EPL ndiyo ligi inayoongoza kwa kuwa na thamani kubwa duniani (kwa football).
Hili linachangiwa na wao wenyewe waingereza kupenda mpira (unaweza kuangalia jinsi viwanja vinavyojaa hadi mechi za ligi ndogo).
Pia wameifanyia sana matangazo ligi yao, wana mkataba wa broadcasting ambao ni mkubwa sana, kila timu inapata mgao wa kutosha hapo.
Angalia hata huku kwetu, kupata nafasi ya kuonesha ligi ya EPL siyo shughuli ndogo, ndiyo maana huwezi kupata local channel inashinda hiyo tenda.
Wameweza kufanya ligi yao ipendwe dunia nzima, sina uhakika kwa USA (hawa wana michezo yao kama American Football, Basketball, Baseball na Hockey).
Na Manchester United ndiyo club ya michezo yenye washabiki wengi duniani (michezo yote).