The Official Azam FC Thread

The Official Azam FC Thread

WASHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Nigeria, wanaochezea timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Rafael Chukwu na Muri Ibrahim wanatarajiwa kuwavaa Azam leo katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa itakayochezwa kwenye Uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo. Wachezaji wengine wa kulipwa wa Mamelodi Sundowns ambao watakaonekana katika mechi hiyo ni mshambuliaji Muivory, Frank Guela na Mnigeria kiungo Muis Ajao.

Azam FC ambayo imeweka kambi ya wiki mbili katikati ya jiji katika Hotel ya Randburg Tower, inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, itaanza kucheza na Yanga Agosti 17, mwaka huu, ikiwa ni mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall anatarajia kuwatumia washambuliaji wake, John Bocco, Khamis Mcha, Abdalla Seifa Karie na Kipre Tchtechte ili waweze kuibuka na ushindi baada ya kupoteza kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Kaizer Chiefs. Mechi hiyo iliyochezwa Jumatatu wiki hii, kwenye Uwanja wa mazoezi wa Kaizer Chiefs Sport Village uliopo eneo la Naturena, Azam FC ilifungwa mabao 3-0.

Azam FC jana iliendelea na mazoezi makali katika viwanja wa Wits kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo, iliyopangwa kuchezwa kuanzia saa tisa jioni kwa saa za hapa. Wachezaji wa timu hiyo, walifanya mazoezi kwa muda wa saa tatu chini ya Kocha wao, Stewart ambaye alionekana kuwa makini katika kuwafua washambuliaji wake. Stewart alitumia mazoezi hayo kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi ya kwanza dhidi ya Kaizer Chiefs baada ya kufungwa na timu hiyo.

http:// The Official Website of Azam Football Club | Tucheze pamoja kwa furaha /news/ club- news/2013/ 08/07/ azam-fc-kuwavaa- mamelodi- sundow ns-leo.html
 
Azam fc imeshinda gemu yake huko afrika ya kusini..

FT Mamelodi Sundowns 0 - 1 Azam FC Mwaikimba..
 
Azam fc imeshinda gemu yake huko afrika ya kusini..

FT Mamelodi Sundowns 0 - 1 Azam FC Mwaikimba..

Ndetichia, Asante kwa taarifa hii nzuri ya pre-season matches za Azam FC naona tunaelekea kuzuri. Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na wenyeji ndiyo waliotawala zaidi mchezo kipindi hicho, ingawa Azam walifanikiwa kutengeneza nafasi nzuri zaidi ya kufunga.

Khamis Mcha ‘Vialli’ aliingia vizuri ndani kutokea pembeni kushoto hadi ndani ya eneo la hatari na akampa pasi ya ‘hapa kwa hapa’ John Bocco ‘Adebayor’ akiwa anatazamana na lango, lakini akapiga juu ya lango dakika ya 43.

Kipindi cha pili Azam waliingia kwa ari mpya na kufanikiwa kuuteka mchezo hali ambayo ilisababisha wafanye mashambulizi mengi langoni mwa Mamemlodi.

Almanusra Bocco afunge dakika ya 65 kama si kichwa chake kupaa juu ya lango kufuatia krosi maridadi ya Kipre Herman Tchetche.

Mamelodi walijibu shambulizi hilo dakika ya 70 na shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 19 lililopigwa na Jabu Shongwe liligonga nguzo ya juu ya lango na kurejea uwanjani kabla ya Said Morad ‘Mweda’ kuondosha kwenye hatari.

Katika dakika ya 74, Mwaikimba aliyeingia uwanjani dakika ya 64 kumpokea Bocco aliunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya beki Joackins Atudo kutoka wingi ya kulia, ambaye pia alitokea benchi kipindi cha pili kuipatia Azam bao pekee kwenye mchezo wa leo.

Dakika ya 89 Mwaikimba alikaribia tena kufunga kama si shuti lake kupaa juu ya lango akiwa ndani ya eneo la hatari kufuatia krosi nzuri ya Tchetche.

Baada ya mchezo huo, kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall alifurahia matokeo na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake na pia akasifu ushindani ulioonyeshwa na wapinzani.

Kwa upande wake, Pitso Masomane kocha wa Mamelodi alisifu Azam na akasema kwa soka waliyoonyesha hastaajabu kwa nini wameshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu. Source: JAIZMELALEO: AFRICA NEWS: AZAM FC YAIZABUA MAMELODI SUNDOWNS Website ya Mamelodi Sundowns FC: Landing Page | Mamelodi Sundowns
 
Leo Huko South Afrika

Orlando Pirates 2 - 1 Azam FC

aliyeifungia azam ni Jabir Aziz Stima
 
Klabu 13 zajazwa `minoti` ya Azam Tv

NA SOMOE NG`ITU 8th August 2013

Hatimaye kampuni ya Azam Media imezikabidhi klabu 13 za Ligi Kuu ya Tanzania Bara mamilioni yao yote ya awamu ya kwanza ya fedha zinazolipwa na kampuni hiyo iliyopewa haki ya kuonyesha ‘live’ mechi zote za ligi kuu kuanzia msimu ujao. Mgawo uliotolewa jana ni wa Sh. milioni 25 kwa kila timu, sawa na asilimia 25 ya Sh. milioni 100 ambazo zitalipwa na Azam TV kwa kila klabu ili kuonyesha mechi zao kwenye televisheni.

