Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,041
- 13,907
Kheli man city ashinde sio man uJapo mashushushu wekundu walimpiga arsenal ila mpira wao ulikuwa chini sana, arsenal walistahili ushindi kwenye ile mechi. Man U akicheza ule mpira aliocheza na arsenal juzi, Basi pont 3 kwa City mapema sana.
José Mourinho ni mkali sana wa kuweka defence, anaakili sana kwenye kutengeneza matokeo, Ila squad ya Mancity inatisha mkuu.
Sure bossMwaka huu anabeba kikombe
Asante kwa taarifaRatiba ya raundi ya tatu ya michuano ya kombe la Fa, imetangazwa usiku huu na michezo hiyo itachezwa wikiendi ya januari 6 na 7 mwaka 2018
Majogoo Liverpool wataanza michuano hiyo kwa kuchuana na wapinzani wao wa jadi Everton,huku bingwa mtetezi Arsenal akianzia ugenini kwa kucheza na Nottingham Forest.
Matajiri wa Manchester City wataanzia nyumbani katika dimba la Etihad,kwa kucheza na Burnley nao Manchester United wakiwalika Derby County.
Vijana wa Antonio Conte, Chelsea wataanzia ugenini kwa kucheza na Norwich, Tottenham Hotspur watakua wenyeji wa AFC Wimbledon
Jesus yuko poa kwa sasa kuliko AgueroMshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero anaweza kuachwa kwenye kikosi cha Jumapili kitakachoikabili United ili kumpa nafasi Gabriel Jesus
Aguero ameanza mechi nne za mwisho za City katika michuano yote, lakini amefunga goli moja tu katika mecho hizo na alikuwa kimya tena katika mechi waliyoshinda 2-1 dhidi ya West Ham United katika uwanja wa Etihad.
Jesus aliingia kipindi cha pili cha mchezo huo na kusaidia kubadili mchezo kwa kutoa pasi ya goli la kusawazisha, na inasadikika kuwa meneja Pep Guardiola yupo tayari kumwanzisha Mbrazili huyo badala ya Aguero kwenye mechi kubwa ya City ya msimu.
Manchester Evening News kimedai kuwa Guardiola anaona kuwa kiwango cha Aguero kimeanza kushuka tangu alipovunjika mbavu Septemba, ingawa Mwargentina huyo amefanikiwa kufunga magoli 11 katika mechi 15 alizoanza msimu huu.
Jesus ana magoli 10 kwenye kampeni za msimu huu katika michuano yote, lakini amefunga mara mbili tu katika mechi zake 11 za mwisho na mchango wake umekuwa mkubwa zaidi akiingia utokea benchi wiki za hivi karibuni.
City wataingia kwenye Manchester derby Old Trafford wakiwa wameitangulia United pointi nane na wanataka kuweka rekodi ya kushinda mechi 14 mfululizo Ligi Kuu Uingereza.
Mwishoni mwa wiki hii dunia itasimama, mchezo mkubwa kabisa wa kufunga mwaka EPL utapigea kati ya majirani wawili Manchester United watakaokuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester City
Huu ni mchezo baina ya vilabu viwili vyenye nguvu ya pesa lakini pia ni mchezo kati ya makocha wawili ambao wanatajwa kuwa moja kati ya makocha bora sana duniani katika kizazi cha sasa.
Kama kawaida Jose Mourinho na Pep Gurdiola mara zote maneno hayakosekani, tayari Jose Mourinho ameanza maneno kwa kumshutumu kocha wa Manchester City Pep Gurdiola kwamba anadanganya kuhusu majeruhi.
Gurdiola alinukuliwa akisema kwamba David Silva ni majeruhi na anaweza kukosa mchezo wa Derby, jambo hilo limepokelewa tofauti na Mourinho kwani anaamini sio kweli na Pep anajua kwamba Silva atakuwepo.
Mourinho amedai kwamba yeye kwa upande wake hawezi kusema uongo hata siku moja kuhusu majeruhi, na majeruhi wote ambao Mourinho alisema awali hawatakuwepo katika kikosi hicho hawatakuwepo kweli.
United wanakutana na City ambao msimu huu wanaonekana kuwa tishia kubwa si tu nchini Uingereza bali barani Ulaya kwa ujumla, kama City atashinda mchezo huu atazidi ongeza pengo la alama kati yake na United na United wanahitaji kushinda ili kupunguza pengo.
Kuna uwezekano mkubwa Real Madrid kukutana na kati ya hawa kwenye round inayofuata
• Manchester United
• Roma
• PSG
• Liverpool
• Manchester City
• Besiktas
akutane na yeyote ila sio PSG au Man City,
Ila walivyo washenzi watampangia Roma au Besiktas