April 19, 2016
Tunis, Tunisia
Habari na AFP news (Agence France-Presse) Shirika la Habari Ufaransa
Home | AFP.com
''Wavaa jezi za michirizi ya 'Dhahabu na Damu' a.k.a Esperance wanatarajia ushindi''
Esperance Sportive de Tunis ya Tunisia wameshashinda kombe la CAF mara tano na hivyo kujinasibu kuwa ushindi ni lazima. Pia timu hiyo ya Tunisia inatajwa kama mojawapo ya timu katika michuano hiyo inayotegemewa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Timu hiyo yenye makao yake katika jiji la Tunis na jezi zao za michirizi rangi ya ''Dhahabu na Damu'' wanajivunia kikosi kilichosheheni wachezaji hodari toka mataifa mbalimbali.
Kwa upande wa Azam FC timu ya Tanzania inayoshiriki kwa mara ya tatu michuano ya CAF haijawahi kupenye zaidi ya ngazi ya timu kumi na sita bora za mwisho ya michuano hiyo ya CAF.
Itakuwa ni historia itakayo tikisa mchezo za soka Afrika kama Azam FC wataweza kuigoa timu kigogo ya Esperance katika uwanja wake wa nyumbani wa Stade Rades jijini Tunis.
Pia pamoja na uzoefu wa kimataifa wa kocha Stewart Hall wa Azam FC kuzifundisha timu za India , Saint Vincent and the Grenadines, Zanzibar and Kenya hali itakuwa ngumu kwake kutokana na Azam FC kuwakosa wachezaji wazoefu kutokana na kuwa majeruhi au wagonjwa.
Mshambuliaji Mzaliwa wa Ivory Coast Kipre Tchetche, aliyefunga hat trick katika michezo ya awali dhini ya BidVest Wits ya Afrika ya Kusini pia ni majeruhi. Pia Mu-Ivory-Coast beki kisiki Serge Wawa ni majeruhi huku Mtanzania Shomari Kapombe mlinzi wa kulia ndiyo kwanza amerejea toka Afrika ya Kusini kwa matibabu pia atakosekana katika pambano la leo jioni.
Lakini habari za faraja kwa Kocha Hall ni kuwa mlinzi Erasto Nyoni, kiungo Salum Aboubakar na nahodha aliye pia mshambuliaji John Bocco wamepona maumivu na wanatarajiwa kucheza katika mechi ya leo.
Tunajua hakuna changamoto kubwa kama kucheza na timu nzuri kigogo Afrika ya Esperance nyumbani kwao Tunis, lakini tunaimani Azam FC tutaibuka na ushindi Kocha Hall anahitimisha kuelezea mtihani wa leo
Mchezaji wa Esperance , Haythem Jouini alifunga bao la kuongoza kipindi cha kwanza jijini Dar es Salaam lililokuja kusawazishwa kwa magoli ya haraka haraka ya Azam FC kupitia kwa Farid Mussa na Ramadhani Singano kipindi cha pili cha mchezo.
AZAM VS ESPERANCE HIGHLIGHTS 10 April 2016
Source: Soka360 TV youtube
Klabu ya Zanaco ya Zambia pia itacheza Tunisia, lakini ipo katika hali ngumu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na timu ya Stade Gabesien.
Source:
The 'Blood and Gold' among the favourites