The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

kuna mzozo hapa mchezaji wa lyon kaanguka chini.. ni namba sita mgongoni..
 
imepigwa ndefu sana imemshinda kipre..
 
12692_471804779526550_1418369269_n.jpg


Kila la kheri majembe ya Azam Academy katika mitihani ya kidato cha 4.
Majembe hayo ni Makinda Franco, Bryson Raphael na Aishi Salum.
 
[h=3]MSERBIA KUWANOA MAKIPA WA AZAM[/h]

Na Mahmoud Zubeiry

AZAM FC, washindi waMedali tatu za Fedha, Ligi Kuu msimu uliopita, Kombe la Urafiki na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wameimarisha benchi lao la ufundi kwa kuleta kocha mpya kutoka Serbia, Slobodan.

Slobodan ametua Azam kwa kazi moja tu maalum, kuwanoa makipa wa timu hiyo inayo fukuzana na Simba kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Slobodan ni chaguo la kocha wa sasa wa Azam, kutoka Serbia pia, Boris Bunjak 'Boca' ambaye amerithi mikoba ya Muingereza Stewart Hall aliyefukuzwa Julai mwaka huu.


Source: BIN ZUBEIRY
 
[h=2]TENGA ataka Kamati zifanye kazi zake kwa kuzingatia Kanuni![/h]

TFF_LOGO12.png
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga, leo akizungumza na Waandishi wa Habari amezitaka Kamati za Uchaguzi kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
SOMA TAARIFA KAMIL TOKA TFF:
Release No. 165
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 9, 2012
TENGA AZITAKA KAMATI ZA UCHAGUZI KUSIMAMIA KANUNI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amezitaka Kamati za Uchaguzi kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema uongozi wa mpira wa miguu unahitaji uamuzi mgumu, hivyo Kamati za Uchaguzi ambazo zimeundwa kwa mujibu wa Katiba zinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na si kuangalia sura za watu.
Amepongeza kamati zilizosimamia uchaguzi kwa kufuata kanuni, na ingawa kila mtu ana haki ya kuongoza, jambo lolote lazima liwe na kanuni, kwani hata kwenye mikutano ya hadhara kuna kanuni.
"Huwezi kufika kwenye mkutano wa hadhara na wewe unaanzisha mkutano wako. Lazima kanuni ziheshimiwe ili kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki. Nini kimetokea kwenye maeneo ambayo kuna matatizo? Kila mwanachama wetu (mkoa/chama shiriki) ana Kamati ya Uchaguzi ambayo imeundwa kwa mujibu wa kanuni.
"Zile kamati hazitekelezi majukumu yake, unampitisha mtu unajua hana sifa unasema acha akafie mbele (Kamati ya Uchaguzi ya TFF). Kanuni zinasema jaza fomu mwenyewe, weka nakala za vyeti na si kwamba huyu tunamjua. Kanuni zinatakiwa zifuatwe, ukienda kinyume unaondolewa," amesema.
Amesisitiza kamati zifanye kazi kwa kufuata kanuni ili kusaidia mpira wa miguu kwani zimeundwa kihalali, kwa hiyo zisiogope kuengua hata walioziteua kama hawana sifa.
Pia Rais Tenga amezitaka Kamati za Utendaji na Sekretarieti kutoziingilia Kamati za Uchaguzi katika mchakato wa uchaguzi, badala yake zinatakiwa kuziwezesha tu (facilitation).
Amesema baadhi ya wagombea nao ni tatizo kwani wanaingia kwenye uchaguzi bila kuzielewa Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ni vizuri wakazielewa kwanza.
Rais Tenga amesema ni vizuri wanachama wote wakafanya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa TFF utakaofanyika Desemba mwaka huu ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa shirikisho.
Vilevile amewataka wadau kujitokeza kwa wingi kuwania uongozi kwenye chaguzi za vyama wanachama wa TFF, kwani mwitikio umeonekana kuwa mdogo kulinganisha na umaarufu wa mchezo wenyewe.
Amepongeza vyama vya mikoa ambavyo tayari vimefanya uchaguzi wao. Baadhi ya vyama hivyo ni Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara na Singida.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 
Azam FC kesho itashuka kwenye uwanja wa Jamhuri kujaribu kushinda mechi ya nne mfululizo na kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo hata mmoja pale itakapokwaana na Polisi Moro

Kocha Boris Bunjak amepania kushinda mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja mbovu wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kikosi cha Azam FC kiliwasili mjini Morogoro jana jioni na leo jioni walifanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Jamhuri.

Kikosi kinachotarajiwa kuanza kesho ni

GK- Mwadini Ally

DF- Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Moradi & Aggrey Morris

MD- Abdulhalim Humud, Jabir Aziz, Abubakar Salum & Himid Mao

ST- John Bocco, Kipre Tchetche
 

[h=3]SIMBA NA YANGA KUJA CHAMANZI[/h]

Uongozi wa Azam FC imetuma barua kwa TFF kuomba mchezo yake ya nyumbani dhidi ya Simba na Yanga ipigwe katika uwanja wa Chamanzi unaomilikiwa na Azam FC.

Azam FC hutumia uwanja wa Taifa kama uwanja wa nyumbani pale wanapocheza na Simba na Yanga na ratiba ya ligi kuu ya Vodacom inaonyesha Azam FC atatumia uwanja wa Taifa kama uwanja wake wa nyumbani pale watakapo kabiliana na timu hizo, ambazo ndizo uwanja wake wa nyumbani.

