The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Japo mashushushu wekundu walimpiga arsenal ila mpira wao ulikuwa chini sana, arsenal walistahili ushindi kwenye ile mechi. Man U akicheza ule mpira aliocheza na arsenal juzi, Basi pont 3 kwa City mapema sana.
José Mourinho ni mkali sana wa kuweka defence, anaakili sana kwenye kutengeneza matokeo, Ila squad ya Mancity inatisha mkuu.
Kheli man city ashinde sio man u
Siyapendi kbs haya majamaa
Man city!!!!!! Saga kabisa haya j2
 
Ratiba ya raundi ya tatu ya michuano ya kombe la Fa, imetangazwa usiku huu na michezo hiyo itachezwa wikiendi ya januari 6 na 7 mwaka 2018

Majogoo Liverpool wataanza michuano hiyo kwa kuchuana na wapinzani wao wa jadi Everton,huku bingwa mtetezi Arsenal akianzia ugenini kwa kucheza na Nottingham Forest.

Matajiri wa Manchester City wataanzia nyumbani katika dimba la Etihad,kwa kucheza na Burnley nao Manchester United wakiwalika Derby County.

Vijana wa Antonio Conte, Chelsea wataanzia ugenini kwa kucheza na Norwich, Tottenham Hotspur watakua wenyeji wa AFC Wimbledon
 
Asante kwa taarifa
 
Ratiba ya michezo mingine ya raundi ya tatu ya kombe la Fa.

Birmingham City v Burton Albion

Brighton & Hove Albion v Crystal Palace

Coventry City v Stoke City

Bolton Wanderers v Huddersfield Town

Queens Park Rangers v MK Dons

Middlesbrough v Sunderland

Fleetwood or Hereford v Leicester City

Blackburn Rovers or Crewe Alexandra v Hull City

Cardiff City v Mansfield Town

Shrewsbury Town v West Ham United

Wolverhampton Wanderers v Swansea City

Newcastle United v Luton Town

Fulham v Southampton
 
Kiungo wa Manchester City Kevin De Bruyne amepuuzia umuhimu wa ushindi wa Manchester City dhidi ya Manchester United Jumamosi
Kikosi cha Pep Guardiola kina fursa ya kuongoza kwa pointi 11 dhidi ya Mashetani Wekundu ikiwa watashinda Old Trafford.
Timu hiyo imekuwa katika kiwango safi baada ya kushinda mechi 13 za ligi na hadi sasa hawajafungwa katika michuano yote.
De Bruyne anaamini kuwa takwimu nzuri za City hazitakuwa na maana yoyote ikiwa watamaliza msimu bila taji.
"Ningependelea kuwa mbele kwa pointi 11 kuliko tano au nane kwa sababu ni bora zaidi na hiyo inamaanisha tuna faida ya mechi nne," Telegraph lilimnukuu De Bruyne akisema.
"Ni pengo zuri lakini halimaanishi chochote. Soka huenda kwa kasi sana. Ni miezi miwili ya kushughulika sana ambako lolote linaweza kutokea, lakini namna tunavyokwenda inapendeza na tunahitaji kuendelea hivyo.
"Naam, [ushindi 20 mfululizo ni mafanikio] lakini haijalishi kama hatushindi chochote mwisho wa msimu. Hakuna atakayejali kama ikiwa hatujashinda chochote mwisho wa msimu, Je! utaongelea mechi 20 tulizoshinda sasa? Ni jambo la kipekee lakini tunahitaji kushinda mwisho wa siku."
De Bruyne amefunga magoli manne na kutoa pasi nane za goli katika mechi 15 za ligi.
 
