The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Mkuu wa akademi ya Manchester City Brian Marwood amekwenda kumtazama kiungo wa Lille Boubakary Soumare, 18, ambaye ametajwa kuwa ni "Paul Pogba mpya". (Mail)
 
Tetesi

Manchester City inatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte wikendi hii. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amebadilisha nia yake baada ya kukataa uhamisho wa kueleka City miezi 18 iliopita.{Mirror}
 
Tetesi

Manchester City wako tayari kutoboa mfuko wao kwa kitita cha Euro milioni 150 kummendea mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 27, baada ya Pep Guardiola kumbaini winga wa Ubelgiji kama mchezaji muhimu atakaemtia kibindoni wakati wa majira ya joto kulingana na gazeti la Sunday Mirror
 
Tetesi
Manchester City na Manchester United wanatarajia kung'ang'ana kujaribu kumchukua mchezaji wa kati mBrazil Fred mwenye umri wa miaka 24, kutoka Shakhtar Donetsk limesema kazeti la Daily Star Jumapili.
 
Tetesi

Wakati huo huo gazeti la Daily Star la Jumapili limethibitisha kuwa Arsenal wamepania kushinda mchuano wa kutia saini mkataba na mlinzi wa West Brom Jonny Evans, mwenye miaka 30, huku Manchester City wakiwa na uhakika wa kusaini mkataba na Aymeric Laporte kutoka Athletic Bilbao.
 
Klabu ya Manchester City kupitia tovuti yake imetangaza kumsajili beki wakati wa timu ya taifa ya Ufaransa, Aymeric Laporte.

Laporte mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na klabu ya Athletic Bilbao kabla ya meneja wa City,Pep Guardiola kumsajili kwa kwa dili litakalo muweka hapo mpaka mwaka 2023.

Mlinzi huyo ambaye ni chaguo la Guardiola, atavaa jezi namba 14 na kuisaidia timu hiyo kushinda mataji mbali mbali.

Laporte mara baada ya kuingia kandarasi na City amesema “Ni mwenye furaha kubwa kuwa hapa katika timu yenye malengo makubwa na miongoni mwa klabu kubwa barani Ulaya,” amesema Laporte.

Aymeric Laporte ameongeza “Nitaendelea kupambana na kufanya kazi kwa juhudi nikiwa chini ya Pep Guardiola na kuisaidia timu kufikia mafanikio.”

Laporte alianza soka la kulipwa akiwa na Bilbao mwaka 2012
 
Manager wa Manchester City Pep Guardiola , Amethibitisha kuwa mchezaji wake mahiri Leroy Sane aliyeumia Kiunga cha mguu katika mechi ya FA Cup iliyochezwa jumapili na Cardiff City anatarajiwa kuwa nje kwa majuma saba.

Leroy Sane.png

Sane atakosa mechi ya fainali ya kombe cha Carabao kati ya Manchester City na Arsenal hapo whembley na vilevile Champions League last 16 kati ya Manchester City na Basel.

sane3.png

Kukosekana kwa mchezaji huyu na hapohapo tumemkosa Alexis Sanchez, kumetuumiza sana sisi washabiki na nahisi safu ya ushambuliaji wa timu ya Manchester City wasipofanya mpango wa kumtafuta mbadala wake mapema kutaathiri yale Meno yetu. wakati hatuna tumaini la lini Gabriel Jesus atarudi uwanjani.

City wanabaki na front three wao pekee kina, Raheem Sterling, Bernardo Silva na Sergio Aguero.

DUBHIYLX4AE_xX4.jpg
 
Manager wa Manchester City Pep Guardiola , Amethibitisha kuwa mchezaji wake mahiri Leroy Sane aliyeumia Kiunga cha mguu katika mechi ya FA Cup iliyochezwa jumapili na Cardiff City anatarajiwa kuwa nje kwa majuma saba.

View attachment 689525

Sane atakosa mechi ya fainali ya kombe cha Carabao kati ya Manchester City na Arsenal hapo whembley na vilevile Champions League last 16 kati ya Manchester City na Basel.

View attachment 689526

Kukosekana kwa mchezaji huyu na hapohapo tumemkosa Alexis Sanchez, kumetuumiza sana sisi washabiki na nahisi safu ya ushambuliaji wa timu ya Manchester City wasipofanya mpango wa kumtafuta mbadala wake mapema kutaathiri yale Meno yetu. wakati hatuna tumaini la lini Gabriel Jesus atarudi uwanjani.

City wanabaki na front three wao pekee kina, Raheem Sterling, Bernardo Silva na Sergio Aguero.

View attachment 689529
Ila tutafika tu tuendako mkuu. Usihofu. Tunakikosi kipana.
 
Ila tutafika tu tuendako mkuu. Usihofu. Tunakikosi kipana.
Sure mkuu, tuna watu wengi wapo vizur na nafasi hawapati sana.... ukiangalia mtu kama Bernardo Silver mm namuamini sana naimani ata kocha akimuamini pia atapiga kazi nzuri wakati tukimsubiri Sane
 
Back
Top Bottom