The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

Timu ya Azam FC imemkaribisha kocha wake wa zamani Stewart Hall kwa kuifunga Coastal Union 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo, Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Azam FC leo iliongozwa na kocha huyo kwenye benchi la ufundi ikiwa ni siku moja baada ya kuwasili kuifundisha timu hiyo, pia ni siku nne tangu kusitisha mkataba wa kocha Boris Bunjak 'Boca' aliyeiongoza timu hiyo tangu kuanza kwa ligi kuu ya Vodacom (VPL) 2012-2013.

Katika mchezo huo wachezaji walicheza kiwango kizuri wakitumia mtindo wa kocha huyo ambao ni kucheza mipira ya chini huku wakifanya mashambulizi.

Azam walipata bao la kwanza dk 22 ya mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji Gaudence Mwaikimba aliyefunga kwa kichwa akimalizia krosi ya Samih Nuhu

Bao hilo la Mwaikimba ni goli lake la kwanza kwenye ligi kuu tangu asajiliwe na klabu hiyo katikati ya msimu uliopita akitokea Moro United.

Dk 36 mshambuliaji Kipre Tchetche alionyesha umahiri wake kwa kuipatia Azam FC goli bili baada ya kuwapita mabeki na kumzungusha kipa wa Coastal Union, Jackson Chove na kuachia shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Kipindi cha kwanza kilikua cha Azam FC dk 45 Khamis Mcha Viali aliipachika goli la tatu kwa shuti kali lililogonga mwamba na kuingia wavuni akimuacha kipa wa Coastal asijue la kufanya, timu zilienda mapumziko Azam FC ikiwa mbele kwa 3-0 dhidi ya Coastal.

Katika kipindi cha pili kasi ya Azam FC iliongezeka na kuongeza goli la nne lililowekwa wavuni na Mcha aliemalizia mpira wa mwisho wa Salum Abubakar 'Sure Boy'.

Goli pekee la Coastal lilifungwa na Jerry Santo katika dk 87 akitumia uzembe wa beki ya Azam FC na kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni wachezaji wa Coastal Jamal Machelenga na Daniel Lyanga watajutia nafasi za wazi walizopata kwa kupiga mipira nje na mwingine kuokolewa na kipa Mwadini Aly wa Azam FC.

Ushindi huo wa 4-1 umeipeleka Azam FC kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 21 nyuma ya Simba na Yanga zenye pointi 23 kila moja, lakini Azam FC bado wanamchezo mmoja mkononi.

Baada ya kumalizika mchezo huo kocha Stewart aliwapongeza wachezaji wake na uongozi mzima wa Azam FC kwa kurejea katika kikosi hicho na kuahidi kuendeleza mapambano katika mechi zijazo ikiwepo mechi ya Jumapili dhidi ya Yanga itakayochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Azam FC kilichomkaribisha kocha huyo Mwadini Ally, Ibrahim Shikanda, Said Morad, Agrey Moris, Samih Haji Nuhu, Jabir Aziz, Michael Bolou/Ibrahim Mwaipopo 69', Salum Abubakar 'Sure Boy'/Himid Mao 76', Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim 'Babi', Tchetche Kipre na Khamis Mcha Viali.






 
vp mdau mbna updates ziliishia hapa au bundle lilikata

Mabao mawili ya Dedier Kavumbangu na Khamis Kiiza jana yalipeperusha tena ndoto za Azam FC za kukaa kileleni kwa mara ya nne msimu huu.

Mara ya kwanza ilikuwa ni katika mechi dhidi ya Tanzani Prisons ambapo endapo Azam FC ingeshinda basi ingekwea hadi kileleni

Mara ya pili ilikuwa ni katika sare dhidi ya Ruvu Shooting Stars na baadaye ilipopoteza dhidi ya Simba kwa kufungwa 3-1.

Azam FC inabaki na pointi 21 na michezo miwili mkononi huku yanga ikitinga kileleni kwa mara ya kwanza kwa kufikisha pointi 26

Ligi hiyo itaendelea tena jumatano hii ambapo Azam FC itakwaana na JKT Oljoro Chamazi Dar es Salaam
Yanga 2-0 Azam, Yanga yatinga kileleni | The Official Website of Azam Football Club
 
King Abedi Pele jana alitua kwenye kituo cha soka cha Azam FC akiwa ameambatana na Wajumbe wenzake wa FIFA Ashford Mamelody na Emanuel ambapo wote walisema Wamezunguka Afrika nzima lakini hawajawahi kuona kituo kilichojitosheleza kama cha Azam FC.

Usikose kuangalia ziara hii kupitia Azam FC TV Show leo saa tatu kamili usiku Chanel 10



 
Game is over Azam fc 1 - 0 JKT Oljoro mfungaji ni :A S soccer:kipre Tchetche na Himid Mao akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada yakupewa kadi mbili za njano..
 
