The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

[h=3]AZAM KUSAJILI WAKENYA WATATU - KUJIIMARISHA LIGI KUU RAUNDI YA PILI NA MICHUANO YA KIMATAIFA[/h]
Katika kujiimarisha kwa ajili ya michuano ya kimataifa na ligi kuu ya Tanzania raundi ya pili, klabu ya Azam FC imetajwa kuwa katika mazungumzo na wachezaji watatu kutoka Sofapaka ya Kenya.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa chanzo kilicho karibu na Azam ambayo wiki iliyopita waliwasimamisha wachezaji wao wanne, Dida Munishi, Said Morad, Aggrey Morris na Erasto Nyoni kwa tuhuma za kupokea rushwa, kimesema majina ya wachezaji watatu kutoka Sofapaka ni Eugene Ambuchi Asike, James Situma na Humphrey Mieno

Wachezaji hao watatu wa kikenya inasemekana ni kocha Stewart Hall ndio aliyetoa maombi ya kusajiliwa kwa wachezaji hao ambao alifanya nao kazi wakati akiwa kocha wa Sofapaka baada ya kutimuliwa Azam FC miezi kadhaa iliyopita.
 
November 23, 2012
Dar-es-Salaam, Tanzania.

Kocha Stewart Hall ( http://en.wikipedia.org/wiki/Stewart_Hall_(football_coach) wa Azam FC azungumzia mzunguko wa kwanza wa ligi ya Tanzania bara na mkakati wake mzunguko wa pili na pia tofauti ya ligi ya soka Kenya na Tanzania ktk kipindi cha AZAM FC TV :


source: khaleed mohd wa youtube
 
Last edited by a moderator:
November 23, 2012
Dar-es-Salaam, Tanzania.

Kocha Stewart Hall ( http://en.wikipedia.org/wiki/Stewart_Hall_(football_coach) wa Azam FC azungumzia mzunguko wa kwanza wa ligi ya Tanzania bara na mkakati wake mzunguko wa pili na pia tofauti ya ligi ya soka Kenya na Tanzania ktk kipindi cha AZAM FC TV :


source: khaleed mohd wa youtube


Stewart Hall bonge la kocha, yeye, Bob Williamson na Micho.
Achana na hawa wauza matikiti...
 
Last edited by a moderator:
[h=5]David John Mwantika, beki kisiki wa Tanzania Prisons anakuwa beki wa tatu kusajiliwa na Azam FC baada ya Malika Ndeule na Omary Mtaki, hawa wanaungana na Uhuru Selemani na kufanya jumla ya wachezaji waliosajiliwa na Azam FC kufikia wachezaji wanne. zoezi bado linaendelea... Stay Tunned[/h]source: azam fc
 

Siku chache baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kutoka timu ya Simba na kujiunga na Azam FC, kiungo mshambuliaji wa pembeni, Uhuru Seleiman Mwambungu, ameelezea mikakati yake mipya katika soka lake. Uhuru ambaye alishinda ubingwa wa Tusker Cup, akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar, mwaka 2009 na mataji mawili ya ligi kuu katika miaka yake mitatu na nusu kama mchezaji wa Simba, ameondoka klabuni, Simba uku akiwa si mchezaji muhimu kama mwanzo, mara nyingi amekuwa benchi na hata alipotumika ilikuwa ni kwa muda mchache tu. Tovuti ya kandanda, ilifanya mahojiano na kiungo huyu.
kandanda-jibu.png
kandanda-jibu.png
kandanda-jibu.png
kandanda-jibu.png
kandanda-jibu.png
kandanda-jibu.png

[TD="width: 64, bgcolor: #F7F7F7"]
kandanda-swali.png
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"] Hali ilikuwaje kwa upande wako katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu, Tanzania Bara?[/TD]

[TD="width: 469"]Ilikuwa mbaya, sababu mimi ni mchezaji nisiyependa kubaki nyuma, yaani kukaa bila kucheza. Alafu timu inafanya vibaya, zaidi nilichukia kabisa mpira. Ila sasa nitarudi katika kiwango changu, na ningependa Milovan ( aliyekuwa kocha wa Simba) awepo Tanzania.[/TD]

[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
kandanda-swali.png
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Unadhani, Milovani ndiye alikuwa tatizo kwako? Labda wewe hukuwa ukitimiza majukumu aliyokuwa akitaka uyafanye na ukashindwa ndiyo maana akawa anakuacha nje?[/TD]

[TD="width: 469"]OK, ni hivi akili yangu haipo tena Simba na sitaki kuwaza kuhusu niliyokutana nayo uko ( Simba). Sasa naangalia ni vipi nitashirikiana na wenzangu katika timu yangu mpya ( Azam).[/TD]

[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
kandanda-swali.png
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Nini ambacho kilikufanya kufikiria kujiunga na Azam na si timu nyingine mara baada ya kuamua kuachana na Simba?[/TD]

[TD="width: 469"]Azam ni timu yenye malengo. Naamini itafanya vizuri, kikubwa nimeangalia nafasi ya kucheza katika mashindano ya kimataifa.[/TD]