Timu hizo 13 zilizopata mgawo wa Sh. milioni 25 ni Simba, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Azam, Coastal Union, Mbeya City, Ashanti, Rhino, JKT Oljoro, JKT Ruvu, JKT Mgambo, Tanzania Prison na Ruvu Shooting. Akizungumza na NIPASHE jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Wallace Karia, alisema kuwa zoezi la kuziweka fedha hizo katika akaunti za klabu lilifanyika jana mchana na sasa viongozi wa timu hizo watakuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea na maandalizi.

Karia alisema kwamba wanaipongeza kampuni hiyo kwa kuanza kutekeleza kivitendo makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wao na wanaamini kuwa kwa kasi hiyo, hatimaye ushindani utakuwa mkali katika ligi kuu kuanzia msimu ujao. "Tayari klabu 13 tumeshaziwekea fedha za udhamini wa Azam, leo (jana) asubuhi walituwekea katika akaunti ya bodi ya ligi na sisi mchana huu (jana mchana) tumeshazisambaz a kwa klabu zote isipokuwa Yanga," alisema Karia. Aliongeza kuwa wanazitaka klabu kuzitumia vyema fedha hizo na kukamilisha malengo ya kuendeleza timu.

"Tunajua bado wako katika maandalizi ya kuanzisha televisheni yao lakini kwa kutangulia kutupa fedha kwetu ni faraja na ndiyo makubaliano yalivyokuwa kwenye mkataba," aliongeza kiongozi huyo. Alisema kwamba awamu ya pili ya fedha za udhamini huo itatolewa kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza Novemba 3 mwaka huu na kwa msimu mmoja kila timu itapata Sh. milioni 100. Alizikumbusha klabu hizo kuhakikisha kwamba zinakamilisha maandalizi ya msingi ili kushiriki ligi hiyo na si kuangalia zoezi la usajili wa wachezaji na makocha peke yake.

"Bima za wachezaji ni suala muhimu lililopo katika kanuni na msimu huu hatutakubali kuona ubabaishaji unafanyika kama ilivyokuwa huko nyuma. Tunataka kuwa na ligi bora, hivyo kila jambo ni lazima lifuatwe ili kufikia maendeleo," aliongeza Karia. Alisema vilevile kuwa klabu zinatakiwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja ili kurekebisha kasoro zilizopo na endapo hakutakuwa na marekebisho, timu zitatakiwa kuhama viwanja walivyovichagua .
http:// www.ippmedia.com /frontend/ index.php? l=5796 4
 
Leo Huko South Afrika

Orlando Pirates 2 - 1 Azam FC

aliyeifungia azam ni Jabir Aziz Stima
Tukirudi zetu huko (S A) Yanga watatueleza kwanini wanakataa fedha zetu?, lazima tuanze kuchukua ngao kwanza arafu tunamalizia na kombe lenyewe kabisaa (ligikuu)
 
Keho gemu ya mwisho south afrika halafu tunarudi zetu homu..
 
Tukirudi zetu huko (S A) Yanga watatueleza kwanini wanakataa fedha zetu?, lazima tuanze kuchukua ngao kwanza arafu tunamalizia na kombe lenyewe kabisaa (ligikuu)

kweli mkuu..
 
Kikosi cha Leo
1 Aishi Manula
2 Erasto Nyoni
3 Waziri Salum
4 Saidi Moradi
5 Aggrey Morris
6 Himid Mao
7 Ibrahimu Mwaipopo
8 Jabir Aziz
9 Gauedence Mwaikimba
10 Kipre Tchetche
11 Khamis Mcha

Kila la kheri azam fc
 
Full Time: Azam FC 0 - 1 Moraka swallows
Kwama tokeo haya bado timu yetu ni mzuri tena imeonyesha uhai wa kutosha, tofauti nawale wanaopambana na mchangani fc kisha wanajisifu kwakushindana nyingi.

Força AZAM a luta continua.
 
[h=3]AZAM KUREJEA LEO KUTOKA BONDENI[/h]

Makamu bingwa wa Tanzania bara na bingwa wa kombe la Mapinduzi Azam fc wanataraji kurejea nchini hii leo wakitoka Afrika kusini 'Bondeni' walipokuwa na kambi ya mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania bara.Azam fc wakiwa Afrika kusinu kwa takribani wiki moja na nusu wamecheza michezo 4 ya kirafiki ambapo katika michezo hiyo wameshinda mchezo mmoja na kufungwa yote mitatu iliyo salia.
Wachezaji wote wa azam fc wanaotarajiwa kuiwakilisha timu hiyo katika ligi kuu ya vodacom walikuwepo Afrika kusini isipokuwa kiungo wa Kenya Humphrey Mieno na mshambuliaji toka Uganda Brian Umonyi.
Azam fc wanataraji kushuka uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam agusti 17 kuwakabili yanga katika mchezo wa ngao ya jamii. Mchezo utakao ashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
Azam fc baada ya mchezo huo wa ngao ya jamii, wataelekea mkoani Morogoro kuwakabili wakatamiwa wa Turiani Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom msimu wa 2013/14.
 
Kwama tokeo haya bado timu yetu ni mzuri tena imeonyesha uhai wa kutosha, tofauti nawale wanaopambana na mchangani fc kisha wanajisifu kwakushindana nyingi.

Força AZAM a luta continua.

Jumamosi njoo Taifa utapata jibu lako. Tunapambana na adui siyo mtani kama Simba hivyo ni lazima Azam wanyee kitanda kama siyo kukikojolea.
 
Back
Top Bottom