The Most Humiliating NBA Draft Picks Of This Millennium: Hasheem Thabeet

The Most Humiliating NBA Draft Picks Of This Millennium: Hasheem Thabeet

Ana laana ya Watanzania. Kipindi flani alipokuja alizoza mbovu sana pale clouds. Nakumbuka alisema kuwa hakuna mtu aliyemsaidia kufika hapo alipofika so na yeye haoni haja ya kusaidia wengine... Can u imagine?
 
Ndo maana unaambiwa kipimo au utaratibu mzuri wa kujijenga katika kipaji au maendeleo binafsi huanza mdogomdogo taratiibu graph ina incline yenyewe.
Hashim Thabit mafanikio yake kwenye game yalikuwa ya ghafla mno. Huwa sielewi sijui wazungu walipapatika na urefu wake au yeye mwenyewe tu alichukulia rahisi fursa ya yeye kuwepo kwenye chart ile akalewa sifa na kushindwa kukaza?!
I feel sorry for you my young... Stretch yourself probably they will re-glance at you and prove to them that you deserve enough to be where you been.
 
Unaweza ukasema huyo kijana ameyachezea maisha....lakini anayeujua uhondo wa ngoma ni yule aliyeingia kati na kucheza , sio yule anayeshangilia........

Hata kama ameharibu upande huo wa mpira wa kikapu( kama ni kweli ameharibu) bado ana fursa kibao za kufanya mambo mengi zaidi yenye mafanikio kuliko sisi tunaoshindia kunywa kahawa hapa mwananyamala kwa kopa......

Kumbuka yupo kwenye moja ya mataifa tajiri na lenye nguvu kiuchumi....na vile vile yeye bado ni kijana mdogo sana kwa hiyo bado ana nafasi zaidi kwenye maisha yake ya kujaribu mambo mengine.....

Anord Schwazneger( sina uhakika hizo herufi) alikuwa ni mtunisha misuli maarufu huko marekani....baadae akawa mcheza filamu maarufu pia huko marekani....baadae akawa Gavana wa jimbo maarufu huko Marekani.....hadi unaweza ukaona ni jinsi gani Amerika ni sehemu ya fursa mbali mbali ambapo anguko...lako la upande huu linaweza kuwa ndio inuko lako la upande mwingine.....tofauti na huku kwetu ambapo ukianguka ndio umeporomoka...tunakukuta shimoni huko.....

By the way kwanini sisi watanzania tunachukia mafanikio ya ndugu zetu sana na tunayafurahia sana maanguko ya ndugu zetu wenye mafanikio....!!?? Hii ni roho gani ya kipuuzi iliyo ndani yetu....kwanini ufurahishwe na anguko la mwenzako baada ya kumuombea...!!!!??? Kwanini unachukia mafanikio ya mwenzako hali ya kuwa hukuwa na mchango wowote kwenye safari yake ya mafanikio.....only in Tanzania.....
hahaha...eti ukiporomoka tunakukuta shimoni huko....kama mr nice vile
 
Kamuulizeni jokate, na rafiki zake pale Samaki samaki mlimani city..
 
mshahara anafanya kazi wapi?

hapa hatumpigi majungu.. tunaongea nini kimemkuta aliyekuwa mwakilishi wa taifa nba.

naomba utuambie kwa facts sasa hivi hasheem anafanya kitu gani na kama anacheza ni timu gani?

...huyo Hasheem bado yuko juu zaidi wengi wetu humu,kwa mshahara aliokuwa analipwa hata kwa mwezi tu,ni mkubwa!

....tuhangaikie ya kwetu, tuachane na ya wenzetu!
 
Cheki hapo wenzake bado wapo NBA tena they're doing very good,yeye I wonder Yupo wapi now aday very sad kijana.
7ef55fb0dfd314005fc3aa3af4e1e4d5.jpg
09503686c30fe7607209f4e05658a464.jpg
Wewe na Hashimu nani ana maisha mazuri?
Labda useme kachezea career ila sio maisha.
 
Asilimia kubwa ya wachezaji wa NBA Wakiondoka hufilisika sanaaa....
 
arudi bongoland sasa. aje awakochi na madogo wengne mbona vipaji vingi tu pale makongo alipotoka yeye!!? btw wabongo tunajisahau na kujiachia.
 
Hivi mnaposema kachezea maisha mnamaanisha nini .............Hana pesa kafulia au ........... Au ni vile hayupo NBA ???
 
Nadhani mkuu hujakuwa mstaarabu kidogo kama ulitoa taarifa flan na watu hawajaelewa kuna haja gani tena ya mitusi.. Waelezee waelewe manake naamini mpaka unaanzisha huu uzi nia ilikuwa kupeleka taarifa flan sio mtihani wa nani anaweza tumia akili zaidi ya mwingine… ni mtizamo tu chif
Tatizo na yeye kacopy hajaelewa ndio maana amekua mkali si unakumbuka kipindi cha shule pale mwalimu anapoulizwa swali gumu anakua mbogo au utasikia hio ndio homework ya leo
 
Back
Top Bottom