Gundogan alifunga goli la kwanza kwa kichwa akiunganisha kona ya Leroy Sane dakika 14 baada ya wenyeji kuumiliki mpira dhidi ya Spurs na waliendelea kutawala mchezo.
Shuti la De Bruyne liliwavunja nguvu Spurs baada ya mpira kuzama wavuni na Sterling aliweka kimiani mara mbili kwa shuti la karibu baada ya kukosa goli la wazi kufuatia Gabriel Jesus kukosa penalti ambayo iligonga mwamba.
Chrstian Eriksen aliipatia Spurs goli la kufutia machozi dakika za mwisho lakini pengo lao dhidi ya vinara hao wa ligi limeongezeka hadi pointi 21.
City wameshawafunga mahasimu wao wote wa taji Ligi Kuu Uingereza msimu huu na mbio zao kuelekea ubingwa wa Uingereza zinaonekana kukosa mpizani.
Walifunga goli lao la kwanza kupitia nafasi yao ya pili, Baada ya Gundogan kuwahadaa mabeki wa Spurs na waliruhusu goli kirahisi mno kupitia Raheem Sterling aliyetupia goli la tatu.
Ukungu ulishuka kwenye uwanja wa Etihad lakini haukuweza kuwazuia City kufanya mambo yao na Hugo Lloris alilazimika kulinda lango hadi kwenda mapumziko wakiwa wa wamefungwa 1-0 tu, Kipa huyo wa Kifaransa aliokoa mara mbili kumzuia Gundogan kufunga goli la pili.
Harry Kane alipiga shuti bomba ambalo lili gonga mwamba Spurs walipotishia kufunga kwa mashambulizi ya kushtukiza, na Mshambuliaji huyo wa Uingereza alikaribia kufunga goli la kusawazisha alipomlazimu Ederson kujinyoosha kuokoa baada ya mapumziko.
Spurs waliongeza nguvu yao lakini mashambulizi ya kushtukiza yaliwagharimu pale De Bruyne alipoweka kimiani dakika ya 70.
Jan Vertonghen alimwangusha De Bruyne ndani ya boksi kwa penalti iliyokuwa dhahiri, lakini Jesus aliyeingia kutokea benchi alipiga mwamba kabla ya Sterling kujaribu kumalizia na kushindwa kwani mpira ulipaa juu.
Sterling alifuta makosa yake ya kukosa magoli ya wazi akiweka kimiani goli rahisi dakika ya 80, kabla ya kufunga jingine kwa kutumia makosa ya Eric Dier baada ya kumpiga tobo Lloris kuipatia City goli la nne.
Spurs wamefanywa zilichofanywa timu nyingine zote zilizotembelea Etihad msimu huu,na Eriksen hakushangilia alipofunga goli la kufutia machozi kwa Spurs dakika za mwisho.