The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Screenshot_2017-10-28-16-40-10.png

Bernardo Silva AKA kisheti ameanza...
Ingawa Kun Aguero ameanzia benchi,sioni West Bromwich akitoka salama katika game hii..!
Man City will score 2+ goals
 
CITY WAANDAA DAU LA BERTRAND


Manchester City wapo tayari kutoa dau la puandi milioni 30 kwa ajili ya nyota wa Southampton Ryan Bertrand, kwa mujibu wa The Sun .
 
MAN CITY YAMFUKUZIA CAN


Manchester City wapo tayari kuchuana na Juventus kumwajili kiungo wa Liverpool Emre Can, kwa mujibu wa Calcio Mercato .
Mkataba wa Can unafikia kikomo mwisho wa msimu huu, na kutakuwa hakuna ada itakayohitajika kumsajili Mjerumani huyo.
 
MESSI AMKATAZA AGUERO KUJIUNGA NA REAL MADRID


Lionel Messi amemshauri Mwargentina mwenzake Sergio Aguero kutojiunga na Real Madrid mwaka ujao, kwa mujibu wa Diario Gol .
Rais wa Madrid Florentino Perez amemtaja straika wa Manchester City, Aguero kuwa mchezaji sahihi na anaamini ataweza kumshawishi kujiunga na Blancos ikiwa Pep atamsajili Alexis Sanchez.
Lakini kwa mujibu wa habari Lionel Messi amemtumia ujumbe Aguero kwa njia ya WhatsApp, na amemwambia rafiki yake kipenzi na Mwargentina mwenzake kuwa ni vema abaki Manchester kwa sababu Madrid inaelekea kuporomoka na City wanazidi kuwa tishio chini ya Guardiola kwa sasa.
 
MAN CITY & EVERTON ZAMWANIA EVANS


Manchester City na Everton zimejikuta zikipgana vikumbo kuiwania saini ya beki wa West Brom Jonny Evans, The Sun limeripoti.
The Baggies wapo tayari kumuuza nahodha wao lakini ikiwa tu watalipwa kiasi wanachokihitaji cha paundi milioni 35.
 
Back
Top Bottom