The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

HANS POPPE: AZAM WATAKULA JEURI YAO
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema Azam FC inalazimika kuvuna matunda ya ukaidi wao kwa kwenda kucheza ‘bonanza’ Zambia na kuacha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiendelea.

“Hatukatai Azam na Yanga kupewa muda wa maandalizi wa mashindano yao ya Afrika, lakini huko nyuma walikwishakosea kwa kwenda kucheza bonanza na kuacha ligi,”.

“Matokeo yake sasa wanazidi kulundikiwa mechi za viporo na kupoteza ladha ya ligi, kama wasingekwenda Zambia, wasingekuwa na viporo vingi, ila kwa kuwa walikaidi mawazo ya timu nyingine, sasa wacheze Ligi,”amesema Hans Poppe.

Na sasa Azam FC ipo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Aprili 10 watamenyana na Esperance ya Tunisa Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili.

Wakiwa wanahitaji muda mzuri wa maandalizi, Azam FC watalazimika kucheza mechi za Kombe la TFF na za Ligi mbili katika wiki ambayo watacheza na Esperance.


Simba SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu kwa sasa ikiwa na pointi 57, ikifuatiwa na Azam na Yanga zenye 50 kila moja, lakini Wekundu wa Msimbazi wana mechi tatu zaidi ya wapinzani wao hao kwenye mbio za ubingwa (24-21).

Source: Kwa Hisani Kubwa ya Bin Zubeiry HANS POPPE: AZAM WATAKULA JEURI YAO | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
 
Azam FC: Tumefuata pointi tatu Mwanza
By ppkahemele on April 01, 2016
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imewasili salama jijini Mwanza ikiwa na ari kubwa ya kuzoa pointi tatu dhidi ya wenyeji wao Toto African katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika ndani ya Uwanja wa Kirumba jijini humo keshokutwa Jumapili (Aprili 3).

Azam FC iliondoka jijini Dar es Salaam saa 9.20 mchana ikiwa na kikosi kamili kasoro beki wa kushoto Gadiel Michael anayeendelea na programu ya kuondoa majeraha yake ya goti yanayomsumbua na imefikia katika Hoteli ya Mipa iliyopo jijini hapa.
IMG_2739.JPG


Akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz muda mchache kabla ya kikosi hicho akijakwea ndege kuelekea mkoani humo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, alisema wamekwenda na lengo moja tu la kuchukua pointi tatu katika mchezo huo.

“Ligi imefikia sehemu muhimu sana, kukusanya pointi ni jambo la msingi sana, tukishinda mechi zet zote zilizobakia tuna uhakika na ubingwa wa ligi, hivyo tumelenga pointi tatu dhidi ya Toto,” alisema.

Akizungumzia programu watakayoanza nayo jijini hapa kabla ya mchezo huo, Hall alisema watafanya mazoezi kesho ndani ya uwanja huo na wanachosubiria ni kutajiwa muda na wenyeji wao.

Azam FC kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 50 sawa na Yanga iliyo juu yake, lakini timu zote hizo zimezidiwa mechi tatu na Simba inayoongoza ligi kwa pointi 57. Azam FC: Tumefuata pointi tatu Mwanza | The Official Website of Azam Football Club
 
April 3, 2016
Mwanza , Tanzania

Matokeo : Toto Afrika 1 - Azam 1

John Bocco akiifungia Azam FC dakika ya 23 na Toto Afrika wakisawazisha dakika ya 40 kupitia Waziri Juma. Hali ya mchezo ilikuwa na changamto kubwa kufuatia mvua kubwa iliyokuwa imenyesha na kuufanya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kujaa maji.
IMG_3377.JPG


Azam FC wamefikisha pointi 51 na kuendelea kushika nafasi ya tatu katika ligi VPL Tanzania. Azam wana viporo vya mechi mbili katika ligi hiyo huku Simba SC ikiwa kileleni na pointi 57.

