.Kuna mechi ambazo Pep Guardiola hatojali kiwango bali atataka matokeo tu , sio kwamba Man City tulikuwa vibaya , hapana bali Leicester walikuwa wabishi sana
.Leicester City walianza mechi kwa kucheza 4-5-1 Vardy akiwa mbele peke yake na pengine inawezekana Ederson aligusa mpira mara nyingi zaidi ya Vardy kwasababu Leicester walikuwa nyuma sana na City walikaa sana na mpira na hata Leicester wakipata mpira hasa dakika 60 za mwanzo mbele walikuwa wanaenda wachezaji wachache sana ( Vardy Barnes na Maddison ) tu
.Wakati Man City na 4-3, KDB na Gundo kwenye namba 8 wawili nyuma ya kiungo cha Leicester , kwenye build yao hawakuhitaji kuwa wengi sana kama wanavyofanya mechi zingine kwasababu Leicester walikuwa na mchezaji mmoja tu mbele ( walibaki Akanji Laporte na mara kadhaa Stones ) lakini City hawakupata sana spaces za kucheza mpaka mpira uliokufa wa KDB uliotinga wavuni
.Nafikiri kuanzia dakika ya 70 mchezo ulikuwa tofauti na Leicester nafikiri walikuwa timu bora katika dakika 20 za mwisho kutoka 4-5-1 mpaka 4-2-3-1 ( Maddison kwenye namba 10 , Tielemans na Mendy kwenye kiungo huku Tielemans akiwa na uhuru wa kusogea juu zaidi ya Mendy ) na hapo Leicester walianza kushambulia zaidi, pressing , pass mpira vizuri , walishinda hata mipira ya pili mingi zaidi ya City , pongezi kwa City tu walizuia vizuri na hawakutaka kufanya mambo mengi nyuma zaidi ya kuuhamisha haraka mpira kwenda mbele
NOTE
1: Leicester wanaweza kupata matunda ya kumvumilia Rodgers maana katika mechi kama 4 zilizopita unaona uimara umerejea
2: Golikipa huwa wanavuna alama kwa timu zao na Ederson leo kavuna alama 3 kwa City , mkwaju mkali ( Volley ) ya Tielemans kaugusa kidogo na kugonga mwamba wa juu
3: ILE FREEKICK YA KDB [emoji91] hakuna Kipa yoyote Duniani anaokoa