The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

HUKO England kumenoga, ni amshaamsha tu. Ile mikikimikiki ya Ligi Kuu England imerudi rasmi, usiku wa jana Ijumaa kulikuwa na mechi moja, lakini uhondo kamili unaanza leo Jumamosi na kuendelea kesho Jumapili.

Jana Manchester United ilikuwa na shughuli pevu huko Old Trafford ilipoikaribisha Leicester City na hiyo ilikuwa mechi ya kufungua pazia la Ligi Kuu England, ambapo kila kocha anajaribu kusaka njia za kuubeba ubingwa ambao msimu uliopita ulinyakuliwa na Manchester City ya Pep Guardiola.

Utamu wa ligi hiyo kwa timu za Top Six kwa msimu huu ni kwamba kutakuwa na makocha wawili wageni, Unai Emery huko Arsenal na Maurizio Sarri huko Chelsea.

Makocha hao wanakuja kuwapa changamoto wenyeji wao, Guardiola wa Man City, Jose Mourinho wa Man United, Jurgen Klopp wa Liverpool na Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur.

Mchakamchaka wa msimu huu utashuhudia pia mastaa wa kigeni kibao wakitua kwenye Ligi Kuu England kuongeza uhondo utakaofanya utamu wa michuano hiyo pengine kuzidi misimu uliopita.

Mechi ya kwanza itakayofanyika mchana wa leo Jumamosi, Newcastle United inayonolewa na Rafa Benitez itakuwa nyumbani kuikaribisha Spurs, mechi inayotazamwa itakuwa ngumu kwelikweli kabla ya Bournemouth kumaliza ubishi na Cardiff City, Fulham ikiwa na mastaa wapya kibao wakishuka uwanjani kucheza na Crystal Palace, Watford ikicheza na Brighton na Wolves itakuwa na kasheshe mbele ya Everton. Kocha Sarri ataanzia shughuli ya Ligi Kuu England ugenini wakati atakapoifuata Huddersfield.

Lakini yote hiyo ni tisa, kumi bana ni vipute vya hiyo kesho Jumapili. Huko Emirates kutakuwa na kasheshe zito, wakati Emery na chama lake la Arsenal watakapowakaribisha mabingwa watetezi Man City.

Mechi hiyo inatarajia kuwa na ufundi mkubwa, huku Arsenal ikiingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa Tatu Bila katika mechi ya mwisho ya ligi ilipocheza uwanjani Emirates dhidi ya vijana hao wa Guardiola.

Lakini mechi hiyo ya baadaye, itatanguliwa na mechi mbili matata, wakati Liverpool itakapokuwa Anfield kuikaribisha West Ham United, ambayo imefanya usajili mkubwa sana kwenye dirisha lililofungwa juzi Alhamisi.

Mechi nyingine itakayopigwa kesho ni ile ya Southampton itakapocheza na Burnely. Macho ya mashabiki baada ya kuona ile shughuli ya Man United usiku wa jana, sasa watasubiri kuona kipi kitafanywa na Chelsea, Tottenham, Man City na Arsenal kwenye mechi zao. Mambo ni moto!
 
Numbisa kwenye ubora wako mkuu.
 
Arsenal XI: Cech, Bellerin, Sokratis, Mustafi, Maitland-Niles, Guendouzi, Xhaka, Mkhitaryan, Ramsey, Ozil, Aubameyang.

Subs: Leno, Elneny, Lacazette, Torreira, Lichtsteiner, Holding, Iwobi.

Manchester City XI: Ederson, Walker, Stones, Laporte, Mendy, Bernardo Silva, Fernandinho, Gundogan, Mahrez, Aguero, Sterling.

Subs: Bravo, Kompany, De Bruyne, Sane, Otamendi, Jesus, Foden.
 
Sterling goal
1534087550961.gif
1534087567169.jpg
 
1534094777637.jpg
1534094782829.jpg
1534094798232.jpg
1534094854912.jpg
1534094791793.jpg
1534094875810.jpg
1534094854912.jpg
 
Attachments

  • 1534094875810.jpg
    1534094875810.jpg
    44.9 KB · Views: 27
  • 1534094791793.jpg
    1534094791793.jpg
    21.3 KB · Views: 31
washabiki wengi wa man city ..walikuwa liver na arsenal ..kwaiyo mkuu wacha usaliti rudi kweny yako ya zamani.