Jumatano April 6, 2016 Azam FC watawakaribisha Ndada FC ktk uwanja wa Azam Complex , Chamazi, Dar-es-Salaam. Hall: Mechi v Toto ilibidi ihairishwe dakika 20 za mwanzo | The Official Website of Azam Football Club
 
Azam FC yaianzia kazi Esperance
By ppkahemele on April 03, 2016

Uongozi wa Azam FC katika kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi zote mbili, tayari Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba na Kocha Msaidizi, Dennis Kitambi, wapo jijini Tunis kuwasoma wapinzani wao hao, ikiwemo kuandaa mazingira watakapofikia wachezaji pindi timu itakapowasili nchini humo kwa mchezo wa marudiano.

Kama hiyo haitoshi leo jioni walikuwepo uwanjani kushuhudia ‘live’ mechi ya Esperance waliokuwa wakipambana na mahasimu wao, Club African iliyofanyika Uwanja wa Stade Olympique De Rades unaotumiwa na Esperance, ambao wameibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mbali na kuangalia mchezo huo, tayari benchi la ufundi la Azam FC limepata DVD za mechi zilizopita na wamefanya hivyo ili kuwaandaa wachezaji kimbinu kwa ajili ya kumenyana vema na waarabu hao.

Azam FC itaanza kucheza na miamba hiyo nyumbani Aprili 10 mwaka huu kabla ya kuelekea jijini Tunis kwa ajili ya mchezo wa marudiano, ambao utatoa mshindi wa jumla wa kupenya hadi hatua ya mwisho ya mchujo na kutinga hatua ya robo fainali (makundi). Azam FC yaianzia kazi Esperance | The Official Website of Azam Football Club
 
April 6 , 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

Matokeo : Azam FC 2 - Ndanda FC 2

Timu ya Azam Fc imelazimishwa matokeo ya sare katika mchezo wake na Ndanda Fc ktk uwanja wa nyumbani wa Azam Complex, Chamazi Dar -es- Salaam .

Mabao katika mchezo huo wa Vodacom Premier league Tanzania kwa Azam yalifungwa na Ramadhani Singano na Didier Kavumbagu. Wakati ya Ndanda yatiwa kimiani moja kwa njia ya penalti na Atupele Green, huku Hemed Msumi akisawazisha matokeo kwa bao la pili.

Azam Fc imefikisha pointi 53 nakupanda mpaka nafasi ya pili ktk msimamo wa ligi ya VPL Tanzania 2015/2016.
 
Jana wameonyesha kiwanngo cha chini sana kweli hatuko serious na kuchukua kombe
 
MATCH PREVIEW: Sure Boy, Kapombe nje Azam FC v Esperance
By ppkahemele on April 10, 2016

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Leo Jumapili itarusha karata yake ya kwanza muhimu kwenye raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, pale itakapowakaribisha Esperance ya Tunisia katika Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Kapombe hivi sasa bado yupo nchini Afrika Kusini akiendelea na vipimo kwa ajili ya kubaini tatizo linalomsumbua kutokana na kubanwa mbavu huku Sure Boy akisumbulia na majeraha ya nyonga aliyoyapata wakati wa mchezo wa Ndanda.

Akizungumza na mtandao wa www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya Jumamosi April 9, 2016 asubuhi Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, alisema licha ya kuwakosa nyota wake hao wawili amejipanga kuja na mfumo mpya utakao wawezesha kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Esperance.

“Nitakuja na mfumo mpya kwa ajili ya kupambana na hali hiyo ambao utaanza tukiwa na mabeki wanne ambao utakuwa ni mzuri wa kupambana na mfumo wa 4-2-3-1 wanaotumia wapinzani wetu Esperance.

Rekodi ya Azam FC (Azam Complex)
Azam FC bado ina rekodi nzuri kila ikitumia uwanja wake wa nyumbani kwani mpaka sasa kwenye michuano yote ya kimataifa haijawahi kufungwa ndani ya dimba hilo tokea waanze kuutumia kwa mechi hizo mwaka juzi.

