The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Ni kweli
Ila nyie kwa kuwa mnaendesha mambo kisasa na mnakocha mzuri its possible.

Man utd bado tuko kwenye transition, Chelsea huwa hawatabiriki, Liver wana kocha mzuri asiye jua finishing na Arsenal ndio kama walivo.
Kwa hiyo mkijipanga mna beba
Huyu kocha hatabiriki mkuu, anaweza kusepa muda wowote.
 
Guardiola, anaelekea kuiongoza timu yake kunyakua taji la ligi kuu msimu huu kwa sababu inaongoza ligi kwa alama 78, baada ya mechi 29 ikifuatwa na Manchester United ambayo ina alama 65 baada ya mechi 30.

Kuna tofauti ya alama 13 kati ya timu hizi mbili kuelekea kumalizika kwa msimu wa ligi mwezi Mei.

Ushindi dhidi ya Stoke City siku ya Jumatatu, utaihakikishia zaidi Manchester City kunyakua ubingwa msimu huu kwa sababu itakuwa inaongoza alama 18 zaidi.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina Sergio Aguero, atakosa mchuano wa Jumatatu na atasalia nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili baada ya kupata jeraha la goti wakati akiwa mazoezini.

Kocha Guardiola anatarajiwa kukutana na Mwenyekiti wa klabu hiyo Khaldoon al Mubarak baada ya mechi ya Jumatatu.
 
Back
Top Bottom