Jana sikufanikiwa kuangalia game yote, ndio nimemaliza kuangalia replays.
Gundogan na walker, hawa wazee inabidi watupishe kwakweli, very poor perfomance hiyo jana.
Mtu kama Gvardiol, japo ni natural CB lakini unamuona kabisa ni mzuri kushambulia ila defensively ni urojo urojo urojo.
Ederson confidence hakuna tena.
Pale katikati bila KDB hakuna creativity yeyote.
Hiki kikosi kinahitaji kufumuliwa upya.
January Walker atafutiwe pa kwenda atupishe, tupate young fullback mwingine ambaye ni versatile kama Lewis, Gundogan ale benchi tupate solid DM wa kueleweka (Kova sio wa kumuamini)
Gvardiol acheze LB, pale kati awaachie Akanji, Stones na Ake.
January pekee tunahitaji sajili si chini ya 2 za watu ambao wako tayari kwa kazi.