwa.
Leo watakuja kutafuta ushindi tu, watakuwa aggressive sana ila defence yetu kwasasa iko settled naamin itahimili pressure ya arsenal.
Tunahitaji kuwa clinical kutumia nafasi tunazopata kama tulivyofanya game iliyopita maana kuna uwezekano mkubwa sana arsenal watautawala mchezo.