The most profitable business idea (ufugaji samaki)

Asante mkuu kwa kutufungua macho, nimejiona mjinga sana niliishi sehemu yenye mifereji ya asili nikashindwa kufuga
 
Acha ujuaji ndugu. Hivi kweli unaweza kuuliza soko la nyama ya ng'ombe kwa mfano? Wewe fuga tu, wanunuzi ni masoko ya ndani na madalali. Tena wanakufuata huko huko shambani kwako.
Du. Hivi ukitaka kuingia kwenye biashara ya kuuza nyama hufanyi market research ya soko? Kwa sababu watu wanakula nyama basi una assume kuwa lazima soko litaendana na supply yako? Umenishtua sana.
 
Hao samaki artificial, watakuwa na virutubisho kweli, si ni kama broilers tu
 
Ungeandika bisiness plan kisha ufanye fund rising kana TALA au mr kuku.
Je ulishaji samaki sio ghali?
Je naweza kufuga samaki kiasili wakajilisha wenyewe kwa ecosystem kwenye bwawa dogo. Ninashamba lipo karibu na mto natamani niweke bwawa walau dogo kulisha familia yangu na wanakijiji wachache.
Je Baridi ya Njombe samaki tilapia anaimudu?
 
Mkuu business plan nimeandika Sana Hadi kufikia Sasa hivi Ila hela kutoka ndio imekuwa mtihani

Ulishaji wa samaki ni ghali Kama ukiwalisha kula cha kununua kutoka kwa supplier wanaoagiza kutoka nje Ila kama ukitengeneza mwenyewe gharama zake sio kubwa ni Kama tu gharama za kulisha kuku, ingredients ni Hizi Hizi za kawaida dagaa/uduvi, Pumba za mahindi/mchele, mashudu ya pamba/alizeti n.k unasaga na kuwalisha kikiwa kwenye powder form au pellets....

Kufuga samaki kiasili pia inawezekana, muhimu ni kurutubisha bwawa na kuweka idadi ya samaki sawa sawa na kiasi cha chakula kinachozalishwa kwenye hayo mazingira

Ndio inawezekana maeneo mengi ya Tanzania mazingira yake Yana ruhusu ufugaji samaki

Tuna weza tukafanya kitu Mkuu, unaweza ukinipigia tukaongea kwa kina ujue unaanzia wapi

Karibu
 
Sitaki kufanya kiutalaamu sana. Nataka bwawa dogo la kulisha familia tu sio biashara. Mimi kwetu mwisho wa reli nimezoea samaki sipendi nyama, huku Njombe kupata samaki hasa fresh ni ishu na ghali kidogo, sasa nataka nifuge wakula mimi hata kilo tano kwa mwexi sio mbaya.Nina eneo lipo mtoni kabisa na maji mda wote. Nitafuata ushauri wako.
 
Inawezekana ufuagi wa samaki hauna utofauti Sana na ufugaji wa kuku, changamoto ni kuwa hatuna utamudi huo Ila kwa nchi za Asia ni Jambo la kawaida

Nitakueleza utafanya, then utaleta ushuhuda wako hapa siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…