Viingilio Azam FC v Esperance

Kiingilio ni Sh. 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko. Kwa majukwaa ya watu maalumu (VIP), kiingilio cha VIP A kitakuwa ni Sh. 20,000 tu huku VIP B kikiwa ni Sh. 10,000.

Tiketi zote hizo zitapatikana kuanzia Leo Jumapili saa 3.00 asubuhi kwa kuuzwa kwenye Ukumbi wa Dar Live Mbagala Rangi Tatu na kituo kingine kitakuwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam itakapofanyika mechi hiyo.

Source: MATCH PREVIEW: Sure Boy, Kapombe nje Azam FC v Esperance | The Official Website of Azam Football Club
 
Published in 2016
SEKILOJO CHAMBUA, Mchezaji wa zamani wa Yanga aichambua Azam FC na klabu ya Yanga dhidi ya waarabu. Mahojiano na Mlimani TV ya Dsm , Tanzania

Source: hamza fumo wa youtube
 
Full time final score
Azam FC 2 - Esperance de Sportive Tunis 1
Scorers for Azam FC were Farid on the 68'' minutes and Singano 69'' minutes while Esperance scored early in the game at 33'' minutes.


Source: ArtiseTunisienVEVO youtube
 
Video
Caf 2016 Azam FC vs Esperance Sportive de Tunis 10/04/2016 dans Dar-es-Salaam, Tanzanie

Source: ArtisteTunisienVEVO youtube
 
Azam's Farid Musa goal scored in the Azam FC vs Esperance Sportive de Tunis, AFRICA's CAF Competition match 10.04.2016 held in Dar-es-Salaam, Tanzania.


Source: ArtiseTunisienVevo
 
Singano's second goal for the Tanzanian team Azam FC on the 69th minute of the game between Azam FC vs Esperance Sportive de Tunis

Source: ArtiseTunisienVEVO
 
April 11, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania


IMG_4572.JPG

Picha: Farid Musa wa Azam FC (kushoto) akimiliki mpira mbele ya walinzi wa Esperance Sportive de Tunis.

Farid: Haikuwa rahisi, tumepambana kinoma

By ppkahemele
Azam FC
WINGA machachari wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa walichofanya jana walipoichapa Esperance ya Tunisia mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF.

Farid, 19, alikuwa katika kiwango bora jana akifunga bao la kusawazisha dakika ya 69 lililowarudisha mchezoni Azam FC na kupata bao la ushindi ndani ya dakika moja lililofungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ dakika ya 70.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Farid alisema kuwa haikuwa kazi rahisi na wamepambana kinoma kutokana na Esperance Sportive de Tunis kuwa na uzoefu mkubwa kwenye michuano hiyo na pia ukizingatia wamewaacha mbali kisoka.

Source: ArtiseTunisienVEVO youtube

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kucheza vema leo (jana) na kuifungia bao timu yangu, haikuwa kazi rahisi kufanya hivyo tumepambana sana hadi kupata matokeo hayo,” alisema.

Azam FC ina nafasi Tunis

Farid alizungumzia pia mchezo wa marudiano utakaofanyika Aprili 20 mwaka huu jijini Tunis, Tunisia na kudai kuwa wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri ugenini.

“Bado nina uhakika wa asilimia 100 kwa Azam FC kufanya vizuri ugenini, na hii itawezekana kama watu watajituma kama tulivyojituma hapa kipindi cha pili, vilevile kupeana moyo naamini tutafanikiwa,” alisema.

Source: Farid: Haikuwa rahisi, tumepambana kinoma | The Official Website of Azam Football Club
 
April 12, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

Draw ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), Semi Finals

Tarehe 24.04.2016 mechi za mzunguko wa kwanza itakuwa , Mwadui kuikaribisha Azam FC huko Shinyanga na Coastal Union itawakaribisha Young Africans ktk uwanja wa Mkwakwani.

