The Official Azam FC Thread

Maneno ya Super Coach Julio wa Mwadui kuhusu Azam FC, Simba na Young Africans kubebwa na marefa pia wachezaji wa Tanzania kukosa focus mchezaji akitolewa kwa kadi nyekundu

Baada ya kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha wa Mwadui FC kaongea haya

Source: Millard Ayo
 
Mbona kama kawa Msemaji Mkuu wa Club ya Mwadui
 
April 15, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By ppkahemele

Kapombe atoka hospitali, arejea Bongo

BEKI kisiki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, amerejea nchini jana jioni baada ya wataalamu wa Hospitali ya Morningside Mediclinic ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini kuridhishwa na maendeleo ya afya yake.

Kapombe alikuwa jijini humo katika hospitali hiyo tokea Alhamisi iliyopita akipatiwa matibabu baada ya kugundulika anasumbuliwa na ugonjwa wa Pulmonary Embolism (donge la damu kuziba mishipa ya damu katika mapafu) Pulmonary embolism: Take measures to lower your risk Causes - Mayo Clinic na sasa afya yake imezidi kuimarika hali iliyopelekea kuruhusiwa kutoka hospitali.

Daktari Mkuu wa Azam FC, Dr. Juma Mwimbe, ameuthibitshia mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz kuhusu kurejea kwa Kapombe na amedai kuwa kwa sasa yupo kwenye mapumziko nyumbani kwake akiendelea na dozi ya matibabu aliyopewa na wataalamu hao kutoka Afrika Kusini na huenda akarejea uwanjani wakati Azam FC itakapoanza kujiandaa na msimu ujao, lakini bado atakuwa akiendela na dozi aliyopewa kwani itamchukua si chini ya mwaka mmoja hadi miwili hadi kuweza kumaliza matibabu yote.
Source: Kapombe atoka hospitali, arejea Bongo | The Official Website of Azam Football Club

More info Pulmonary Embolism :

Blood clots are more likely to form in your legs during periods of inactivity, such as:

  • Bed rest. Being confined to bed for an extended period after surgery, a heart attack, leg fracture, trauma or any serious illness makes you far more vulnerable to blood clots. When the lower extremities are horizontal for long periods of time, the flow of venous blood slows and blood pools in the legs.
  • Long journeys. Sitting in a cramped position during lengthy plane or car trips slows blood flow, which contributes to the formation of clots in your legs. Pulmonary embolism: Take measures to lower your risk Risk factors - Mayo Clinic
 
April 18, 2016
Tunis, Tunisia

Kocha Stewart Hall ushindi lazima kesho kwa Azam FC, aliyasema hayo wakati wakiwaelekeza vijana wake wa Azam FC ktk darasa maalum kupitia video kuona mapungufu ya Esperance Sportive de Tunis 1919.

 
April 19, 2016
Tunis, Tunisia

Habari na AFP news (Agence France-Presse) Shirika la Habari Ufaransa Home | AFP.com

''Wavaa jezi za michirizi ya 'Dhahabu na Damu' a.k.a Esperance wanatarajia ushindi''



Esperance Sportive de Tunis ya Tunisia wameshashinda kombe la CAF mara tano na hivyo kujinasibu kuwa ushindi ni lazima. Pia timu hiyo ya Tunisia inatajwa kama mojawapo ya timu katika michuano hiyo inayotegemewa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Timu hiyo yenye makao yake katika jiji la Tunis na jezi zao za michirizi rangi ya ''Dhahabu na Damu'' wanajivunia kikosi kilichosheheni wachezaji hodari toka mataifa mbalimbali.

Kwa upande wa Azam FC timu ya Tanzania inayoshiriki kwa mara ya tatu michuano ya CAF haijawahi kupenye zaidi ya ngazi ya timu kumi na sita bora za mwisho ya michuano hiyo ya CAF.

Itakuwa ni historia itakayo tikisa mchezo za soka Afrika kama Azam FC wataweza kuigoa timu kigogo ya Esperance katika uwanja wake wa nyumbani wa Stade Rades jijini Tunis.

Pia pamoja na uzoefu wa kimataifa wa kocha Stewart Hall wa Azam FC kuzifundisha timu za India , Saint Vincent and the Grenadines, Zanzibar and Kenya hali itakuwa ngumu kwake kutokana na Azam FC kuwakosa wachezaji wazoefu kutokana na kuwa majeruhi au wagonjwa.