"Azam imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye uwanja wake wa Azam Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa," ilieleza taarifa ya TFF iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa; "Maombi hayo yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa kufanyika kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi."


Wakati huo huo kikosi cha Azam FC kipo mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya vodacom dhidi ya Polisi Moro utakaochezwa katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro hapo kesho.
 
[h=3]HIMID MAO: AZAM TUPO VIZURI KILA IDARA - SURE BOY NDIO KIUNGO BORA KABISA KWA SASA TANZANIA[/h]

Kuwasili kwa Boris Bunjuk kama kocha mkuu wa timu ya Azam FC, ni wazi kuwa wachezaji fulani watanufaika na wengine wataathiriwa na mabadiliko hayo. Azam inaonekana kucheza katika lugha moja na hata kimpira hawatofautiani sana kiuchezaji. Himid Mao Mkami kiungo chipukizi wa timu hiyo na mtoto wa mchezaji wa zamani, wa Taifa Star, Mao Mkami. Katika uchezaji wake, Himid amejitambulisha kama kiungo mwenye nguvu, wakati Baba yake alitamba zaidi akiwa na timu za Pamba ya Mwanza na Reli ya Morogoro na kujitambulisha kama 'ball dancer' mbele ya mashabiki wa soka nchi, kwa Himid ni tofauti kabisa yeye ana miaka mitano ndani ya Azam FC na anataka kuwa shujaa wa klabu yake.


SWALI; Tuzungumzie mambo ya ufundi na mbinu, unadhani nini siri ya ninyi kuwa na ukuta mgumu kwa msimu wa pili sasa, unadhani mabeki wenu ni bora zaidi nchini au kuna cha ziada ambacho kinawafanya muwe imara, kipi hicho?

HIMID; Kwanza kabisa timu yetu ni nzuri sana kuanzia mbele katikati na nyuma, pia tuna mabeki na kipa mzuri lakin siri ya kuwa na ukuta mgumu ni wachezaj wote kujitolea 100% tunapokuwa uwanjani.
SWALI; Ninapoitazama Azam kiujumla inaonekana ni timu iliyokamilika hasa na yenye wachezaji mahiri, pamoja na ubora wenu unadhani nini ni udhaifu wenu na kipi ambacho ungependa kuwaambia wenzako kuhusu hilo la udhaifu ili mpate kuwa na matokeo bora zaidi katika ligi na michuano ya kimataifa?



HIMID; Kweli timu yetu ipo vizuri kila idara, sidhan kama kuna mapungufu sehemu yeyote kwakuwa hatujapoteza mchezo wowote hadi sasa, nafikiri tunatakiwa kupata magoli mengi zaidi ili tujiweke katika mazingira mazuri katika ligi na mashindano ya kimataifa .

SWALI; Unamzungumziaje kocha, Boris mbinu zake na malengo ya klabu vinaendana?

Coach ni mzuri pia Ana mbinu nzuri za ushindi ndiyo maana tuna matokeo mazuri kwa ligi

SWALI; Ipi silaha yako uwapo uwanjani?

HIMID; Silaha yangu ni uwezo mkubwa wa kukaba.

SWALI; Kiungo gani bora ambaye umewahi kucheza naye timu moja?

HIMID; Kiungo bora kuwahi kucheza nae ni Sureboy, ana kipaji cha hali ya juu,

SWALI; Umesema silaha yako kubwa ni uwezo wa kukaba, unadhani nini unahitaji kuongeza katika mchezo wako ili uwe bora zaidi?

HIMID; Nafikiri ni mazoez ndio nahitaji kuongeza ili niwe bora zaidi

SWALI; Sifa tano ambazo zinakufanya uwe katika kikosi cha kwanza cha Azam?

HIMID; 1. Uvumilivu,
2 kujituma,
3. Kushirikiana vizuri na wenzangu,
4. Kufuata maelekezo ya kocha,
5. Support kutoka kwa Mungu, wazazi, familia yangu na rafiki zangu

SWALI; Polisi Moro ambayo mnacheza nayo jumamosi hii, haijashinda mchezo wowote kati ya mitano iliyocheza, unafikiria itakuwa mechi ya aina gani kwani wewe unaijua vizuri Polisi?

HIMID; Mechi itakua ngumu sana, tumejiandaa vya kutosha nafikiri tutapata matokeo mazuri


SWALI; Kwa msimu huu umeshacheza michezo mingapi na umetengeneza ama kufunga mabao mara ngapi?


HIMID; Nimecheza mechi 6, sijafunga mara nyingi nakua nyuma kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi.

Swali: Unazungumziaje mwenendo wa timu nne za juu katika ligi, ni nini taswira ya ligi uionavyo hadi kufikia raundi ya kumi?


HIMID; Ushindani ni mkubwa sana kwa timu nne za juu, lakin naweza kusema ni kwa timu zote, ligi inazidi kuwa ngumu na ikifika round ya kumi ndio itazidi kuwa ngumu na ushindani utaongezeka

SWALI; Kipi kikosi bora ambacho umewahi kukichezea, ukiwa Azam au timu ya Taifa?

HIMID; Vikosi vyote vilikua bora........


SWALI; Nini mtazamo wako kuhusiana na soka la Tanzania?
HIMID; Soka la Tanzania liko vizuri, sema inahitajika jitihada za makusudi ili kuliinua zaidi..
 
Back
Top Bottom