Kiukweli kwa mpira tunaocheza, Harry kane ndio alikuwa chaguo sahihi kabisa.
Ukiachana na uwezo wake wa kufunga, anatengeneza nafasi za kufunga pia na ana uwezo mzuri wa kuplay part kwenye build up.
mtu kama huyu angetufaa pale mbele.
Haaland yeye ni wale old fashioned strikers ambao wanasubiri final passes waweke kambani na si zaidi ya hapo.
uwepo wa mtu kama huyo kwenye timu inayocheza pasi nyingi kunapunguza ile fluidity ya uchezaji wa timu.
ndicho kinachotokea city
sasahivi.
Toka msimu huu uanze, ile signature style of play ya man city ya misimu yote haipo tena.
Timu inacheza kwa kutegemea kumlisha haaland huku yeye mwenyewe akiwa yupo tu pale kati anasubiri kufanya tap in.
Timu ikibanwa, haaland anakuwa useless.
Kiukweli kama tukiendelea kustick kwenye huu mpira wa pasi nyingi basi alvarez ndio atatufaa zaidi.
Ana uwezo wa kutengeneza nafasi, ana high pressing ability na ana uwezo wa kufunga.
Ama tuswitch kwenda kwenye direct football ambao ndio style inayofaa zaidi kwa mastraika aina ya haaland.