[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
kandanda-swali.png
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"] Kama ni nafasi ya mashindano ya kimataifa, Simba pia itacheza na kama ni nafasi ya kucheza kikosini, mbona umekwenda kujirundika katika mkusanyiko mkubwa zaidi wa nafasi ndani ya Azam?[/TD]

[TD="width: 469"]Unapokuwa mchezaji, hilo si jambo la kujadili. Muhimu ni kuungana na wachezaji uliowakuta na kufanya kazi kwa pamoja. Mwalimu ndiye ataamua nani amtumie katika wakati upi.[/TD]

[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
kandanda-swali.png
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Kwa uzoefu wako wa kuzichezea timu kubwa kama Mtibwa na Simba na kushinda mataji, unadhani itakuwa hivyo pia kwa Azam?[/TD]

[TD="width: 469"]Naamini, Azam ni timu bora na imejipanga kufanya mapinduzi katika soka letu, hivyo kwa kushirikiana na wenzangu, nitafanya kila jitihada kuifanya, Azam kuchukua nafasi za juu katika mashindano ya Afrika na ligi kuu, ambayo naamini sasa utakuja kwetu.[/TD]

[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
kandanda-swali.png
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Timu nyingi zimeshindwa kuzipiku, Simba na Yanga na kutwaa taji la ligi, Mtibwa ilikuwa ni timu ya mwisho kufanikiwa kutwaa taji hilo mwaka 1999 na kurudia mwaka 2000, unadhani, Azam itazipiku timu hizo na kutwaa taji?[/TD]

[TD="width: 469"]Najua, Simba na Yanga ndiyo zinaisumbua, Azam, lakini mimi ninayo dawa yao na ninaijua.[/TD]

source:kandanda.co.tz
 
Azam FC inatarajia kuelekea Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 13 hadi 23 December kushiriki mashindano ya Ngao ya Jamii (Charity Cup) Mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu kubwa za kutoka Kongo kama DCMP na AS Vita Club timu kutoka nje ya kongo kama Azam FC, Tusker FC, Gombe United ya Nigeria na Diable Noirs na Congo Brazavile yatatumika na Azam FC kama maanadalizi ya Confederations Cup Azam FC inahitaji maandalizi na mechi nyingi za kirafiki nje ya Tanzania ili
kupata uzoefu kabla ya kushiriki
Confederations Cup.
Kwa maana hiyo hii ni nafasi muhimu sana kwa Azam FC.
Chanzo: Ukurasa wao wa Facebook
 
mkuu ndetichia hujambo azam mnavyo komaa lakini mjue nafasi yenu mwaka huu ni ya tatu..
 
Last edited by a moderator:
Mwenyekiti wa AZAM FC ndugu Said Moh'd na pia mchezaji wa kulipwa wa AZAM FC toka Cote D'Ivoire, Kipre wafanya mahojiano na AZAM FC TV .

Mwenyekiti wa Azam Fc anaweka wazi visheni na historia timu tangu kuanzishwa mwaka 2004 mpaka sasa na kuwa mpira ni sayansi na masuala ya sayansi yanaenda kimpangilio, wadau tuendelee kusikiliza mahojiano;


Video kwa hisani ya Khaleed Mohd wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Mwenyekiti wa AZAM FC ndugu Said Moh'd na pia mchezaji wa kulipwa wa AZAM FC toka Cote D'Ivoire, Kipre wafanya mahojiano na AZAM FC TV .

Mwenyekiti wa Azam Fc anaweka wazi visheni na historia timu tangu kuanzishwa mwaka 2004 mpaka sasa na kuwa mpira ni sayansi na masuala ya sayansi yanaenda kimpangilio, wadau tuendelee kusikiliza mahojiano;


Video kwa hisani ya Khaleed Mohd wa youtube


thanks man kwa updates...
 
Last edited by a moderator:
[h=5]Azam FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.
El-Mereik wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.
Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.
Meng
i yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa.
Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.
Azam FC inamuuza Mrisho Ngasa kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya mchezaji mwenyewe kimpira na kwa kipato, pia kwa kuzingatia kwamba Tanzania inahitaji wachezaji wengi wanaocheza nje kwenye vilabu vikubwa ili wanaporudi waweze kuisaidia timu ya Taifa.
Imetolewa na Utawala

Ngasa atua Ell Mereikh kwa $75,000 | The Official Website of Azam Football Club

[/h]
 
[h=5]Azam FC imeandika barua TFF leo ikiwaomba wamruhusu Ngasa kwenda Sudan baada ya mchezo for medical test with Mareikh nakala imeenda kwa simba

Msukumo uliotufanya tuandike barua hii ni kwa kutambua kuwa hii ni nafasi muhimu kwa ngasa na Taifa kwani anakwenda kucheza kwenye timu yenye uwezo na miundombinu kama barani Afrika na inayoshiriki ligi ya mabingwa Afrika karibu kila msimu kitu ambacho kitamuongezea Ngasa kiwango na kuwa na msaada kwa Tafa

Pia tunapenda kuweka wazi Value ya Signing Fees na Mshahara ambao Ngasa atapewa na Elmereikh ambao ni $4000 (Shilingi Milioni 6 kwa mwezi kwa miaka miwili takribani 144 Milioni) na Signing Fees $ 50,000 Milioni 80 kwa hiyo Ngasa ataweka kibindoni zaidi ya shilingi milioni 230 kwa miezi 24... hizi ni pesa nyingi kwa mchezaji wa kitanzania kwa maendeleo ya mchezaji na Familia yake na yatawapa msukumo vijana wengi wenye kipaji kama Ngasa kufanya bidii kwenye soka na kuliletea maendeleo taifa.