Man city ni timu ya juz tu 2011
Mi nilihama toka barca. Wingereza sijawahi kuw na team nyingine yote?
 
Kinyang’anyiro cha Ligi Kuu England, kimeanza tangu wikiendi iliyopita, timu zinazotabiriwa kumaliza ndani ya nne bora, mabingwa watetezi Manchester City, Liverpool, Tottenham na Manchester United zikianza kwa kishindo.
Tottenham iliyoziengua Chelsea na Arsenal katika ‘top four’ ikitamba kwa msimu wa tatu mfululizo licha ya kujadiliwa sana kutokana na kutosajili mchezaji yeyote katika dirisha la usajili wa kiangazi, lakini imethitisha kuwa haikuwa na sababu za kusajili kwani inacho kikosi bora baada ya kushinda ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United.

Ujio wa Kocha, Maurizio Sarri, unaweza kuwa suluhisho kwa Chelsea, kwani aliiwezesha kushinda mabao 3-0 dhidi ya timu ngeni katika Ligi hiyo, Huddersfield Town, lakini wikiendi hii ndipo atapaswa kuthibitisha kama anao ubavu wa kuchuana kuing’oa Tottenham ndani ya nne bora.
Sarri atathibitisha hilo, atakapoiongoza Chelsea kuikaribisha Arsenal kwenye Uwanja wa Stamfodge Bridge, iwapo itaondoka na ushindi wa kishindo kama ilioupata kwa Huddersfield ataanza kuwashawishi wengi kuipa nafasi ya kufanya vema msimu huu.
Arsenal jana Jumapili iliyopita ilicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani bila Arsene Wenger kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996, licha ya kuwa nyumbani kocha Emery Unai hakuweza kuiepusha na adhabu kutoka kwa mabingwa watetezi City na kufungwa mabao 2-0.

Kocha wa kuwa huyo wikiendi ijayo pia atakuwa katika wakati mgumu kwani atasafiri kuifuata Chelsea moja ya timu ambazo zinaonekana zina vikosi bora vinavyoweza kupigania ubingwa.
Kwa upande wake Kocha City, Pep Guardiola alitamba kuwa kikosi chake kitazidi kutoa dozi kwa kila timu itakayocheza nayo akidai timu hiyo inamarika siku hadi siku.
Guardiola alisema kuwa anaamini katika mechi ijayo sio Bernardo Silva na Raheem Sterling pekee walioifungia mabao hayo, watakafunga tena wikiendi ijayo bali wafungaji wataongezeka watakapoikaribisha Huddersfield Jumapili hii.

Nayo Manchester United chini ya Jose Mourinho imeanza vema Ligi baada ya kuichapa timu bingwa ya Ligi hiyo msimu wa 2015/16, Leicester City kwa mabao 2-1 na wikiendi hii itaifuata timu isiyo na uzoefu ya Brighton.
Upande mwingine, Henrikh Mkhitaryan aliyehamia Arsenal akitokea United pamoja na washambuliaji mahiri Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette hawakuibeba Arsenal kama walivyofanya katika timu zao za zamani Aubameyang alikua tegemeo la mabao kwa Borussia Dortmund ya Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ na Lyon ya Ufaransa ‘Ligue 1’.
City ambayo iliilaza Chelsea mabao 2-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii inaonekana kuzidi kuimarika kila kukicha na sasa ni wazi kuwa inaweza kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Ligi Kuu.

City iliyomnunua Riyad Mahrez pekee katika dirisha la usajili wa kiangazi kwa Pauni 60 milioni kutoka Leicester City, alionyesha ana kitu amekiongeza kwa City.
Mitambo ya Liverpool inaonekana imeongezeka nguvu na imeonyesha dalili kuwa itaangamiza zaidi msimu huu baada ya Sadio Mane kufunga mawili, Mohamed Salah na Daniel Sturridge nao wakitupia, huku James Milner na Robeto Firmino, wakicheza soka la kiwango cha juu, hata hivyo Liverpool wikendi hii itakuwa ugenini ikiifuata Crystal Palace.
 
Huwezi bahatisha mara mbili!
Mwaka huu hamna chenu hamchukui hata FA
Mbunu zile zile haziwezi kukupa EPL mara mbili mfululizo!
Kw amabeki hawa wazito Liverpool anakufunga home and away
Liverpool ndiyo mabingwa wapya wa EPL
Nani hapa anaweza simama na kusema hayaogopi majogoo ya ANFIELD?
 
Back
Top Bottom