MESSI AMKATAZA AGUERO KUJIUNGA NA REAL MADRID
Lionel Messi amemshauri Mwargentina mwenzake Sergio Aguero kutojiunga na Real Madrid mwaka ujao, kwa mujibu wa Diario Gol .
Rais wa Madrid Florentino Perez amemtaja straika wa Manchester City, Aguero kuwa mchezaji sahihi na anaamini ataweza kumshawishi kujiunga na Blancos ikiwa Pep atamsajili Alexis Sanchez.
Lakini kwa mujibu wa habari Lionel Messi amemtumia ujumbe Aguero kwa njia ya WhatsApp, na amemwambia rafiki yake kipenzi na Mwargentina mwenzake kuwa ni vema abaki Manchester kwa sababu Madrid inaelekea kuporomoka na City wanazidi kuwa tishio chini ya Guardiola kwa sasa.