Tetesi

Mshambuliajia wa Manchester City na England Raheem Sterling, 22, atasitisha mazungumnzo kuhusu mkataba mpya huko Etihad hadi baada ya kombe la dunia. (Daily Mirror)
 
Tetesi
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atarudi na ofa kubwa ya kumsaini mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez, 28, mwezi Januari. (Independent)
 
Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero anaweza kuachwa kwenye kikosi cha Jumapili kitakachoikabili United ili kumpa nafasi Gabriel Jesus
Aguero ameanza mechi nne za mwisho za City katika michuano yote, lakini amefunga goli moja tu katika mecho hizo na alikuwa kimya tena katika mechi waliyoshinda 2-1 dhidi ya West Ham United katika uwanja wa Etihad.
Jesus aliingia kipindi cha pili cha mchezo huo na kusaidia kubadili mchezo kwa kutoa pasi ya goli la kusawazisha, na inasadikika kuwa meneja Pep Guardiola yupo tayari kumwanzisha Mbrazili huyo badala ya Aguero kwenye mechi kubwa ya City ya msimu.
Manchester Evening News kimedai kuwa Guardiola anaona kuwa kiwango cha Aguero kimeanza kushuka tangu alipovunjika mbavu Septemba, ingawa Mwargentina huyo amefanikiwa kufunga magoli 11 katika mechi 15 alizoanza msimu huu.
Jesus ana magoli 10 kwenye kampeni za msimu huu katika michuano yote, lakini amefunga mara mbili tu katika mechi zake 11 za mwisho na mchango wake umekuwa mkubwa zaidi akiingia utokea benchi wiki za hivi karibuni.
City wataingia kwenye Manchester derby Old Trafford wakiwa wameitangulia United pointi nane na wanataka kuweka rekodi ya kushinda mechi 14 mfululizo Ligi Kuu Uingereza.
 
Jesus yuko poa kwa sasa kuliko Aguero
 
Mwishoni mwa wiki hii dunia itasimama, mchezo mkubwa kabisa wa kufunga mwaka EPL utapigea kati ya majirani wawili Manchester United watakaokuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester City

Huu ni mchezo baina ya vilabu viwili vyenye nguvu ya pesa lakini pia ni mchezo kati ya makocha wawili ambao wanatajwa kuwa moja kati ya makocha bora sana duniani katika kizazi cha sasa.

Kama kawaida Jose Mourinho na Pep Gurdiola mara zote maneno hayakosekani, tayari Jose Mourinho ameanza maneno kwa kumshutumu kocha wa Manchester City Pep Gurdiola kwamba anadanganya kuhusu majeruhi.

Gurdiola alinukuliwa akisema kwamba David Silva ni majeruhi na anaweza kukosa mchezo wa Derby, jambo hilo limepokelewa tofauti na Mourinho kwani anaamini sio kweli na Pep anajua kwamba Silva atakuwepo.

Mourinho amedai kwamba yeye kwa upande wake hawezi kusema uongo hata siku moja kuhusu majeruhi, na majeruhi wote ambao Mourinho alisema awali hawatakuwepo katika kikosi hicho hawatakuwepo kweli.

United wanakutana na City ambao msimu huu wanaonekana kuwa tishia kubwa si tu nchini Uingereza bali barani Ulaya kwa ujumla, kama City atashinda mchezo huu atazidi ongeza pengo la alama kati yake na United na United wanahitaji kushinda ili kupunguza pengo.
 
Welcome Aboard Numbisa
 
Tetesi
Manchester City na Liverpool wote wanamtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Nice Jean Seri , 26, ambaye pia anatazamwa na Barcelona. (Daily Mail)
 
Kuna uwezekano mkubwa Real Madrid kukutana na kati ya hawa kwenye round inayofuata

• Manchester United
• Roma
• PSG
• Liverpool
• Manchester City
• Besiktas

akutane na yeyote ila sio PSG au Man City,

Ila walivyo washenzi watampangia Roma au Besiktas
 
Kocha Pep Guardiola wa Manchester City amewataka wachezaji wake kuepuka mipira ya adhabu.

Guardiola amewaonya wachezaji wake kuacha kutengeneza mazingira ya mipira ya adhabu katika mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu wao Manchester United.

Kocha huyo Mhispania, anahofia Man United inaweza kupata mabao kupitia mipira ya adhabu endapo Man City haitakuwa makini.

Man United ina wachezaji wengi warefu kulinganisha na Man City. Kiungo wa pembeni aliyerudishwa kucheza beki wa kushoto Ashley Young amepata umaarufu kwa mashuti ya mpira wa adhabu.

