Mimi bado namuamini ni kocha nzuri, ni kocha bora kabisa mwenye uwezo wa kutimiza malengo yetu. Kikubwa tuwe na moyo wa Subira na tusitake vitu vitimie kwa muda tunaotaka sisi.....
Hakuna timu isiyofungwa wala hakuna timu isiyotolewa kwenye michuano. Kutolewa CL kusitufanye tusahau wema na mazuri yoye ya Pep, japo ni kawaida ya binadamu kuangali makosa tu ila tusisahau zile sifa kede kede tuliokua tukimmwagia kocha wetu.....
Tulivyopangiwa Tot watu walionekana kumdharau ata humu ndani kuna kauli zilionekana wadau wakisema wanamtaka ata Barca, japo huwa kuna kauli nyingine za kishabiki ila nilisema humu bado hatupo sawa kuvaana na timu kama Barca ila niliwaudhi watu wengine wakaniita mamluki.....
Tot ni timu kubwa tusijisikie vibaya kututoa kwenye CL, hapa tusubiri msimu ujao ila kikubwa bado tunanafasi ya kuendelea kupambania EPL na FA CUP tunaisubiri kukipiga final....