The mind of the commoners (akili ya watu wengi)

The mind of the commoners (akili ya watu wengi)

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,315
Reaction score
13,269
Nikifanya kitu kilicho ktk akili ya wengi watu watanipenda watanipa likes,

Hii inanifanya niwe sawa na wengi, nikiwa sawa na wengi maana yake akili yangu na yao zinafanana,

Kama akili yangu na yao zinafanana tupo sawa ktk mambo mengi kiuchumi, kielimu hata kimtazamo


Ili nifanikiwe inabidi niwe na akili tofauti na wengi, niwe na uwezo wa kuwatumia wengi waninufaishe,


Utofauti wa akili(fikra) zangu na wengi ndio utakao nitofautisha ktk jamii kati yangu na wao, kimafanikio na kimaendeleo

Huenda waliofanikiwa wana fikra tofauti na wengi,

Nikiandika kitu ukanipa like maana yake akili yako na yangu zinafanana

Nikiandika kitu uzi ukakosa wachangiaji maana yake akili yangu na wengi ni tofauti hazikubaliani zinatofautiana


Huenda akili yangu ni ndogo kuliko ya wengi au yangu ni kubwa kuliko ya wengi huu ni mtazamo

Ili unijubali inabidi nifanye kitu kilicho ktk akili yako, maana yake nikuburudishe, ili uburudike inabodi niyajue mawazonyako, hii inanifanya nikutegemee kisaikolojia na kiuchumi,

Nisipojitambua ukanikosoa badala ya kunikubali nitakuwa na akili ndogo kuliko yako


Ila nikijitambua nitakuwa na akili kubwa kuliko yako


Matabaka ktk jamii ni matokeo ya utofauti wa akili au fikra

Wengi wapo sawa tabaka la chini, kuliko walio tabaka la juu

Nadhani mafanikio yanaanzia kichwani

Ukimuona mwenzako ni chizi au kichaa hajitambui basi kuna mmoja kati yenu ndio chizi kati yako wewe au yeye sababu akili zimetofautiana

Nawaza tu


Kuna mengi ya kutafakari
 
Watu wanahisi umechanganyikiwa lakini kwa upande wangu naona upo sawa
 
Back
Top Bottom