Mshambuliaji Mzaliwa wa Ivory Coast Kipre Tchetche, aliyefunga hat trick katika michezo ya awali dhini ya BidVest Wits ya Afrika ya Kusini pia ni majeruhi. Pia Mu-Ivory-Coast beki kisiki Serge Wawa ni majeruhi huku Mtanzania Shomari Kapombe mlinzi wa kulia ndiyo kwanza amerejea toka Afrika ya Kusini kwa matibabu pia atakosekana katika pambano la leo jioni.

Lakini habari za faraja kwa Kocha Hall ni kuwa mlinzi Erasto Nyoni, kiungo Salum Aboubakar na nahodha aliye pia mshambuliaji John Bocco wamepona maumivu na wanatarajiwa kucheza katika mechi ya leo.

Tunajua hakuna changamoto kubwa kama kucheza na timu nzuri kigogo Afrika ya Esperance nyumbani kwao Tunis, lakini tunaimani Azam FC tutaibuka na ushindi Kocha Hall anahitimisha kuelezea mtihani wa leo

Mchezaji wa Esperance , Haythem Jouini alifunga bao la kuongoza kipindi cha kwanza jijini Dar es Salaam lililokuja kusawazishwa kwa magoli ya haraka haraka ya Azam FC kupitia kwa Farid Mussa na Ramadhani Singano kipindi cha pili cha mchezo.
AZAM VS ESPERANCE HIGHLIGHTS 10 April 2016
Source: Soka360 TV youtube

Klabu ya Zanaco ya Zambia pia itacheza Tunisia, lakini ipo katika hali ngumu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na timu ya Stade Gabesien.

Source: The 'Blood and Gold' among the favourites
 
Waarabu wana uoga na wasiwasi mkubwa maana Azam FC imekuwa ndiyo gumzo ktk jiji la Tunis miongoni mwa wa-Tunisia, cheki waandishi wa habari wanavyomkaba Kocha Ammar Souayah wa Esperance awape uhakika wa leo maana leo-ni-leo - hakuna kesho Kocha huyu kibarua chake kinaweza ota mbawa mashabikiwa Easperance Sportive de Tunis 1919 hawana uvumilivu:


Source: Official EST Web Site - Taraji | Espérance sportive de tunis
 
Asilimia 100 Esperance vs Azam FC 'live'
---------------------------------------------------
Mpaka sasa ni asilimia 100 kuwa mechi kati ya Azam FC na Esperance ya Tunisia itakayofanyika leo saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, itarushwa moja kwa moja kupitia Kingamuzi cha Azam TV (Azam TWO).
Hivyo mashabiki wa Azam FC pamoja na Watanzania kwa ujumla kaeni mkao wa kula kutazama mpambano huo, kama ulikuwa ujalipia Kingamuzi cha Azam TV, tafadhali lipia haraka ili uweze kushuhudia mchezo huo.
Kama hiyo haitoshi, ukurasa huu utakuwa ukikupa matokeo 'live' kwa kila kinachojiri ndani ya Uwanja wa Olympique de Rades.

Kitoabu

Azam wamethibitisha kwamba wataonyesha. ni kuanzia SAA tatu usiku, Tuwe pamoja

BACK TANGANYIKA
 
Leo kigogo Esperance Sportive de Tunis ya mwaka 1919 lazima wangolewe katka mashindano haya na mechi hii kuingia katika vitabu vya historia ya soka barani Afrika kuwa sasa Azam FC iliyoanzishwa mwaka 2007 ni kiboko ya klabu kongwe..
 
mkuu mbona kimya azam tv?
 
TV Nationale 2 Tunisie tazama live Wataniya 2 live online | Tunisie 14

Dakika ya 22'' Yallah! Yallah! huyu Coulibaly wa Esperance hatari sana !
Dakika ta 23'' Krosi ya Esperance inangonga mtambaa wa juu wa goli la Azam!
Dakika 25'' Jamaa wanaweka pressure kubwa kwa Azam FC lakini wachezaji wa Azam FC wametulia hawababaiki
Dakika 29'' Manula anadaka shuti kali la shambulizi la Esperance
Dakika 31'' Hawa jamaa Esperance wanacheza kwa kukamia mpira upo half ya pitch ubabe wa Azam FC tu
Dakika 44'' Hongera kwa wachezaji wa Azam FC hasa safu ya ulinzi pamoja na kipa Aishi Manula ni jihadi kwenda mbele Esperance hawaamini wanayoona!
Dakika 45'' shuti! Aisha Manula anaokoa inakuwa kona
Dakika 45 + 1 Mpira ni mapumziko
Esperance 0 - Azam FC 0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…