Azam FC inaomba TFF imruhusu Ngasa kwenda Sudan akitokea Uganda kwenda kukamilisha vipimo vya Afya na usajili na Azam FC ipo tayari kukaa na simba na kuzungumza juu ya uhamisho huu kwa usimamizi wa TFF.


hapa ieleweke kuwa ingawa Azam FC inajua haki zake kisheria lakini pia imeamua kupunguza msimamo wake kukubali mazungumzo kwa kuangalia zaidi athari ambazo mchezaji anaweza kupata kimaslahi na kimaendeleo ya uchezaji wake na mpira wa Tanzania kwa ujumla kutokana na mgogoro huu.
[/h]
Chanzo: Facebook Page ya Azam FC
 
Azam wanatumia facebook na website yao kuweka habari, lakini hawaiandikii TFF. Azam bwana!
 
Kwa habari toka kwenye Facebook account ya Azam FC na tweeter Yao ni Kuwa mshambuliaji wa Uganda Cranes Brian UMONY ametua Azam ingawa bado hawajaweka ni Mkataba wa muda gani na wa KIASI gani.... Je is this right move kwa Azam au yaleyale ya kuleta maproo mizigo?

kwa hisani Pukudu
 
Last edited by a moderator:
FC Wachezaji wa Azam FC wanaosafiri leo kuelekea Kinshasa DRC ni
HERMAN/KIPRE TCHETCHE
RASHID/ABDALLAH SEIF
MICHAEL/KIPRE BOLOU
PAZI/ZAHORO IDDI
WANDWI/JACKSON
NDEULE/MALIKA PHILIP
MWAMBUNGU/UHURU SELEMANI MTAKI/OMARI MSAFIRI
STIMA/JABIR AZIZ
MWAIPOPO/IBRAHIM
MWAIKIMBA/GAUDENCE
SADALA/ABDI KASSIM
KAKOLAKI/LUCKSON
NUHU/SAMIH
MWADINI/ALLY MWADINI
MKAMI/HIMID MAO
MWANTIKA/DAVID JOHN
OMAR/WAZIRI SALUM
JOCKINS/ATUDO
HUMPHREY/MIENO
VIONGOZI
IDRISSA/NASSOR
MAPWISA/ABUBAKAR ONGALA/KALIMANGONGA
GOMES/PAULO
ABUBAKAR/IDDI
NZAWILA/YUSUPH
HALL/STEWART JOHN
SAID/JEMEDARY

chanzo: Facebook azam fanpage..
 
Maneno ya yusuf bakhressa; Mrisho ngasa atajijutiya maisha yake. Mimi ndo niliye
kuwa wakala wake ila alivyofanya na kusema uwongo
kwa viombo vya habari kukataa kama hajahusishwa
ni uwongo. Mimi kwanzia leo nimejitowa kuwa wakala
wake ili watu wajuwe. Yenye mwenyewe ndo aliyetaka
na kanipigiya simu mimi nimshughulikie. ila kwa kunifedhehesha mimi mungu ndo atanilipiya. Mimi
nilichotaka nione maisha yake yafanikiwe. Na nafurai
mimi binafsi nikiona watanzania wanacheza nje ili
waje kusaidia taifa letu. Leo hii sisi tutafika vipi kama
mtu anamruka wakala wake na kusema uwongo. Mimi
sipendi kuongeya kwenye habari ila nimependa kupost hii watu wa mpira ndo watanielewa.
 
Maneno ya yusuf bakhressa; Mrisho ngasa atajijutiya maisha yake. Mimi ndo niliye
kuwa wakala wake ila alivyofanya na kusema uwongo
kwa viombo vya habari kukataa kama hajahusishwa
ni uwongo. Mimi kwanzia leo nimejitowa kuwa wakala
wake ili watu wajuwe. Yenye mwenyewe ndo aliyetaka
na kanipigiya simu mimi nimshughulikie. ila kwa kunifedhehesha mimi mungu ndo atanilipiya. Mimi
nilichotaka nione maisha yake yafanikiwe. Na nafurai
mimi binafsi nikiona watanzania wanacheza nje ili
waje kusaidia taifa letu. Leo hii sisi tutafika vipi kama
mtu anamruka wakala wake na kusema uwongo. Mimi
sipendi kuongeya kwenye habari ila nimependa kupost hii watu wa mpira ndo watanielewa.

tatizo wale pro niniliu ndio tabu kabisa kazi ipo tz maana wachezaji wetu hawajielewi babu...
 
Back
Top Bottom