The Most Humiliating NBA Draft Picks Of This Millennium: Hasheem Thabeet

The Most Humiliating NBA Draft Picks Of This Millennium: Hasheem Thabeet

Umeleta mada alafu hapo hapo unatuuliza swali ambalo umeweka na jibu, ungeuliza tu hasheem alikua analipwa sh ngapi?
 
mwaka wa hasheem wenzake wengi wamekuwa mastaa wanakula pesa ndefu.. yeye hata nba wamemtimua...

na akaenda ligi daraja la chini napo wamemtimua...

wachezaji walioingia nba mwaka mmoja na hasheem,,,,,,,,steph curry, de mar derozan, james harden, ricky rubio, blake gliflin, wote wamekuwa nyota wa timu zao
 
mwaka wa hasheem wenzake wengi wamekuwa mastaa wanakula pesa ndefu.. yeye hata nba wamemtimua...

na akaenda ligi daraja la chini napo wamemtimua...

wachezaji walioingia nba mwaka mmoja na hasheem,,,,,,,,steph curry, de mar derozan, james harden, ricky rubio, blake gliflin, wote wamekuwa nyota wa timu zao

Aisee kama haondio alioingia nao NBA tena akiwa # 2 Draft. Bsi kachemsha sanaaa
 
We jamaa sio muungwana,unafikiri watu wote wanajua kuzitafakuri picha.
At least explain the message behind hizi picha zako na si kuona wenzako ni fyatu wakikuuliza jambo acha majivuno dogo.Na dharau si vyema ukawafanyia walimwengu, mfanyie mamako huko nyumbani kwenu.
 
Ahahaha!! Haya maisha bwana. Usipokaza utakazwa.

Tatizo Wanadamu huwa tuna njaa pale tunapokuwa na shida lakini tukishapata tunaregeza.
Leo Hasheem Thabit kama kasahaurika kabisa. Zamani kila akija likizo Bongo lazima mtajua tu. Media zote zinaandika habari yake. Kwasasa huwa anakuja kimyakimya.

Ila Hasheem bado ana maisha mazuri hata kama akisema asijeze tena Basketball. Mpunga aliovuna kipindi kile ni mrefu sana.
Kama alijisahau kuwekeza basi amepoteza.
 
Unaweza ukasema huyo kijana ameyachezea maisha....lakini anayeujua uhondo wa ngoma ni yule aliyeingia kati na kucheza , sio yule anayeshangilia........

Hata kama ameharibu upande huo wa mpira wa kikapu( kama ni kweli ameharibu) bado ana fursa kibao za kufanya mambo mengi zaidi yenye mafanikio kuliko sisi tunaoshindia kunywa kahawa hapa mwananyamala kwa kopa......

Kumbuka yupo kwenye moja ya mataifa tajiri na lenye nguvu kiuchumi....na vile vile yeye bado ni kijana mdogo sana kwa hiyo bado ana nafasi zaidi kwenye maisha yake ya kujaribu mambo mengine.....

Anord Schwazneger( sina uhakika hizo herufi) alikuwa ni mtunisha misuli maarufu huko marekani....baadae akawa mcheza filamu maarufu pia huko marekani....baadae akawa Gavana wa jimbo maarufu huko Marekani.....hadi unaweza ukaona ni jinsi gani Amerika ni sehemu ya fursa mbali mbali ambapo anguko...lako la upande huu linaweza kuwa ndio inuko lako la upande mwingine.....tofauti na huku kwetu ambapo ukianguka ndio umeporomoka...tunakukuta shimoni huko.....

By the way kwanini sisi watanzania tunachukia mafanikio ya ndugu zetu sana na tunayafurahia sana maanguko ya ndugu zetu wenye mafanikio....!!?? Hii ni roho gani ya kipuuzi iliyo ndani yetu....kwanini ufurahishwe na anguko la mwenzako baada ya kumuombea...!!!!??? Kwanini unachukia mafanikio ya mwenzako hali ya kuwa hukuwa na mchango wowote kwenye safari yake ya mafanikio.....only in Tanzania.....
 
Back
Top Bottom