Man City itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Old Trafford kuikabili Man United katika mchezo wa Ligi Kuu England.Romelu Lukaku, Nemanja Matic, Chris Smalling na Zlatan Ibrahimovic ni wachezaji warefua ambao watakuwa tishio kwa Man City.
 
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa yeye na Jose Mourinho ni 'kama mapacha' kutokan na shauku zao kutwaa mataji.
Wawili hao wataendeleza uhasimu wao katika Old Trafford Jumapili mchana City watakapoikabili Manchester United katika mechi ya vinara wa ligi.
Guardiola na Mourinho hawajawahi kutazamana machoni, mara ya kwanza wakianza wakiwa Hispania Barcelona na Real Madrid, lakini kocha huyo wa City amesema wanafanana kuliko watu wanavyodhani.
Alipoulizwa kama Mourinho naye amedhamiria kutwaa mataji, Guardiola aliwaambia waandishi: "Kabisa! Katika hilo sisi ni mapacha. Anataka kushinda mataji, Nataka kushinda mataji.
"Antonio Conte kama ilivyo kwa Jurgen Klopp na Mauricio [Pochettino]. Tunapenda kushindana, tunapenda kushinda mechi lakini amini maneno yangu, wala si jambo la kipekee kwetu kuzifunga timu za Mourinho.Tumekutana mara nyingi katika nyakati kubwa."
Guardiola anamzidi Mourinho kwa kushinda mechi nane katika mechi 19.
 
Natabiri kesho manchester united anashinda 1-0 ushindi wa nyumbani ni 100%√√√ hakuna cha drooo pale ktk mech zote alizocheza sasa nendeni na kale ka jesus kanakofunga magoli karibia na kipa mkifikir mtapata hiyo nafas
 
Kuna uwezekano mkubwa Real Madrid kukutana na kati ya hawa kwenye round inayofuata

• Manchester United
• Roma
• PSG
• Liverpool
• Manchester City
• Besiktas

akutane na yeyote ila sio PSG au Man City,

Ila walivyo washenzi watampangia Roma au Besiktas

Ukiangalia mpira anaochezaga madrid hatua za mtoano utajiona mdogo kuzitaja timu za kiarabu hapo
 
Jose Mourinho amesema mchezo mkubwa baina yake na Guardiola hautabiriki lakini Pep amedai kuwa atafuraha mechi hiyo dhidi ya mahasimu wake
Zlatan Ibrahimovic, Phil Jones na Nemanja Matic wapo tayari kwa mechi ya Man United watakapoikabili Man City kwenye mechi inayosubiriwa kwa hamu kwenye jiji la Manchester, mubashara kupitia Goal.
Timu hizo mbili zinazoongoza Ligi Kuu zitakutana katika dimba la Old Trafford - matangazo yote ya mechi hiyo yatakuwa mubashara kupitia Goal.com - timu ya Jose Mourinho inataka kupunguza pengo la pointi dhidi ya City.

Timu yake ikiwa inajiandaa kwa mtanange huo, Mreno huyo amesema mechi kubwa huwa zina changamoto ambazo hazizuiliki.
"Soka halitabiriki," Mourinho alisema. "Kama meneja, naweza kujaribu kuelezea mipango ya mchezo na kuonyesha mwelekeo wangu lakini huwezi jua nini kitatokea. Kuna mambo mengi ambayo yapo nje ya uwezo wangu ambayo yanaweza kuubadili mchezo kabisa.

Kwangu mimi, ni mechi kubwa nyingine dhidi ya timu kubwa katika nchi hii. Tumekuwa timu bora kuliko mwaka jana - Nadhani pia Man City ni bora zaidi ya msimu uliopita."
City hawajafungwa katika ligi msimu huu lakini wamepoteza mechi yao ya kwanza katika kampeni za msimu huu katikati ya wiki baada ya kufungwa 2-1 na Shakhtar Donetsk Ligi ya Mabingwa.
 
Back
Top Bottom