King Abedi Pele jana alitua kwenye kituo cha soka cha Azam FC akiwa ameambatana na Wajumbe wenzake wa FIFA Ashford Mamelody na Emanuel ambapo wote walisema Wamezunguka Afrika nzima lakini hawajawahi kuona kituo kilichojitosheleza kama cha Azam FC.

Usikose kuangalia ziara hii kupitia Azam FC TV Show leo saa tatu kamili usiku Chanel 10




Angalia ziara hii kupitia Azam FC TV Show Channel 10
  • Abedi Pele asifia uwanja wa Chamzi na 'facilities' zote kwa wanasoka wa soka wa klabu ya Azam FC
  • Alinganisha Azam FC facilities na alizoona Ulaya
  • Vision ya Azam FC ni ya kuigwa
  • Abeid Pele anasema baada ya kufika ktk makao makuu ya Azam Fc ni yeye ambaye sasa anajifunza mbinu bora za Azam Fc badala ya Azam FC kujifunza kwake
  • Abeid Pele anasema nchi yake ya Ghana ina yakujifunza toka Azam Fc na pia Azam FC kujifunza jinsi ya kuwachochea wanasoka wa Azam FC kuwa na hamu ya kufanya vizuri zaidi kama nchi za Ghana, Nigeria, Cameroun, Egypt, Tunisia n.k

 
Last edited by a moderator:
TANZIA
Azam FC inatangaza msiba wa mchua misuli (Masseur) wake Khamis Mbembe uliotokea leo saa tano asubuhi... Khamis Mbembe alikuwa mcheshi, muungwana na mchapakazi hodari ambaye anatuachia pengo kubwa sana klabuni.
Mbembe alipata maradhi ya kupooza yaliyomsumbua kwa kipindi kirefu taratibu tangia June mwaka jana ambapo alipumzika kufanya kazi Azam FC Novemba mwaka jana ili kupata matibabu zaidi ambapo Klabu ya Azam FC na familia ya Mbembe kwa pamoja tulihangaika bila mafanikio. mwenyezi mungu alitoa na yeye ndiye aliyetwaa... Tunamuombea dua marehemu roho yake ipumzike mahala pema peponi. Amin

pichani Mbembe kushoto mwenye ndevu na koti jeusi akiwa na Katibu mkuu wa Azam FC Nassor Idrissa na kocha msaidizi Kally Ongala nchini Rwanda






 
150542_431592873555737_540049480_n.jpg
 
[h=5]Tuhuma zinazowakabili wachezaji wetu wanne zimekabidhiwa kwa chombo cha Serekali cha kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU, kisheria na kwa taratibu tuhuma zikikabidhiwa kwenye chombo husika kupisha uchunguzi, ni busara kwa watuhumu kukaa kimya ili kuwapa nafasi TAKUKURU wafanye kazi yao kwa uweledi. Azam FC inawaomba wapenzi na mashabiki wake kuvuta subira wakati wa kipindi hiki kigumu wakisubiri ripoti ya uchunguzi toka TAKUKURU.

Imetolewa na ofisi ya utawala
Azam FC
TANGAZO, Taarifa ya RUSHWA yakabidhiwa TAKUKURU kwa uchunguzi zaidi | The Official Website of Azam Football Club[/h]
 
FT mgambo Jkt 2 - 1 azam fc

mzunguko ndivyo ulivyoisha..
 
Wadau na mashabiki wa mpira Tanzania na pia wa timu ya Azam FC wakitoa maoni yao juu ya juhudi za Azam FC kuweka mikakati endelevu kati soka ili Tanzania ingare ktk soka barani Afrika.

Timu kongwe kama Young Africans (Yanga) na Simba SC ni timu zenye mtizamo wa ndani ya Tanzania kimafanikio lakini timu hizo kongwe hazijaweza kujikita ktk ramani ya bara la Afrika kama timu za kuogopwa na kutwaa vikombe vya mashindano barani Afrika.

Endelea kusikiliza maoni ya juhudi za Azam FC kubadilisha hali hiyo:


Source: video ya mdau : Khaleed mohd wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Azam FC wiki iliyopita iliwapeleka India kwa uchunguzi na matibabu wachezaji watatu wa timu yetu ya vijana na mmoja wa timu ya wakubwa, waliosafiri ni Viungo Ibrahim Rajab Jeba & Ryna Mgungila, Beki wa Kulia Deogratium Nemes, na mshambuliaji Ahmed Abbas Machupa, Azam FC inawatakia kila la kheri waweze kupata matibabu na kurejea nyumbani kujifunza na kuitumikia Azam Academy na Azam FC
 
Back
Top Bottom