The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Doku yupo vizuri ana kipaji ila hana uzoefu. Laiti angekuwa na uzoefu mancity wangeongoza sasa hivi 4-1 kwasababu upande wake mbele kushoto alikuwa ana nafasi ya kupiga pasi nakuvungua njia ya magoli.

Naona Pep taratibu anaacha UBAGUZI.

Senior JF accredited sports analysist and correspondent
 
Spurs wametushinda aisee
IMG-20231203-WA0083.jpg
 
[emoji1593]Ange Postecoglou kabla ya mechi kwenye press alisema kwamba anaweza kufungwa na Man City lakini itakuwa burudani. Kweli nimeshuhudia burudani

[emoji1593]Ange alishasema hatobadilisha staili yake ya uchezaji hata wawe 7 uwanjani , bila kujalia mpinzani na bila kujali uwanja gani . Kuna risk zake lakini bila risk hupati mafanikio.

1: Spurs kwenye muundo wa 2-3-2-2 wakiwa na mali leo dhumuni lake ilikuwa ...

2: Kuwavuta City kufanya pressing ili kufungua space juu kwa namba 8 wao wawili nyuma ya Rodri na kuna nyakati nyingi walifanikiwa

3: Emerson na Davies nyuma mbele yao mabeki wawili wa pembeni wanaingia ndani inakuwa Porro Bissouma na Udogie kwenye mstari mmoja namba 8 wawili walianza Lo Celso na Kulusevski na mbele Bryan Gil Son na Jonhson .

[emoji1593]Man City pressing yao ilikuwa nzuri ambayo kuna nyakati kadhaa iliwalazimisha Spurs kutupa mpira au kuporwa kabisa : Man to Man Pressing ambayo ilikuwa ya watu watano dhidi ya watano wa Spurs waliokuwa wanahusika kwenye build up

[emoji1593]Shida kwa Man City ilikuwa ule muundo wao wa ulinzi pili Spurs wakiishinda pressing yao , kulikuwa na gap kubwa sana baina ya mstari wao wa ulinzi na kiungo na kwanini ? Kwasababu ya Position ya Heung Son ... Spurs wakifanya build up yeye hashuki chini matokeo yake anasababisha mstari wa ulinzi wa City ubaki chini ... kwahiyo Space inakuwa kubwa between the lines .

NOTE

1: Jeremy Doku kipindi cha kwanza alipata mipira mingi sana lakini ufanisi duni

2: Recovery pace ya Walker ni ya juu sana [emoji91]

3: Rodri ukimtenga peke yake hasa pale unaposhambulia kupitia katikati anapata tabu ( Chelsea na Liverpool walimfanyia hivyo na leo Spurs pia )

4: Haaland anaboresha uwezo wake wa kukaa na mpira [emoji736]

5: Bissouma hana hofu akiwa na mali , risk sana lakini ina faida kubwa kwenye ufanisi wa timu

6: Kulusevski akicheza namba 8 wa kushoto hatari, akicheza winga wa kulia hatari pia .
 
Hii timu sikuizi mbona inazingua sana wakuu shida Nini? Wachezaji wanacheza kama wa Simba.!!
Ni ngumu sana kwa timu yoyote Ile kupata mafanikio aliyoyapata city msimu uliopita na Kisha kuendelea kubaki katika ubora ule ule msimu unaofuata.... Tena Mimi naona hata kuwa hapa city kajitahidi sana. Nilitegemea muda kama huu awe nafasi ya 6 huko
 
Back
Top Bottom