Azam itarejea Tanzania tarehe 22.04.2016 kutoka Tunis, Tunisia baada ya kupambana na Esperance Sportive de Tunis ktk mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF na siku mbili baadaye kutua Shinyanga kwa mchezo wa tarehe 24.04.2016 ktk kombe la FA kukumbana na Mwadui Football Club.

Semi Finals timu zinazoanza nyumbani 24.04.2016
Mwadui FC vs Azam FC
Coastal Union Vs Young Africans

Source: Watch Azam Tv Live Online
 
April 13, 2016
Turiani Morogoro
Tanzania

Matokeo mechi ligi ya VPL (Vodacom Premier League) Mtibwa 0 - Azam FC 1

By ppkahemele
Azam FC, imezidi kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 katika Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro jioni ya leo.

Ushindi huo wa Azam FC umekuja wakati ikitoka kupata sare mbili mfululizo kwenye mechi zilizopita za ligi dhidi ya Toto Africans (1-1) na Ndanda (2-2).

Shukrani za kipekee ziende kwa nahodha John Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga bao hilo pekee kwa njia ya mkwaju wa penalti na kuihakikishia Azam FC pointi zote tatu muhimu ugenini. Ushindi wa Azam umeifanya kufikisha jumla ya pointi 55 katika nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi mbili na Simba inayoongoza kileleni na pointi moja dhidi ya Yanga, ambayo ipo nyuma mchezo mmoja.

Kikosi cha Azam FC kwa mara ya kwanza kwenye ligi, leo kilikuwa bila beki kisiki Pascal Wawa, ambaye amekusanya kadi tatu za njano na akiwa katika programu ya kuwekwa fiti kwa ajili mchezo ujao dhidi ya Esperance, nafasi yake ilichukuliwa na Racine Diouf.

Dakika ya 16 beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vincent ‘Dante’ alifanya kazi ya ziada kuinyima bao Azam FC baada ya kuokoa mpira kwenye mstari kufuatia kichwa kilichopigwa na Bocco, aliyetumia uzembe wa kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed aliyeuokoa vibaya mpira wakati akiruka naye juu.

Azam FC wangeweza kuondoka na mabao mawili kipindi cha kwanza kama wachezaji wake Kipre Tchetche na beki Racine Diouf wangekuwa makini kutumia nafasi walizopata na hivyo .

Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana Kipindi cha pili kilianza kwa benchi la ufundi la Azam FC chini ya Stewart Hall, kufanya mabadiliko ya kutoka Diouf na nafasi yake kuchukuliwa na Abdallah Kheri, lengo likiwa ni kuimarisha eneo la ulinzi.

Dakika ya 61 Tchetche alifanya kazi ya ziada kumkimbiza Andrew Vincent ‘Dante’ wa Mtibwa Sugar na kupiga krosi ya hatari pembeni kidogo ya eneo la 18 na beki huyo alijikuta akiunawa mpira huo katika harakati za kuokoa na mwamuzi Alex Mahagi kutoka Mwanza kuamuru penalty ipigwe langoni mwa Wakata miwa hao.

Dakika ya 90 mwamuzi Mahagi alimuonyesha kadi nyekundu kiungo wa Azam FC, Himid Mao.baada ya kumuonyesha mwamuzi kutokukubaliana na namna alivyofanyiwa na watu wa huduma ya kwanza waliompandisha vibaya kwenye machela kufuatia kudondoka chini kufuatia kupigwa usoni na mchezaji wa Mtibwa Sugar.

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kitaanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kesho saa 1 asubuhi na mara moja kitafikia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF CF dhidi ya Esperance Sportive de Tunis utakaofanyika jijini Tunis,Tunisia Aprili 19 mwaka huu.

Kikosi cha Azam FC leo:

Aishi Manula, Wazir Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Racine Diouf/Abdallah Kheri dk 46, Himid Mao, Michael Bolou/Jean Mugiraneza dk 82, Frank Domayo, Ramadhan Singano, John Bocco, Kipre Tchetche/Allan Wanga dk 79

Source: Azam FC yaibwaga Mtibwa Manungu | The Official Website of Azam Football Club
 
Back
Top Bottom